image

Dalili za vidonda vya tumbo

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za vidonda vya tumbo

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO

 

 

Vidonda vya tumbo huweza kutokea ndani ya tumbo kutokana na mashambulizi ya bakteria aina ya H.pylori, ama kutokana na athari za madawa flani ama mashambulizi ya wadudu wengineo ama kwa sababu ya ugonjwa wa saratani. Makala hii inakwenda kukuletea dalili duu za vidonda vya tumbo.

 

1.Maumivu ya tumbo; hii pengine ndio katika dalili kuu zaidi ambazo wengi wenye vidonda vya tumo wanaipata. Maumivu haya yanawza kuwa makali sana wakati mgonjwa akiwa na njaa.Tumbo hili ni tofauti na tumbo la ngiri ama chango. Maumivu haya yanaweza kuanzia chini ya kitomvu na kupanda juu hadi kifuani. Maumivu haya yanaweza kufuatana na dalili zifuatazo hapo chini.

 

2.Tumbo kujaa; tumbo linaweza kujaa gesi hata akashindwa kula vyema. Huenda mgonjwa akajihisi ameshiba badala ya kuka kidogo. Uhalisia si kwamba ameshiba ila tumbo ndio limejawa na gesi.

 

3.Kukosa hamu ya kula; hii ni katika dalili ya hatari sana, maana umuhimu wa chakula unafahamika vyema. Mgonjwa anaumwa na tumbo na anakosa kabisa hamu ya kula pia anahisi tumbo kujaa.

 

4.Kupata kiungulia cha mara kwa mara. Kiungulia unaweza kukitibu kwa kutumia dawa, kwani hazina tabu kwa vidonda vya tumbo. Pia unaweza kulamba majivu, hii ni tiba mbadala ambayo inatumka kutibu kiungulia. Lakini epuka kula vyakula vyenye gesi.

 

5.Kupungua uzito; vidonda vya tumbo vinaweza kusababisha mtu kupungua uzito, bila ya kujuwa sababu maalumu. Inaweza kuwa ni kutokana na kutokula kwake kwa sababu ya kukosa hamu ya kula.

 

6.Kichefuchefu na kutapika. mgonjwa wa vidonda vya tumbo wakati mwingine anapata kichefuchefu kisicho na sababu maalumu. Hali hii inaweza kumpelekea akatapika ama asitapike. Na wakati mwingine anaweza kuona dmau kwenye matapishi yake.

 

7.Mapadiliko kwenye kinyesi. Mgonjwa anaweza kuona mabadiliko kwenye rangi ya kinyesi chake. Kinaweza kuwa cheusi sana na chenye harufu mbaya sana. Na wakati mwingine kinaweza kuwa na damu.

 

 

Masharti kwa mwenye vidonda vya tumbo.

 

 

Makala hii inakwenda kukuletea masharti yanayompasa mwenye vidonda vya tumbo ayafate. Je ni vyakula gani vinafaha sana kwa mwenye vidonda vya tumbo?

Masharti ya vidonda vya tumbo

1.Punguza ama wacha kabisa unywaji wa pombe

 

2.Punguza misongo ya mawazo

 

3.Epuka vyakula vyenye gesi kama baadhi ya aina za maharagwe

 

4.Hakikisha unakula kwa wakati.

 

5.Epuka kukaa na njaa kwa muda mrefu

 

6.Epuka matumizi ya madawa ya aspirin na jamii za madawa hayo. Kama ni lazima utumie madawa mbalimbali na ya mchanganyiko hasa yale ya kuzuia maumivu, basi kwanza zungumza na daktari akupe maelekezo.

 

7.Punguza ama wacha kabisa uvutaji wa sigara

 

8.Hata kama hutakuwa na hamu ya kula jilazimishe ule ama tumia dawa za kuongeza hamu ya kula.

 

9.Epuka vyakula vyenye mafuta kwa wingi.

 

10.Kunywa maji mengi ya ya kutosha kila siku

 

11.Onana na daktari mara kwa mara unapohisi mabadiliko ya hatari mwilini mwako.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1869


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Kiungulia, dawa yake na namna ya kuzuia kiungulia
Tambuwa kiungulia, sababu zake, dawa za kiungulia na namna ya kupambana na kiungulia Soma Zaidi...

Fahamu Ugonjwa wa mshtuko wa sumu.
Ugonjwa wa Mshtuko wa Sumu ni matatizo ya nadra, yanayotishia maisha ya aina fulani za maambukizi ya bakteria. Mara nyingi ugonjwa wa mshtuko wenye sumu hutokana na sumu zinazozalishwa na bakteria. Soma Zaidi...

Ufahamu Ugonjwa wa hepatitis B
Hepatitis B Ni maambukizi ya ini ambayo yamekuwa sugu kuanzia mwezi na kuendelea. Soma Zaidi...

Dalili za maumivu ya uti wa Mgongo
Posti hii inahusu zaidi dalili za uti wa mgongo ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye tatizo la uti wa Mgongo. Soma Zaidi...

DALILI ZA HOMA YA BONDE LA UFA (RVFD) NA INAVYOSAMBAZWA.
Homa hii inapatikana katika maeneo ya bonde la ufa barani Afrika na na Mashariki ya kati. Soma Zaidi...

DAWA MBADALA ZA VIDONDA VYA TUMBO
DAWA MBADALA ZA VIDONDA VYA TUMBO Dawa za kukabiliana na zaidi ambazo zina calcium carbonate (Tums, Rolaids), zinaweza kusaidia kutibu vidonda vya tumbo lakini hazipaswi kutumiwa kama matibabu ya msingi. Soma Zaidi...

Dalili za sukari kupungua mwilini (Hypoglycemia)
sukari kupungua mwilini (Hypoglycemia) huhusishwa kwa kawaida na matibabu ya Kisukari. Hata hivyo, hali mbalimbali, nyingi zikiwa nadra, zinaweza kusababisha sukari ya chini ya damu kwa watu wasio na Kisukari. Kama vile Homa, Hy Soma Zaidi...

Maambukizi kwenye mfumo wa usagaji chakula unaotokea kwenye utumbo mkubwa (diverticulitis)
Posti hii inazungumzia kuhusiana na mifuko midogo midogo, iliyobubujika ambayo inaweza kuunda kwenye utando wa mfumo wako wa usagaji chakula. Wao hupatikana mara nyingi katika sehemu ya chini ya utumbo mkubwa (koloni). Hali hiyo inajulikana kama Divert Soma Zaidi...

Nini chanzo cha malaria
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu chanzo cha ugonjwa wa malaria Soma Zaidi...

Dalili za selulitis.
Selulitis ni maambukizi ya ngozi ya bakteria ya kawaida, ambayo yanaweza kuwa mbaya. Cellulitis inaonekana kama sehemu nyekundu ya ngozi iliyovimba na inahisi joto na laini. Inaweza kuenea kwa kasi kwa sehemu nyingine za mwili. Cellulitis haienei kuto Soma Zaidi...

Madhara ya kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu
Post hii inahusu Zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea Kwa mgonjwa mweye usaha kwenye mapafu. Soma Zaidi...

Masharti ya vidonda vya tumbo
Haya ni masharti ya mwenye vidonda vya tumbo. Mgojwa wa vidonda vya hatumbo hatakiwi kufanya yafuatayo Soma Zaidi...