Pisti hii inahusu zaidi dalili za mtoto mwenye Maambukizi ya ugonjwa wa Dondakoo, tunajua wazi kuwa ugonjwa huu uwashambulia hasa watoto wadogo ambao wako chini ya miaka mitano, kwa hiyo zifuatazo ni baadhi ya Dalili zinazoweza kujitokeza kwa watoto hawa.
Dalili za ugonjwa wa Dondakoo.
1. Kukoroma wakati wa kuingiza hewa.
Hii ni mojawapo ya Dalili ya kuwepo kwa ugonjwa wa Dondakoo kwa mtoto ambapo mtoto anapokuwa anaingiza hewa ndan huwa anakoroma hali hii utokea kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi kwenye koo, kwa hiyo walezi wa watoto wadogo wanapaswa kutambua Dalili hii mapema na kuchukua hatua, ingawa kukoroma kunaweza kufanana na mafua ya kawa ila kukoroma kwa maambukizi ya Dondakoo utokea pale hewa inapokuwa inaingia ndani .
2. Kiwango cha mapigo ya moyo kuongezeka.
Hii nayo ni mojawapo ya Dalili ya kuwepo kwa Maambukizi kwenye koo yanayosababishwa na bakteria kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi hasa ya mda mrefu na sehemu mbalimbali za moyo ushambuliwa ambazo ufanya mapigo ya moyo kwenda mbio na wakati mwingine kwa sababu ya kuwepo kwa homa pia usababisha mapigo ya moyo kuongezeka, kwa hiyo tunapaswa kutibu ugonjwa huu mapema ili kuepuka kuwepo kwa matatizo mengine.
3. Kuvimba kwa sehemu ya juu ya tezi.
Dalili hii ujitokeza kwa mtoto hasa hasa kama Ugonjwa umesbaa sana, matezi yanaanza kuvimba kwa sehemu ya juu, hali hii tunapaswa kuitafautisha na tonslis ambapo matezi ya chini ndo uvimba kwa hiyo tukiona tu matezi ya juu yamevimba na mtoto anashindwa kimeza vizuri moja kwa moja tunapaswa kutambua kuwa ni ugonjwa wa Dondakoo na kutafuta matibabu mara moja.
4. Vidonda kwenye koo na sauti kubwa nzito.
Kwa sababu ya Maambukizi kwenye koo, hali ya kooni ushambuliwa na kusababisha madonda ambayo uleta maumivu kwa mtoto kwa hiyo mtoto kushindwa kumeza na wakati mwingine kama ananyonya ushindwa kabisa kwa hiyo hali hii upelekea kuwepo kwa madonda ambayo usababisha sauti kubwa nzito, kama mtoto haongei utagundua pale anapolia ambapo sauti yake ibadilika kabisa, kwa hiyo walezi wanapaswa kugundua dalili hii mara moja na kupata matibabu.
5. Kupumua kwa shida na wakati mwingine kupumua haraka haraka.
Hii ni mojawapo ya Dalili ya kuwepo kwa Maambukizi kwenye koo ambapo koo linakuwa limearibiwa na bakteria na Maambukizi yanakuwa yameenea kwenye kifua ambapo kusababisha matatizo kwenye upumuaji na pengine mtoto upumua kwa haraka haraka.kwa hiyo tunapaswa kutofautisha kupumua kwa mafua ya kawaida na kupumua kwa sababu ya Maambukizi ya Dondakoo.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 3355
Sponsored links
👉1
kitabu cha Simulizi
👉2
Madrasa kiganjani
👉3
Kitau cha Fiqh
👉4
Simulizi za Hadithi Audio
👉5
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉6
Kitabu cha Afya
Dalili za presha ya kushuka
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za presha ya kushuka Soma Zaidi...
Maumivu ya kiuno na dalili zake
Posti hii inahusu zaidi maumivu ya kiuno na dalili zake, ni maumivu ambayo utokea kwenye kiuno na kusababisha madhara mbalimbali katika mwili, Soma Zaidi...
Athari za kutotibu fangasi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu athari za kutokutibu fangasi Soma Zaidi...
Huduma kwa mtoto mwenye Maambukizi kwenye mifupa
Posti hii inahusu zaidi msaada kwa mtoto mwenye Maambukizi kwenye mifupa, ni huduma anayopewa mtoto mwenye Maambukizi kwenye mifupa. Soma Zaidi...
MALARIA INATOKEAJE? (Namna ambavyo malaria inatokea, inaanza na inavyoathiri afya)
Kama tulivyokwisha kuona kuwa malaria inaweza kuambukizwa kwa kung'atwa na mbu aina ya anophelesi. Soma Zaidi...
Madhara ya fangasi.
Posti hii inahusu zaidi madhara ya fangasi za ukeni kwa kawaida tunajua kubwa fangasi zikiingia kwenye uke usababisha madhara mbalimbali ambayo mengine yanaweza ya kudumu na mengine ya mda kama yametibiwa mapema. Soma Zaidi...
Elimu kuhusu HIV na UKIMWI
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu elimu ya kuhusu HIV na UKIMWI Soma Zaidi...
Dalili za ugonjwa wa vericose veini
Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa vericose veini Soma Zaidi...
Dalili za UKIMWI
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za UKIMWI Soma Zaidi...
Ninashida Kuna mtu anaumwa pressure Kila anap pima Iko juu il mwil aumuumi at kidg n dawa anatumia unawez kunisaidiaj
Kama unasumbuliwa na presha post hii ni kwa ajili yako. Hapa tutakuoatia ushauri kutokana na swali alilouliza mdau wetu. Soma Zaidi...