DAWA YA RIFAMPICIN NA KAZI ZAKE


image


Posti hii inahusu zaidi Dawa ya Rifampicin na kazi zake, hii ni dawa mojawapo inayotibu kifua kikuu kati ya Dawa zilizoteuliwa kutibu ugonjwa wa kifua kikuu.


Dawa ya Rifampicin na kazi zake.

1.Dawa ya Rifampicin ni dawa ambayo utumika katika kipindi cha kwanza na cha pili katika vipindi vikuu viwili vya matibabu ya kifua kikuu, hii dawa usaidia kuuua bakteria wanaosababisha kifua kikuu na pia kuzuia protein ya bakteria isizalishwe kwa hiyo bakteria hao hawawezi kuishi na kuzaliana kwa sababu ya kuwepo kwa dawa ya Rifampicin.

 

2.Pia hii dawa usaidia kuua bakteria anayeitwa TB bacill  na pia dawa hiii uweza kuua bakteria ambao wameshaene kwenye mwili wa binadamu na pia uua bakteria wale ambao wamekaa mda mrefu kwenye mwili wa binadamu, kwa hiyo tunaona faida kubwa ya dawa hii tunapaswa kuitumia kwa maelekezo ya wataalamu wa afya, pia dawa hii haiwezi kutumika ikiwa yenyewe bali huwa na mchanganyiko wa madawa mengine.

 

3.Dawa hii ya Rifampicin utumiwa na watu wenye kifua kikuu lakini sio wote wenye kifua kikuu wanaweza kutumia kwa sababu mbalimbali kwa mfano wale wanaotumia uzazi wa mpango na wana Ugonjwa wa kifua kikuu wanapaswa kuona madaktari ili waweze kupata njia za uzazi wa mpango hambazo haziingilian na dawa ya Rifampicin kwa sababu kuna njia za uzazi wa mpango ukizitumia pamoja na dawa ya Rifampicin dawa hii uweza kumaliza dawa za njia ya mpango nguvu na mtu akapata mimba.

 

4.Pamoja na kutumia njia hii kuna maudhi mbalimbali ambayo yanaweza kujitokeza katika kutumia dawa hizi ni kama kichefuchefu, kutapika na hata kuharisha kwa wagonjwa wengine, na maumivu ya kichwa yanaweza kutokea pia pamoja na homa, kwa hiyo hizi Dalili zikitokea mgonjwa hasiogope ni kawaida ila kwa wanaoanza maudhi haya yakiendelea wanapaswa kwenda hospitalini ili kuangalia labda kuna tatizo fulani.

 

5.Kwa kubwa ugonjwa huu unatibika tunapaswa kuwapeleka wagonjwa wetu hospitali ikiwa wataonesha Dalili za kifua kikuu ambazo ni pamoja na homa za mara kwa mara, kupungua uzito , kukohoa kwa wiki mbili na kukonda hizi ni baadhi ya Dalili tunapaswa kuwahi mapema kwa sababu Ugonjwa huu usambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kama mgonjwa hajatumia dawa akishatumia dawa kwa wiki mbili hawezi kuambukiza wengine.

 

6.Kwa hiyo elimu inapaswa kutolewa kwa jamii ili kuwaleta wagonjwa wao hospitalini wasiwafiche na kuna imani potovu ambayo utokea kubwa mgonjwa wa kifua kikuu ufuchwa ndani wakidai kuwa ana Maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi kumbe ni kifua kikuu kwa sababu ya kufanana kwa baadhi ya Dalili, kwa hiyo elimu inapaswa kutolewa ili kuweza kutokomeza kabisa janga hili



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    2 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    3 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    4 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    5 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    6 Mafunzo ya php    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Dalili za jeraha la kawaida kwenye ubongo
Posti hii inahusu zaidi dalili la jeraha la kawaida kwenye ubongo, jeraha la kawaida utokea kwa sababu mbalimbali kama vile kupata ajali na kugongwa na kitu chochote kichwani, Soma Zaidi...

image Dalili za tezi dume ambayo hazijashuka (cryptorchidism)
Tezi dume ambayo haijashuka si ya kawaida kwa ujumla, lakini ni ya kawaida kwa wavulana waliozaliwa kabla ya wakati.na muda mwingine zikipanda tumboni huwa hazishuki kabisa kwenye korodani. Soma Zaidi...

image Huduma ya Kwanza kwa aliyeungua
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa aliyeungua Soma Zaidi...

image Dalili za minyoo ya tumbo
Posti hii inaelezea kuhusiana na dalili za minyoo ya tumbo ambapo minyoo hawa husababishwa na mtu kula vyakula vichafu ambavyo havijaiva vizuri au maji machafu pia au bacteria. Soma Zaidi...

image Njia za kuzuia kiungulia
Somo hili linakwenda kukueleza baadhi ya njia za kuzuia kiungulia Soma Zaidi...

image Dawa za kutibu kiungulia
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za kutibu kiungulia Soma Zaidi...

image Njia za kukabiliana na minyoo
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kukabiliana na minyoo Soma Zaidi...

image Faida za kula mayai
Posti hii inahusu zaidi faida anazozipata mtu anayekula mayai hasa wakati wa kifua kinywa, tunajua wazi kuwa mayai yana kiwango kikubwa cha protini pamoja na hayo kuna faida nyingi za kutumia mayai hasa wakati wa asubuhi kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

image Kichwa kinaniuma mbele sielewi nini
Zijuwe sababu za kuumwa nankichwa upande mmoja wa kichwa. Soma Zaidi...

image Huduma kwa mtoto mdogo anayeumwa
Mtoto mdogo ni mtoto chini ya miaka mitano, yaan kuanzia pale anapozaliwa mpaka anapafikisha miaka mitano Soma Zaidi...