image

Damu, uteute na maji yanayotoka ukeni kipindi cha ujauzito

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu damu, uteute na maji yanayotoka ukeni kipindi cha ujauzito

DAMU NA UTEUTE NA MAJIMAJI YANAYOTOKA UKENI WAKATI WA UJAUZITO:

Majimaji yanayotoka ukeni wakati wa ujauzito (Damu na uteute)Ni kawaida kwa mjamzito kushuhudia kwenye uke wake kutokwa na kama uteute na huongezeka kila mimba inapoendelea kukomaa. Wakatiflani anaweza kuona nguo zake zina madoa ya damu, ama akashuhudia matone kadhaa ya damu. Wapo pia wanaingia hedhi kwa damu chache. Sasa hebu tuangalie kwa ufupi hali hizi:-

 

1.Baada ya kutoka hedhi uke wa mwanamke unakuwa mkavu bila ya kuwa na utelezi telezi. Hiki ni kipindi ambacho mwanamke hawezi kubeba ujauzito. Katika kipindi hiki hata akitia kidole hakitoki na utelezitelezi. Kipindi hiki kinaweza kuchukuwa takribani siki tano hadi 10 inategemea na mzunguruko wa mwanamke. Huu ni kuda mzuri wa kushiriki tendo kwa wale ambao hawahitaji kulea ujauzito.

 

2.Zitakapoanza kuingia siku hatari mwanamke ataanza kuhisi uwepo wa uteute kwenye uke wake anapotia kidole kwa ndani. Siku hizi pia zinatofautiana kulingana na idadi ya mzunguruko. Ila zinaweza kuazia siku ya 11 hadi 14 inaweza pia kuwa chini ya papo lwa baadhi ya wanawake ama juu ya hapo.

 

3.Siku moja kabla ya kukomaa kwa yai na kuwa tayari kwenye mirija ya falopian tayari kutungisha mimba, uteute huu huongezeka zaidi. Sifa za uteute huu ni kuwa ni wenye kuteleza sana ila sio mzito na wenye kunatanata ama kuvutikana. Kwa wanaotumia njia za uzazi wa mpango hasa zile za homoni uteute wao upo muda wowote kwa hiyo ni ngumu sana kwao kuiona hali hii.

 

4.Siku ya hatario zaidi mwanamke atapata mabadiliko ya hamu ya kutaka kushiriki tendo la ndoa. Yaani hamu itaongezeka zaidi siku hii kuliko siku iliyotangulia. Hapa kwa wale ambao hawataki ujauzito sio siku salama kwao kushiriki tendo landoa.

 

5.Uteute huu katika siku hizi kuandaliwa kwa ajili ya kusaidia mbegu za kiume ziweze kusafiri vyema, kuogelea vyema na kulifikia yai. Pia kuhakikisha kuwa mbegu za kiume haziathiriwi na asidi ya tumboni kwa mama kwa kiasi kikubwa. Hivyo uteute huu katika kipindi hiki ni muhimu sana.

 

6.Kali hii inaweza kudumu kwa masiku kadhaa toka 14 hadi 17 kwa makadirio inaweza kupungua ama kuongezeka kulingana na mzunguruko wa mwanamke. Baada ya hapo kama mwanamke alibeba ujauzito majimaji haya yanaongezeka uzito saa na kuwa yenye kunata na kufanana na utelezi wa yai pindi unapolibanja. Baada ya mimba majimaji haya yataendelea kutoka na kuongezeka na kuwa mazito zaidi hadi atakapojifungua.

 

Katika ujauzito majimaji haya yanakazi ya kulinda njia ya kuingilia kwenye mji wa mimba dhidi ya mashambulizi na aambukizi ya bakteria. Yaani kuhakikisha kuwa hakuba bakteria ama fangasi atakayeweza kuingia na kumzuru mtoto tumboni.

 

7.Kama hakuna ujauzito uliobebwa majimaji yataanza kurudi kutoka hali yake ya kawaida na kuwa safi, yenye harufu kwa mbali ila si harufu ya kukera, pia yanaweza kuwa na rangi ya maziwa hivi.

