4.
4.3 Kutoa Zakat na Sadaqat.
Kilugha: Maana yake ni utakaso (purification).
Rejea Qur’an (91:9), (9:103) na (87:14).
Kisheria: Maana yake ni sehemu ya mali (2.5% au 1/40) ya tajiri anayotakiwa kutoa
kuwapa wanaostahiki baada ya kufikia kiwango cha Nisaab.
Nisaab: Ni kiwango (kima) akifikia au kuzaidi muislamu, analazimika kutoa zakat.
Kilugha: Neno ‘sadaqat’ linatokana na neno “sidiq” lenye maana ya ukweli.
Kisheria: Sadaqat maana yake ni mali au huduma inayotolewa kwa mtu yeyote
anayohitajia.
| Na. | Zakat | Sadaqat | 
| 1. | Inahusiana na utoaji wa mali tu. | Inahusiana na utoaji wa mali na huduma. | 
| 2. | Ni faradhi (amri) tu kwa tajiri muislamu aliyefikia kiwango cha Nisaab. | Ni wajibu kwa kila mtu kadri ya uwezo wake pindi inapohitajika. | 
| 3. | Zakat hutolewa kwa kiwango maalumu (2.5% au 1/40) cha mali inayojuzu kutolewa zaka. | Sadaqat haina kiwango maalumu. Kila muislamu atatoa kulingana na uwezo wake. | 
| 4. | Zakat hutolewa baada ya mwaka au mavuno. | Sadaqat haina muda maalumu wa kutoa. | 
| 5. | Zakat hustahiki kupewa Waislamu tu. | Hupewa mtu yeyote bila kujali dini au uwezo wake, bali kila anayehitajia. | 
Rejea Qur’an (14:31) na (2:254).
Rejea Qur’an (9:11) na (2:2-3).
Rejea Qur’an (2:2-3), (23:1-4), (22:34-45) na (2:262,274).
Rejea Qur’an (9:34-35), (92:8-10) na (3:180).
- Mali ya halali na iliyochumwa kwa njia ya halali ndio inayofaa kutolewa Zakat ua Sadaqat. Mali ya haramu au iliyochumwa kwa njia ya haramu haikubaliki.
Rejea Qur’an (4:10), (23:51) na (2:172).
- Ni kutoa kile ukipendacho kwa dhati na ndio zina malipo makubwa kwa Allah.
Rejea Qur’an (2:267) na (3:92).
- Ni kutoa kwa kuzingatia kipimo (kiasi) ambacho hakiwezi kukuathiri katika matumizi ya maisha yako na familia pia.
Rejea Qur’an (2:219) na (17:29).
- Ni kutoa mali au huduma kwa ajili ya Allah pasina kujionyesha na kufuatilia kwa masimbulizi.
Rejea Qur’an (2:264), (2:271) na (2:274).
- Zakat au Sadaqat hutolewa kupewa watu maalumu wanaohitajia, wenye matatizo na zikitolewa kwa asiyestahiki, huwa ni dhuluma.
Rejea Qur’an (9:60).
Kwa mujibu wa Qur’an (9:60) na (2:273), wanaostahiki kupewa Zakat ni waislamu tu katika makundi yafuatayo;
- Ni kundi la wale wasiojiweza kwa chochote cha kumudu maisha yao kabisa ya kila siku bila kusaidiwa.
- Ni wale wasio na uwezo wa kupata mahitaji yao ya msingi ya kimaisha ila wana uwezo wa kujikimu kwa kiasi fulani tu.
- Ni wale wote wanaozikusanya na kuzigawanya kwa wanaohusika bila kujali uwezo wao.
- Ni wale walioingia katika Uislamu karibuni na wanahitajika kuimarishwa imani zao juu ya Uislamu.
- Ni kuwakomboa au kuwanunua watumwa au watu wote wanaoishi chini ya miliki ya watu (mabwana) na kuwaachia huru.
- Ni kuwalipia waislamu madeni yao waliokopa ili kujikimu kimaisha lakini bila kukusudia wameshindwa kulipa deni zao.
- Ni kutumika katika shughuli zote zinazopelekea kuhuisha na kusimamisha Uislamu katika jamii.
- Msafiri yeyote muislamu aliyeharibikiwa kwa kupoteza, kuibiwa au kuishiwa mali yake hata kama ni tajiri, ni wajibu kupewa zakat.
Kwa mujibu wa Qur’an (4:36) na (51:9);
- Sadaqat hupewa wale wale wanaopewa Zakat lakini bila kiwango au muda
maalumu au kufikia nisaab.
- Sadaqat hupewa mwanaadamu yeyote hata wasiokuwa Waislamu ikiwa tu ni
mwenye kuhitajia.
- Kila muislamu anao uwezo wa kutoa sadaqat, kwani inahusika na kutoa mali,
huduma, tabia nzuri, n.k.
Rejea Qur’an (2:263).
- Pia haifai kurejesha sadaqat baada ya kuitoa.
Rejea Hadith ya Umar (r.a); Kitabu cha 2; EDK. Uk. 80.
Rejea Jedwali lifuatalo na pia katika Kitabu cha 2; EDK, uk. 80-87.
| Na. | Mali zinazojuzu kutolewa Zakat | Nisaab (Kiwango) | Kiasi (%) | Muda wa Kutoa | 
| 1. | Mazao yote ya shambani. | Wasaq 5 au kg 666 (Wasaq 1 = 133.5kg) | (a) Kg 66.6 au ½ wasaq kwa mazao ya maji ya mvua. (b) Kg 33.3 au ¼ wasaq kwa mazao yaliyomwagiliwa. | Baada ya mavuno | 
| 2. | Wanyama wafugwao kwa ajili ya chakula: (a) Ngamia (b) Ng’ombe (c) Mbuzi (d) Kondoo (e) Kondoo au Mbuzi | Ngamia 5 Ng’ombe 30 Mbuzi 40 Kondoo 40 Kondoo au Mbuzi 40 | Mbuzi 1 wa mwaka 1 Ndama 1 wa mwaka 1 Mbuzi 1 wa mwaka 1 Kondoo 1 wa mwaka 1 Kondoo au mbuzi 1 wa mwaka 1 | Baada ya mwaka | 
| 3. | Dhahabu na Vito | Gram 82.5 au tola 7.5 | 2.5 % au 1/40 ya thamani ya mali | Baada ya mwaka | 
| 4. | Fedha na Vito | Gram 577.5 au tola 52 | 2.5 % au 1/40 ya thamani ya mali | Baada ya mwaka | 
| 5. | Mali ya Biashara | Sawa na thamani ya Nisaab ya Dhahabu au Fedha. | 2.5 % au 1/40 ya mali | Baada ya mwaka | 
| 6. | Fedha taslimu | Sawa na mali ya Biashara | 2.5 % au 1/40 ya fedha | Baada ya mwaka | 
| 7. | Mali ya kuokota au kuchimbuliwa ardhini | Haina | 20 % au 1/5 ya mali | Baada ya kuokotwa na kukosa mwenyewe au baada ya kuchimbuliwa. | 
Umeionaje Makala hii.. ?