image

Dalili za UTI

Somo hili linakwenda kukuletea dalili za UTI

Dalili za UTI

1.Kukojoa mara kwa mara

2.Kuhisi kuunguwa ama umoto wakati wa kukojoa

3.Kutoa mikojo kwa uchache

4.Mkojo kuwa mchafu, kama mawingu ama mwekundu uliopauka

5.Harufu kali ya mkojo

6.Maumivu ya kwenye njonga kwa wanawake

7.Maumivu ya mkundu na puru kwa wanaume.

 

Dalili za UTI zinaweza pia kuwa tofauti na hizo hapo juu. Dalili hizi hutofautiana kwa kulingana na aina ya UTI. Kama unataka kuzijuwa dalili zaidi za UTI endelea kusoma makala hii mpaka mwisho.

 

Aina za UTI na dalili zake.

Ugonjwa wa UTI umegawanyika katika makundi mbalimbali. Makundi hayo ni kama:-

1.UTI ya kwenye figo (acute pyelonephritis). UTI hii huathiri figo, na kusababisha dalili kama:-

1.Maumivu ya mgongo kwa juu

2.Homa kali

3.Kuhisi baridi na kutetemeka

4.Kichefuchefu

5.Kutapika.

 

2.UTI ya kwenye kibofu (cystitis). hii ni aina ya UTI ambayo huathiri kibofu cha mkojo. Dalili zake ni:-

1.Maumivu ya nyonga

2.Maumivu ya tumbo kwa chini ya kitovu ama mvurugiko wa tumbo kwa chini

3.Kukojoa mara kwa mara huku ukiwa na maumivu.

4.Kukojoa damu, ama mkojo wenye rangi nyekundu ya kupauka.

 

3.UTI ya kwenye mrija wa mkojo (urethritis). mrija wa mkojo kitaalamu unaitwa urethra. Huu ndio mrija unaotoa mkojo kutoka kwenye kibofu na kuuleta nje. Dalili za UTI hii ni kuhisi kuunguwa wakati wa kukojoa.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1994


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Presha ya kushuka na matibabu yake
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu presha ya kushuka na matibabu yake Soma Zaidi...

Fahamu matatizo ya ini kuwa na kovu
kovu (Fibrosis) ya ini inayosababishwa na aina nyingi za magonjwa na hali ya ini, kama vile Homa ya Ini na unywaji pombe kupita kiasi. Ini hufanya kazi kadhaa muhimu, ikiwa ni pamoja na kuondoa vitu vyenye madhara katika mwili wako, kusafisha damu yako Soma Zaidi...

Njia za kugundua tatizo la kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu
Post hii inahusu Zaidi njia mbali mbali ambazo uweza kitumiwa na wataalamu ili kuweza kugundua tatizo la kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu. Soma Zaidi...

Dalili za ugonjwa wa herpes simplex au vipele kwenye midomo na sehemu za siri
Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa wa vipele kwenye midomo na sehemu za siri ambao kwa kitaalamu huitwa herpes zoster. Kwa hiyo ili kugundua kubwa mtu ana Ugonjwa huu Dalili kama hizi zifuatazo zinaweza kutokea kwa mgonjwa. Soma Zaidi...

Dalili za minyoo mviringo (ascariasis)
Ascariasis ni aina ya maambukizi ya minyoo mviringo. Minyoo hii ni vimelea wanaotumia mwili wako kama mwenyeji kukomaa kutoka kwa mabuu au mayai hadi minyoo wakubwa. Minyoo ya watu wazima, ambayo huzaa, inaweza kuwa zaidi ya futi (sentimita 30) kwa Soma Zaidi...

Dalili za kisukari na njia za kuzuia kisukari
Posti hii inaelezea ugonjwa wa kisakari, dalili zake,na namna ya kujikinga usipate kisukari au Kama tayari unakisukari ukijikinga madhara yanapungua au kupona kabisa.Kisukari au bolisukari (jina la kitaalamu: diabetes mellitus) ni ugonjwa unaoonyesha viwa Soma Zaidi...

Ujuwevmv ugonjwa Nimonia na dalili zake
Nimonia ni Hali ya kuvimba pafu inayoathiri hasa vifuko vya hewa viitwavyo Alveoli, husababishwa na Maambukizi ya virusi Soma Zaidi...

ujuwe ugonjwa wa gout na athari zake mwilini
Post hii itakwenda kuzungumzia ugonjwa wa gout unaosababishwa na ongezeko la asidi mwilini. Soma Zaidi...

Dalili za Ugonjwa wa ini
Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa inni, hizi ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye ugonjwa wa inni, Dalili zenyewe ni kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

Matatizo yanayosababisha saratani ya mapafu
Posti hii inaonyesha matatizo yanayosababisha saratani ya mapafu . Soma Zaidi...

fangasi wa kwenye Mdomo na koo
Soma Zaidi...

Samaani nilikuwa nauriza ninasumburiwa na fanga ya mdomoni naomba ushauri
Fangasi mdomoni wanaweza kuwa tatizo endapo hawatatibiwa mapema. Wanaweza kuongeza majeraha kwenye kinywa. Soma Zaidi...