4.
4.1 Shahada.
Tafsiri na Maana ya Shahada.
- Shahada ya kwanza.
“Nashuhudia kuwa hapana Mola ila Allah”
Sifa (tabia) za mtu aliyetoa Shahada ya Kwanza Kiutendaji:
-Hatamtii yeyote katika maisha yake ya kila siku ila Allah peke yake.
-Hatamuogopa, hatamtegemea na hatamuomba yeyote ila Allah.
-Hatafuata mwongozo wowote ila ule wa Allah pekee.
-Hatamshirikisha Allah (s.w) kwa chochote kile.
-Atajipamba na sifa na tabia njema zilizoainishwa katika Qur’an na Sunnah.
- Shahada ya Pili.
“Nashuhudia kuwa Muhammad ni Mjumbe wa Allah”
Sifa (tabia) za mtu aliyetoa shahada ya Pili Kiutendaji:
- Kumtii Mtume (s.a.w) kwa kufuata aliyoagiza na kuacha aliyokataza.
- Kumuiga Mtume (s.a.w) katika mwenendo na tabia yake.
- Kumfanya Mtume (s.a.w) kuwa hakimu wa mambo yetu yote.
- Kuliendea lengo la kuletwa kwake la kuusimamisha Uislamu katika
jamii.
Umeionaje Makala hii.. ?
Nazingatio muhimu katika uchumi unaofuata sheria za kiislamu.
Soma Zaidi...Je unaijuwa mipaka yako katika kumiliki mali. Ama unajuwa haki zako katika mali inayomiliki. Endelea na somo
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha aina za najis. Pia utajifunza aina za twahara katika uislamu
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kujitwaharisha kutokana na najisi.
Soma Zaidi...Kwa nini ni muhimu kuswali? Post hii itakwenda kukufundisha kuhusu umuhimu wa kusimamisha swala.
Soma Zaidi...Kila najisi ina namna yake ya kutwaharisha, hata hivyo namna hizo hufanana. Katika post hii utakwenda kujifunza jinsi ya kutwaharisha najisi mbalimbali.
Soma Zaidi...