Namna ya kumuosha maiti hatua kwa hatua, nguzo na sunnah za josho la maiti

1.

Namna ya kumuosha maiti hatua kwa hatua, nguzo na sunnah za josho la maiti

Namna ya kumuosha maiti hatua kwa hatua

1.Kuoshwa (Kukoshwa).
Mazingatio kabla ya kuosha maiti.
(a)Maiti ya kiume ioshwe na wanaume na maiti ya kike ioshwe na wanawake pia.
- Maiti ya mtoto yaweza kuoshwa na yeyote.
- Ni Sunnah mke kumuosha mumewe na mume kumuosha mkewe pia



(b)Ni mtu mmoja tu ndiye anayeosha na mwingine ni kwa ajili ya kumpa msaada inapobidi.


(c)Ni muhimu muoshaji afahamu masharti ya kuosha maiti muislamu kama vile;
1. Muoshaji awe muislamu.
2. Mahali pakuoshea pawe faragha (pamesitirika).
3. Maiti aoshwe huku amefunikwa gubi-gubi na nguo nyepesi inayoruhusu maji kupenya kwa urahisi.
4. Ni vyema muoshaji asiishike maiti bali aoshe akiwa amevaa 'gloves'.
5. Kuzingatia masharti ya mwenye kuoga josho la wajibu; kama vile kuwa na maji mengi na safi, pasiwe na kizuizi cha maji kupenya, n.k.



(d)Ni muhimu muoshaji afahamu nguzo na sunnah za kuosha maiti kama ifuatavyo;
- Nguzo za kuosha maiti ni mbili:
1. Nia
2. Kueneza maji mwili mzima wa maiti.
- Ni Sunnah kumuosha maiti mara tatu au zaidi kwa idadi ya witiri.


Namna ya Kuosha Maiti hatua kwa hatua.
i.Maiti awekwe juu ya kitanda chenye tobo katikati ili kupitisha uchafu unaotoka tumboni.
ii.Pawepo na shimo (ufuo) usawa wa tobo la kitanda, kama hakuna uwekano chombo kiwepo cha kukingia uchafu unaotoka kwa maiti.
- Pia maiti inaweza kuoshewa bafuni au kwenye karo liliotengenezwa
kwa kazi hiyo.



iii.Maiti afunikwe na nguo moja kubwa yenye kupenyeza maji wakati wa kuosha.



iv.Maiti akalishwe juu ya kitanda usawa wa tobo na shimo (ufuo) na ainamishwe nyuma kidogo, kama ni mzito ni vizuri msaidizi wa muoshaji amuegemeze kwenye magoti yake.



v.Muoshaji apitishe mkono wa kushoto kwenye tumbo la maiti na kuliminyaminya taratibu ili kutoa uchafu ndani.



vi.Amlaze chali na kuminyaminya tumbo lake kama ilivyo mara ya kwanza.



vii.Aikalishe tena na apitishe mkono wa kushoto chini akiwa amevaa kitambaa au gloves na kusafisha tupu mbili kwa maji safi.
- Kama hapaja takata, basi na avae gloves safi na ile chafu aitupe kwenye
ufuo na asafishe tena kama mara ya kwanza mpaka patakate.



viii.Baada ya hapo, muoshaji afunge kitambaa safi kwenye kidole chake shahada na akichovye kwenye maji na kumswakisha maiti meno yote na kisha akitupe ufuoni.



ix.Muoshaji azungushe kitambaa kingine safi kidole chake kidogo mkono wa kushoto na kumsafisha nacho maiti tundu za pua kisha akitupe ufuoni.



x.Asafishe kucha za maiti kwa kijiti safi na laini iwapo ni ndefu na chafu.



xi.Kisha amkalishe maiti na amtawadhishe kwa kufuata taratibu za kawaida za kutia udhu (kutawadha).



xii.Maiti akiwa amekalishwa, ataanza kumuoshwa kichwa akiwa ameinamishwa mbele kidogo.
- Kama nywele au ndevu ni nyingi zichanwe na kuoshwa kwa sabuni na
maji mpaka zitakate.
- Mwanamke mwenye nywele nyingi zisukwe mikia, na zilizong'oka
ziambatanishwe na sanda.



xiii.Baada ya kuoshwa kichwa, maiti italazwa kwa ubavu wa kushoto na kuanza kuoshwa ubavu wa kulia, mbele na nyuma kwa pamoja kwa sabuni na maji safi mpaka itakate.



xiv.Kisha itaoshwa ubavu wa kushoto kama ilivyooshwa wa kulia.



xv.Baada ya makosho (maosho) haya mawili, la maji na sabuni na la kuondoa sabuni, kosho la tatu la maji liwekewe karafuu na marashi ili kulegeza viungo (maungo) vya maiti.



xvi.Baada ya makosho matatu haya, muoshaji anyooshe viungo vya maiti na kumlaza kama alikuwa mara tu baada ya kufa.



xvii.Kisha achukue nguo kavu na kumfuta maiti, na baada ya hapo maiti awekwe juu ya mkeka mkavu na kufunikwa kwa nguo kavu tayari kuvalishwa sanda (kukafiniwa).



                   



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 702


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Nini maana ya Kibri, madhara yake na kujiepusha na kibri
17. Soma Zaidi...

Kuamini Qadar ya Allah (s.w)
Soma Zaidi...

Vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya kif cha khalifa Uthman
Soma Zaidi...

Aina ya talaka zisizo rejewa
2. Soma Zaidi...

Vipengele vya Mikataba ya 'Aqabah na faida zake katika kuimarisha uislamu Maka na Madina
Katika Hija iliyofuatia katika mwaka wa 621 A. Soma Zaidi...

Msimamo wa Nabii Hud(a.s) Dhidi ya Makafiri wa Kaumu Yake
Pamoja na kwamba alipingwa na nguvu za Dola ya makafiri wa kaumu yake, Mtume Hud(a. Soma Zaidi...

Kujiepusha na Ria na Kujiona
Ria ni kinyume cha Ikhlas. Soma Zaidi...

Haikufundisha Mtume Muhammad quran kwa lengo la kurekebisha tabia za waarabu
Soma Zaidi...

Ndoto ya Nabii Yusufu(a.s) Yatimia
Yusufu(a. Soma Zaidi...

Darsa za sira (maisha ya mtume jaribio la 01
Soma Zaidi...

Darsa za Sira historia ya Mtume (s.a.w) Jaribio la 05
Soma Zaidi...

Kujiepusha na kukaribia zinaa
Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa. Soma Zaidi...