NGUZO ZA UISLAMU: SWALA NA SHAHADA NA FAIDA ZAKE

NGUZO ZA UISLAMU.

NGUZO ZA UISLAMU: SWALA NA SHAHADA NA FAIDA ZAKE

NGUZO ZA UISLAMU: SWALA NA SHAHADA NA FAIDA ZAKE

NGUZO ZA UISLAMU.
1. Maana ya Shahada.
Shahada mbili ndio nguzo ya kwanza ya Uislamu na ndio kiingilio cha mtu katika Uislamu kwa kuyakinishwa moyoni, kutamkwa kinywani na kuthibitishwa kwa vitendo.
Rejea Qurโ€™an (41:30-31), (2:8) na (33:40).

2. Maana ya Kusimamisha Swala.
Ni kuswali kwa kutekeleza kikamilifu nguzo, sharti zote za swala na kuwa na unyenyekevu (khushui) ndani ya swala.

Nafasi na Umuhimu wa Kusimamisha Swala katika Uislamu.
Swala imesisitizwa na ina umuhimu katika Uislamu kwa sababu zifuatazo;

i.Kusimamisha Swala ni Amri ya Mwenyezi Mungu (s.w).
Mwenyezi Mungu (s.w) ameamrisha waumini (waislamu) wote wasimamishe swala zote za faradh na sunnah ipasavyo.
Rejea Qurโ€™an (29:45), (4:103) na (14:31).

ii.Kusimamisha swala ni nguzo ya Pili ya Uislamu.
Baada ya shahada mbili, nguzo ya pili na ya msingi mno katika Uislamu ni kusimamisha swala.

iii.Swala humtakasa muislamu na mambo machafu na maovu.
Bila shaka swala ikiswaliwa vilivyo humuepusha mja na mambo machafu na maovu.
Rejea Qurโ€™an (29:45).

iv.Swala ni amali ya mwanzo kabisa kuhesabiwa siku ya Qiyama.
Swala ya muumini ikitengemaa vizuri ndio sababu ya kufaulu kwake Duniani na Akhera pia.
Rejea Qurโ€™an (23:1-2,9), (87:14-15) na (22:34-35).

v.Kutosimamisha swala ni sababu ya mtu kuingizwa motoni.
Hii ni baada ya muislamu Kupuuza swala kwa kutozingatia sharti na nguzo zake kikamilifu na kukosa unyenyekevu (khushui) ndani ya swala.
Rejea Qurโ€™an (74:42-47), (68:42-43) na (107:4-5).

Lengo la Kusimamisha Swala.
Lengo kuu la kusimamisha swala ni kumkinga mja na mambo machafu na maovu kwa kutekeleza kikamilifu sharti, nguzo na sunnah za swala pamoja na kuwa na khushui ndani ya swala kama ifuatavyo;
i.Swala inamtakasa mja kwa kuzingatia na kutekeleza sharti zake zote kikamilifu ambazo ni kuwa twahara, sitara (kujisitiri), kuchunga wakati wa swala na kuelekea Qibla.
ii. Swala inamtakasa mja kwa kutekeleza kikamilifu nguzo na sunnah za swala kama kumsifu na kumtukuza Mwenyezi Mungu (s.w), kusoma Qurโ€™an, kutoa ahadi ya kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu (s.w), kuomba dua na kutekeleza vitendo vyote vya swala.

Faida (matunda) ya kusimamisha swala katika jamii.
Swala za faradhi zikisimamishwa vilivyo faida zifuatazo hupatikana katika jamii;

i.Usafi na unadhifu wa mwili.
Kwani muislamu hawezi kuswali mpaka ahakikishe kuwa msafi (twahara) kikamilifu katika nguo na mwili pia na sehemu ya kuswalia.
Rejea Qurโ€™an (7:31).

ii.Utakaso wa Nafsi.
Kwa kutekeleza sharti na nguzo za swala pamoja na mnyenyekevu katika swala, hupelekea mja kuwa mtiifu ipasavyo kwa Mola wake muda wote.

iii.Swala za jamaa huimarisha udugu, umoja na usawa.
Kuswali katika jamaa huleta udugu, umoja na usawa wa kweli na kuepusha mfarakano, chuki na ubaguzi miongoni mwa waislamu.
Rejea Qurโ€™an (49:10,13).

iv.Swala za jamaa huwafunza waislamu uongozi bora.
Swala huongozwa na imamu (kiongozi) wa waumini husika anayetokana na wao kutokana na sifa maalumu za kuwa kiongozi.