 

Majimaji haya pia nayaweza kuashiria shida kwenye afya endapo yatakuwa na sifa hizi:-A.Yana rangi ya njao, kijani ama buluuB.Yana harufu kali mbayaC.Yanakusababishia muwasho kwenye uke na mashavu ya ukeD.Yanakusababishia kuvimba kwa uke na mashavu ya uke

 

8.Ama kuhusu kutokwa na damu, ikiwa chache ni kawaida. Ikiwa unaambatana na maumivu makali ya tumbo, ama maumivi makali ya kichwa na homa, basi vyema kumuona daktari kwa ushauri zaidi. Kama nilivtotangulia kusema kuna wanawake wanapata hedhi wakiwa wajawazito. Wenyewe wanaita kupunguzia, kwa ufupi hii si hedhi na pia haiashirii kama kuna tatizo. Ila kama inatoka nyingi na kuambatana na maumivu yasiyo ya kawaida ni vyema kumuona daktari





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2362


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Dalili za PID
Posti hii inahusu zaidi dalili za PID maana yake ni maambukizi kwenye pelvic kwa kitaalamu huitwa pelvic infection disease, ni ugonjwa unaoshambulia sana wanawake na wasichana Soma Zaidi...

Sababu za Kukoma hedhi (perimenopause)
Kukoma hedhi hufafanuliwa kuwa hutokea miezi 12 baada ya kipindi chako cha mwisho cha hedhi na huashiria mwisho wa mizunguko ya hedhi. Kukoma hedhi kunaweza kutokea katika miaka ya 40 au 50. Kukoma hedhi ni mchakato wa asili wa kibaolojia. Ingawa pia in Soma Zaidi...

SABABU ZA KUKOSA NGUVU ZA KIUME AMA KUWA NA UWEZO MDOGO WA KUHIMILI TENDO LA NDOA
Hii ni hali inayowapata wanaume kushindwa kuhimili tendo la ndoa. Soma Zaidi...

Chanzo cha tezidume, dalili zake na tiba zake.
Post hii inakwenda kukufunza mambo mengi kuhusu tezi dume kama chanzo, dalili, matibabu, njia za kujikinga na mambo hatari yanayoweza kukusababishia kupata tezi dume. Soma Zaidi...

Dalili za kupasuka kwa mfuko wa uzazi.
Posti hii inahusu zaidi dalili za kupasuka kwa mfuko wa uzazi,ni Dalili ambazo ujitokeza kwa Mama ambaye anakuwa amepasuka mfuko wa kizazi. Soma Zaidi...

Mambo muhimu kuhusu mbegu za kiume
Post hii inahusu zaidi mambo muhimu ambayo tunapaswa kujua au kufahamu kuhusu mbegu za kiume, kwa kuwa mbegu za kiume usaidia katika utungaji wa mimba kwa hiyo ni vizuri kabisa kuzitunza Ili kuweza kuepuka matatizo mbalimbali ambayo yanaweza kutokea kwa s Soma Zaidi...

Habari nilitaka kujua kuhusu ugonjwa wa fungusi kwenye uume
Je na wewe unasumbuliwa na fangasi wenye uume. Post hii ni kwa ajili yako. Soma Zaidi...

Dawa ya chango na dawa maumivu ya tumbo la hedhi
Nitakujiza dawa ya chango na maumivu ya tumbo lahedhi, dalili zake na njia za kukabiliana na maumivu ya tumbo la chango. Soma Zaidi...

Namna ya kumpima mtoto uzito
Posti hii inahusu namna ya kumpima mtoto uzito, ni njia ambayo utumika kujua uzito wake na maendeleo ya mtoto. Soma Zaidi...

Maumivu ya uume baada ya tendo la ndoa
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maumivu ya uume baada ya tendo la ndoa Soma Zaidi...

Namna ya kumtunza mtoto aliyezaliwa
Post hii inahusu zaidi namna ya kumtunza mtoto mchanga aliyezaliwa, ni njia zitoleeazo na wakunga Ili kumtunza mtoto mchanga aliyezaliwa. Soma Zaidi...

Hatua za ukuwaji was mimba na dalili zake
Somo hili linakwenda kukuletea hatua za ukuaji mimba na dalili zake Soma Zaidi...