Posti hii inahusu zaidi dawa ya ALU kama Dawa inayotibu Ugonjwa wa Malaria ,ni dawa ambayo utumiwa na watu wengi kwa matibabu ya ugonjwa wa Malaria.
Kazi za ALU katika kutibu ugonjwa wa Malaria.
1. ALU ni dawa inayotumiwa kutibu ugonjwa wa Malaria kwa Lugha nyingine huitwa mseto, ALU kwa kirefu chake ni Artemether Lumefantrine, hili ni Jina la kitaalamu ambalo Lina dawa mbili ya kwanza ni Artemether yenye gram ya 20 mg na nyingine ni Lumefantrine yenye milligram ya 120 jumla dawa hii ya ALU Ina milligram 140 mg ambazo utumiwa kulingana na utaratibu inayotolewa na wataalamu wa afya kama vile madaktari, wauguzi na waphamasia kulingana na utaratibu unapaswa kutumiwa kwa mgonjwa.
2.Dawa hii ya Mseto utumiwa na wagonjwa ambao Wana malaria ya kawaida hii dawa siyo ya wagonjwa wenye malaria kali, utawafahamuje wagonjwa wenye Malaria ya kawaida kwa kuangalia dalili mbalimbali kama vile Homa kwa mtu wenye malaria, kuuma kwa joint, kutapika kwa Mgonjwa, maumivu ya kichwa kwa mgonjwa, mwili mzima kuishiwa nguvu, kuharisha kwa mgonjwa lakini sio sana kukosa hamu ya kula chakula, hizi dalili zinatokea kwa Mgonjwa na zinakuwa hazina nguvu sana kwa mgonjwa kwa hiyo mgonjwa akipata dalili kama hizi anapaswa kwenda hospitalini kwa ajili ya vipimo na akigundua kuwa ni malaria anaweza kutumia Mseto kwa sababu hizi na dalili za kawaida.
3. Dawa hizi za Mseto pia hazipaswi kutumiwa na wanawake wajawazito kwa sababu zinaweza kuleta madhara makubwa kwa kwa mtoto akiwa tumboni kwa hiyo akina Mama wajawazito wanapaswa kujua hili na walizingatie na kujua kuwa wanapaswa kutumia dawa zao za SP wakiwa wajawazito Ili kuzuia maambukizi ya malaria kwa mtoto, kwa hiyo elimu inabidi kutolewa kwa akina Mama hasa wajawazito Ili kuepuka matatizo yanayoweza kutokea, pia dawa hii hakipaswi kutumiwa na watu wenye Allergy nayo kwa hiyo labda mtu mwingine anaweza kuitumia akawa na vi upele na matokea ambayo yanaweza kujitokeza na kumweka mtu katika hali ya hatari hasitumie.
4. Dawa hii ya Mseto inaweza kuwa na matokea mbalimbali kama vile kichwa kuuma, kizunguzungu,kutapika kuishiwa nguvu, kukosa hamu ya kula mgonjwa hasishangae au kuogopa haya na maudhi madogo madogo madogo yanatokea kwa mgonjwa ni kwa sababu dawa inakuwa inapambana na bakteria Ambao wapo kwenye mwili.
5. Kwa hiyo mgonjwa akitumia dawa hii anapaswa kula na kushiba kunywa maji mengi, kwa kufanya hivyo dawa ufanya kazi vizuri na matokea mengine kama vile kukosa nguvu anaweza hasiyapate na kumeza dawa zake Huku akiendekea na kazi zake za kawaida katika jamii. Kwa hiyo saw hii ya Mseto ikitumiwa vyema mtu anaweza kupona haraka na iwapo atazingatia masharti katika matumizi yake.kwa hiyo Mseto ni dawa nzuri na ya uhakika katika kutibu ugonjwa wa Malaria.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi njia ya kupitisha dawa kwenye mdomo na vipengele vyake, hii njia dawa umengenywa kwenye tumbo na kupitia kwenye utumbo mdogo na baadae kwenye damu,
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya carvedilo katika matibabu ya magonjwa, ni mojawapo ya dawa kwenye kundi la beta blockers na pia uhusika katika matibabu ya magonjwa ya moyo kama nyingine.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi matibabu kwa mgonjwa wa uti wa mgongo, kwa kawaida tunajua kuwa homa hii ya uti wa mgongo usababisha na wadudu mbalimbali kama vile bakteria, virus, fungasi, sumu mbalimbali kama vile madini ya lead na arseni, na vitu kama vile Mag
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya paracetamol katika kutibu maumivu, ni dawa inayosaidia kutibu maumivu ya Kawaida kama vile aspirin.
Soma Zaidi...Post hii Inahusu zaidi dawa za kutibu maambukizi yoyote Yale yanayosababishwa na bakteria dawa hizi kwa kitaamu huiitwa antibiotics Kuna dawa mbalimbali zinazotibu maambukizi ya bakteria leo tutaanza na dawa ambayo inaitwa penicillin.
Soma Zaidi...Post hii inahusu dawa ya kaoline katika kutibu au kuzuia kuharisha ni dawa ambayo imependekezwa kutumiwa hasa kwa wale walioshindwa kutumia dawa ya loperamide.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ambazo zinatumika kwenye matibabu ya kansa, dawa hizi usaidia kuharibu seli ambazo ambazo hazistahili kwa kitaalamu huitwa malignant seli.
Soma Zaidi...hapa utajifunza dalili za fangasi, dawa ya fangasi na aina za fangasi, pia nitakujuza njia za kukabiliana na fangasi
Soma Zaidi...DAWA YA MAPUNYEMatibabu ya mapunye inategemea ni wapi mapunjye yapo.
Soma Zaidi...