Dawa ya UTI

Dawa ya UTI

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa ya UTI

Dawa ya UTI na UTI iliyo suguKama ulishawahi kujiuliza masalikama chanzo cha UTI, sababu zake, njia za kukabiliana na uti vipi uti inaenezwa na ni zipi dawa zake. Makala hii ni kwa ajili yako, nimeiandaa kwa ufupi na kwa ufanisi kiasi cha kuweza kukuridhisha kwa majibu ya maswali yako. Kama utakuwa na mawazo zaidi, tuachie maoni yako hapo chini.

 

Ugonjwa wa UTI ni nini?UTI ni kifupisho cha maneno Urinary Track Infection. Ni maambukishi na mashambulizi ya bakteria aina ya E.coil katika mfumo wa mkojo. Mwanzoni bakteria huingia kwenye kibofu, figo ama sehemu yeyote kwenye mfumo wa mkojo. Kisha bakteria huyu anaanza kushambulia na kuathiri mfumo huu na ndipo dalili za UTI huanza kuonekana kama maumivu wakati wa kukojoa. Dalili za uti huonekana kuanzia siku 3 mpaka 8 toka kuambukizwa.

 

Ni zipi sababu za UTISababu kuu za ugonjwa wa UTI ni bakteria aina ya E.coil. Bakteria huyu huishi kwenye utumbo. Sasa endapoa atapata njia kutoka kwenye utumbo kupitia haja kubwa na akaingi kwenye mfumo wa mkojo hasa hasa kwa wanawake anasababisha UTI. Pia bakteria wanaoishi kwenye uke, mkundu na kuzunguka sehemu za siri wanaweza rahisi kupata njia na kuingia kwenye mfumo wa mkojo na kusababisha uti. Pia UTI inaweza kusababishwa na baadhi ya magonjwa ya ngono kama gonorrhea, chlamydia na mengine.

 

Ugonjwa wa uti unaenezwa vipi?Mtu ataweza kupata UTI kama atafanya chochote ambacho kitaletwa bakteria wanaoishi kwenye utumbo kwenye kwenye nia ya mkojo. Kwa mfano kama wakati wa kuchamba alichamba kwa kuelekea mbele kisha bakteria waliotoka kupitia haja kubwa wakafikia kwenye uume ama uuke, hawa wataingi ndani na kusababisha uti. Si kawaida sana uti kuambukizwa kupitia ngono lakini inaweza kutokea. Na ndio maana inashauriwa ukakojoe baada ya kufanya ngono.

 

Pia maeneo ya chooni mtu anaweza kupata UTI ila pia hii hutokea mara chache sana na ni kwa wanawake ama kwa wale ambao wanajisaidi kwenye vyoo vya kukaa na si kucuchuchumaa ama kusimama hata hivyo si ahisi kwani lamda kama choo ni kichafu ndipo utapata UTI. Hata hivyo watu hawa wapo hatarini zaidi kupata UTI

 

1.Kama ulishawahi kupata UTI2.Kama una kisikari3.Kama una kiriba tumbo4.Kama unatumia baadhi ya njia za kidhibiti uzazi kama spermicides au diaphrahm5.Kama una vijiwe kwenye figo au kibofu na vijiwe hivi vikawa vinazuia mkojo kutoka kwa urahisi.6.Kama ni mjamzito

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Dawa Main: Post File: Download PDF Views: 3419

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Dua za Mitume na Manabii     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zinazofanana:

Kazi za Dawa ya Artesunate katika kutibu Malaria

Posti hii inahusu zaidi kazi za dawa ya Artesunate katika kutibu Malaria kali, ni dawa ambayo inatumika sana kutibu Malaria kali.

Soma Zaidi...
Fahamu dawa za kutuliza kifafa inayoitwa phenobarbital

Post hii inahusu dawa za kutuliza kifafa, zipo dawa mbalimbali za kutuliza kifafa Leo tutaona dawa mojawapo inayoitwa phenobarbital katika kutuliza kifafa.

Soma Zaidi...
Tiba mbadala za vidonda vya tumbo

Somo hili linakwenda kukuletea tiba mbadala za vidonda vya tumbo

Soma Zaidi...
Faida za vidonge vya zamiconal

Posti hii inahusu zaidi faida za vidonge vya zamiconal, ni baadhi ya faida ambazo upatikana kutokana na vidonge vya zamiconal,ni vidonge ambavyo utibu au kusaidia kwenye matatizo ya viungo vya uzazi.

Soma Zaidi...
IJUE DAWA YA AMOXLINE (antibiotic) NA MATUMIZI YAKE

Posti hii inahusu zaidi dawa ya amoxline .jinsi inavyofanya kazi mwilini.pamoja na matumizi yake.

Soma Zaidi...
Mgawanyo wa tiba ya kifua kikuu

Post hii inahusu zaidi mgawanyiko wa tiba ya kifua kikuu, kwa kawaida tiba hii imegawanyika katika sehemu kuu mbili.

Soma Zaidi...