Kwa nini Wengi wanaoswali hawafikii Lengo la Swala zao?
Miongoni mwa sababu ya wengi kutofikia malengo ya swala zao ingawa wanaziswali misikitini tena kwa jamaa ni;

1.Hawajui lengo halisi la swala.
Waislamu wengi huswali kwa lengo la kufutiwa madhambi na kupata thawabu na sio kuepukana na machafu na maovu, ambalo ndio lengo kuu la swala. Kupata thawabu na kufutiwa madhambi ni matunda ya swala.
Rejea Qurโ€™an (29:45) na (72:23).

2.Waislamu wengi hawana ujuzi sahihi juu ya swala.
Pamoja na waislamu wengi kutekeleza swala zao kwa jamaa lakini wengi wao hawajui kabisa miiko, sharti na nguzo za swala ila wanafuata mkumbo tu.
Rejea Qurโ€™an (7:205), (7:55) na (4:142).

3.Waislamu wengi hawahifadhi swala zao.
Pamoja na kuswali kwao bado wengi hawazingatii na kutekeleza kikamilifu sharti na nguzo za swala zao inavyotakiwa.
Rejea Qurโ€™an (107:4-5) na (23:1,8).

4.Wengi hawaswali kwa Unyenyekevu swala zao.
Kukosa unyenyekevu (utulivu wa mwili, fikra na uzingativu) hupelekea mwenye kuswali kutofikia lengo na matunda ya swala.
Rejea Qurโ€™an (29:45), (23:1-2) na (23:10-11).

5.Kutosimamisha Swala za jamaa ipasavyo.
Waislamu wengi hawaswali jamaa misikitini au hawazingatia sharti za swala ya jamaa kama kunyoosha safu ipasavyo, kugusanisha mabega, vidole, n.k.
Rejea Qurโ€™an (23:1-2).





                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 2126

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 kitabu cha Simulizi    ๐Ÿ‘‰2 Kitau cha Fiqh    ๐Ÿ‘‰3 Dua za Mitume na Manabii    ๐Ÿ‘‰4 Simulizi za Hadithi Audio    ๐Ÿ‘‰5 Bongolite - Game zone - Play free game    ๐Ÿ‘‰6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

Kiasi cha mahari kilicho bora kinachofaaa katika uislamu

Uislamu haukuwekabkiwango maalumu cha mahari. Mwanamke anaweza tajabkiasi atakacho. Ila vyema kuzingatia haya wakayi wa kutamka mahari yako.

Soma Zaidi...
hukumu ya ombaomba katika uchumi wa kiislamu

Suala la omba-ombaTukiliangalia suala la omba-omba kwa upana kidogo, ambalo hivi sasa linaongelewa katika vikao mbalimbali vya kitaifa na kimataifa, tutaona kuwa ni Uislamu pekee unaotoa namna bora ya kulishughulikia suala hili.

Soma Zaidi...
TOFAUTI KATI YA MAKATOZO NA MAAMRISHO KATIKA SUNNAH

ุนูŽู†ู’ ุฃูŽุจููŠ ู‡ูุฑูŽูŠู’ุฑูŽุฉูŽ ุนูŽุจู’ุฏู ุงู„ุฑูŽู‘ุญู’ู…ูŽู†ู ุจู’ู†ู ุตูŽุฎู’ุฑู ุฑูŽุถููŠูŽ ุงู„ู„ู‡ู ุนูŽู†ู’ู‡ู ู‚ูŽุงู„ูŽ: ุณูŽู…ูุนู’ุช ุฑูŽุณููˆู„ูŽ ุงู„ู„ูŽู‘ู‡ู ุตู„ู‰ ุงู„ู„ู‡ ุนู„ูŠู‡ ูˆ ุณู„ู… ูŠูŽู‚ููˆู„ู: "ู…...

Soma Zaidi...
mambo yanayofungua swaumu

post hii ijakwenda kukufundisha mambo yanayoharibu funga

Soma Zaidi...
Riba na Madhara Yake Katika Jamii

- Riba ni kipato chochote kile cha ziada kutokana na mkopo au mtaji bila kushiriki katika faida au hasara.

Soma Zaidi...
Masharti ya swala

Sharti za SwalaSharti za Swala Sharti za swala ni yale mambo ya lazima anayotakiwa Muislamu ayachunge na kuyatekeleza kabla hajaanza kuswali.

Soma Zaidi...
JIFUNZE FIQH

Fahamu darsa mbalimbali za fiqh kama swala, twahara, zaka pamoja na funga. Zijuwe sharti za swala, funga na zaka.

Soma Zaidi...
Namna ya kuswali hatuwa kwa hatuwq

Post hii itakufundisha jinsi ya kuswali hatuwa kwa hatuwa.

Soma Zaidi...