Dawa ya chango na dawa maumivu ya tumbo la hedhi
Nitakujiza dawa ya chango na maumivu ya tumbo lahedhi, dalili zake na njia za kukabiliana na maumivu ya tumbo la chango.
Dawa ya chango na dawa maumivu ya tumbo la hedhi.
Ni hali ya kawaida kwa mwanmke kupatwa na maumivu akikaribia hedhi ama anapokuwa kwenye hedhi. Hali hii haihitaji hata uangalizi wa daktari. Maumivu haya yanaweza kutofautiana kulingana na umri na maumbile. Kwa wanaoanza sasa wanaweza kupatwa na maumivu makali hata kuliko ambao ni wakubwa. Ambao wana matatizo ya homoni mau,ivu yanaweza kuw ani makali pia. Ukali hii ni wenye kuvumilika, lakini inatokea baadhi ya nyakati kwa baadhi ya wanawake maumivu hayawezi kuvumilika ni makali sana, mpaka anapelekwa hospitali.
Basi makala hii ni kwa ajili yako, tutaona sababu za maumivu haya makali yasiyoweza kuvumilika na pia tatuaona dawa za chango na maumivi ya tumbo la hedhi. Usichoke endelea nayo makala hii mpaka mwisho. Ukipenda tuwachie maoni yako hapo chini.
Ni zipio sababu za maumivu makali ya chango na tumbo la hedhi?
1.Kuota kwa vinyama maeneo mengine ndani ya mwili lakini nje ya tumbo la mimba. Hali hii inaweza kuwa na dalili kama kupata hedhi yenye damu nyingi sana na za mabonge, hedhi kuwa zaidi ya siku 7, maumivu makali ya tumb, maumivu makali wajati wa kushiriki tendo la ndoa.
2.Kama mfumo wa homoni haupo sawa yaani hormone imbalance. Tatizo la homoni ni sugu sana kwa wanawake wengi. Inakadiriwa kuwa katika kila wanawake 10 basi mmoja wao atakuwa na tatizo hili. Shida ya homoni inaweza kuwa na dalili kama:- maumivu makali ya chango, kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi, kutokwa na chunusi nyingi usoni, mwanamke kuwa mzito sana, nywele zake zinakuwa dhaifa na kunyonyoka kwa haraka, na ngozi kuwa na madod madoa.
3.Kuwa na uvimbe kwenye mfumo wa uzazi. Mwnamke anaweza kuwa na dalili kama maummivu ya miguu, maumivu ya mgongo kwa chhini, kukosa choo kikubwa, kupata hedhio yenye damu nyingi, maumivu mkakli ya chango, kukojoa mara kwa mara na kushindwa kumaliza mkojo wote anapokojoa.
4.Kuwa na maambukizi au mashambulizi ya bakteria, fangasi na virusi kwenye mfumo wa uzazi. Mwanamke anaweza kupatwa na dalili kama kutokwa na damu kablya ya kuinia hedhi na baada, kutokwa na majimaji yanayotoa harufu ukeni, maumivu makali wakati wa kukojoa, kupata homa.
Sababu nyingine ni:
1.Kukaza kwa tisu za kwenye tumbo la kizazi
2.Matumizi ya baadhi ya njia za uzazi wa mpango
3.Maumbile ya mwanamke.
Dawa ya chango na dawa maumivu ya tumbo la hedhi.
A.Ibuprofen (Advil, Motrin IB)
B.Naproxen sodium (Aleve na Anaprox)
C.Ketoprofen (Actron na Orudis KT)
D.Mefenamic acid
Namna ya kukabiliana na tumbo la chango na maumivu ya tumbo la hedhi
1.Fanya mazoezi ya mrakwa mara
2.Hakikisha huna misongo ya mawazo
3.Punguza kula vyakula vyenye chumvi sana pia punguza kula vitu vya sukari sana
4.Punguza unywaji wa chai ya majani ya chai (caffein)
5.Punguza vyakula vyenye mafuta ya wanyama kwa wingi kama nyama.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitau cha Fiqh 👉2 ai web app 👉3 Dua za Mitume na Manabii 👉4 web hosting 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Yajue mazoezi ya kegel
Posti inahusu zaidi mazoezi ya kegel, ni mazoezi ambayo ufanywa na watu wengi na sehemu yoyote yanaweza kufanywa kama vile chumbani, sebuleni, uwanjani na sehemu yoyote ile na kwa watu tofauti.
Soma Zaidi...anawashwa Sana sehemu ya Siri mpaka anatoka vipele vingi kwenye mapaja korodani zake zimebadilika kuwa nyekundu
Abali mkuu Nina mdogo wangu anawashwa Sana sehemu ya Siri mpaka anatoka vipele vingi kwenye mapaja korodani zake zimebadilika kuwa nyekundu na zenye kutisha uume wake nao umekuwa unakama mabaka umebabuka aisee nime angaika Sana kumtibia mpaka nakata tamaa
Soma Zaidi...Namna ya kufunga kitovu cha mtoto.
Posti hii inahusu zaidi njia au namna ya kufunga kitovu cha mtoto mara tu anapozaliwa, kwa kawaida tunafahamu kwamba ili mtoto aweze kuishi akiwa tumboni anategemea sana kula na kufanya shughuli zake kwa kupitia kwenye plasenta kwa hiyo mtoto akizaliwa tu
Soma Zaidi...Dalili za mama mjamzito akikaribia kujifungua
Post hii inazungumzia mama wajawazito Mara tu mama anapohisi kuwa yeye ni mjamzito anashauriwa kuanza clinic.na clinic hizi zinasaidia kuwapatia wakina mama elimu,namna ya kumkinga Mtoto asipatwe na maradhi Kama UKIMWI. Pia mama anapoanza clinic
Soma Zaidi...Mabadiliko kwenye mfumo wa chakula kwa wajawazito.
Posti hii inahusu zaidi mabadiliko kwenye mfumo wa chakula kwa wajawazito, ni mabadiliko ambayo utokea kwa wajawazito hasa kwenye mfumo wa chakula.
Soma Zaidi...mambo ambayo utaulizwa mama mjamzito ukifika kituo cha afya unatakiwa utoe majibu sahihi.
Posti hii inahusu zaidi mambo ambayo Mama mjamzito anaweza kuulizwa pindi anapokuja kwenye kliniki ya uzazi ,ni mambo muhimu na ya lazima yanayopaswa kuongea na Mama mjamzito ili kuweza kuona maendeleo yake kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...