Utaratibu wa kuzika, hatua kwa hatua, na namna ya kusindikiza jeneza

4.

Utaratibu wa kuzika, hatua kwa hatua, na namna ya kusindikiza jeneza

Utaratibu wa kuzika, hatua kwa hatua, na namna ya kusindikiza jeneza

4. Kuzika.

Kusindikiza jeneza.
- Waislamu (watu) wataongozana nayo mpaka kaburini kimya kimya.
- Jeneza lisitanguliwe na watu (msafara).
- Haitakiwi watu kukaa kabla ya jeneza kukalishwa chini.



Kaburi.
- Kaburi liwe pana na kina cha kutosha, mtu kuweza kusimama na kunyoosha mkono kama kuna uwezekano.
- Kisha lichimbwe shimo dogo (mwana ndani) upande wa Qibla ndani ya kaburi.
- Urefu na ukubwa wa kaburi unategemea na ukubwa wa maiti.



Namna ya Kuzika hatua kwa hatua.
a)Waingie watu kaburini kwa idadi ya witiri; 3, 5, 7, n.k.
b)Jeneza liwekwe upande wa kaburi itakapokuwa miguu ya maiti.
c)Maiti itolewe na kutanguliza kichwa kuelekea kaburini.


d)Wapokeaji kaburini watamuweka magotini mwao ili kufungua kamba kichwani, tumboni na miguuni. Pia watafunua shavu la kulia ili liguse ardhini (mchanga) atakapolazwa ndani ya mwana-ndani.

e)Maiti italazwa katika mwana-ndani kwa ubavu wa kulia na kuelekezwa Qibla. Wakati wa kuilaza ni sunnah kusema,
Kama ilivyosimuliwa na Ibn Umar (r.a) kuwa, Mtume (s.a.w) alipokuwa akizika alikuwa akisema:
'Bismillaah wabilahi wa'alaa millati Rasuulullaahi'
Tafsiri:
'Kwa jina la Allah na kwa uwezo wa Allah na kwa mujibu wa mwenendo wa Mtume wa Allah.' (Ahmad, Tirmidh, Ibn Majah).



f)Maiti ipindishwe miguuni na kichwani ili uso na miguu iweze kugusa kuta za mwana-ndani. Kifua, tumbo na sehemu za katikati zibinuliwe nyuma kidogo.

g)Maiti iwekewe mawe au udongo nyuma ya kichwa na miguu isibinuke. Pia ni sunnah kusoma aya za Qur'an (2:1-5) au (2:285-286).

h)Baada ya maiti kulazwa na kusomewa aya hizi, ifunikwe kwa ubao na kama kuna matundu ya kupitisha udongo pazibwe kwa majani.

i)Kabla kaburi halijafunikwa, vitupiwe viganja vitatu vya udongo, na kila tupo unasoma aya ya Qur'an (20:55).
1. Tupo la 1: 'Min-haa khalaq-naakum' ' Kutokana na hii (ardhi) tumekuumbeni.
2. Tupo la 2: 'Wa fiyhaa nughiydukum' ' Na humo (katika ardhi) tutakurudisheni.
3. Tupo la 3: 'Wa min-haa nukhrjukum taaratan-ukhraa' ' Na humo
(katika ardhi) tutakutoweni mara nyingine.



j)Kaburi lijazwe udongo mpaka lijae na kuinuliwa kiasi cha shiburi moja na kuwekewa alama miguuni na kichwani au kupanda miti mibichi.
- Ni vizuri kumiminia maji juu yake ili kuepusha vumbi kupeperushwa na upepo.
- Ni haramu kujengea kaburi kwa namna yeyote ile, kukaa juu yake, kuwasha taa
juu yake na kuielekea wakati wa kuswali.
'Jabir (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amekataza kuyajengea makaburi au kuyajengea nyumba juu yake au kukaa juu yake'. (Muslim)



Abu Marsad Al-ghafariyyi ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema:
'Msikae juu ya makaburi na wala msiswali kwa kuyaelekea.'
(Muslim)



- Baada ya kuzika Mtume (s.a.w) alikuwa akisimama na kusema:
'Muombeeni msamaha ndugu yenu na muombeeni awe
na kauli thabiti kwani sasa anaulizwa'



- Ni sunnah baada ya mazishi kuwapa mikono wafiwa na kuwausia subira
Rejea Qur'an (2:155-156).
- Pia haifai kusema (kusengenya) mabaya ya marehemu.



                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 196

Post zifazofanana:-

HISTORIA NA MAISHA YA NABII ISMAIL(A.S)
Ismail(a. Soma Zaidi...

Taasisi za Kifedha Katika Mfumo wa Uchumi wa Kiislamu
- Ni taasisi za kifedha zinazohusika na kuhifadhi akiba na mali za watu zenye thamani kubwa kama dhahabu, n. Soma Zaidi...

UANDISHI WA HADITHI WAKATI WA TABI'INA
Wakati wa Wafuasi wa masahaba (Tabi'ina)101-200 A. Soma Zaidi...

quran na sayansi
YALIYOMONENO LA AWALI1. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII YUSUFU
Soma Zaidi...

H-D HASSANI SUKARI YA MASHAIRI: (ndege, sababu ya neno lako, penzi penzini, wa ndotoni)
Soma Zaidi...

Hii ndio namna ya kuswali kama alivyoswali Mtume s.a.w
Mtume (s. Soma Zaidi...

darasa la lishe
Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe Soma Zaidi...

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA KITABU CHA PILI
Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 16
9. Soma Zaidi...

NDANI YA JUMBA LA ALADINI
Soma Zaidi...

AFYA NA MAGONJWA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...