Utajifunza dalili za fangasi mdomoni na ulimini, sababu za fangasi wa mdomoni na ulimini, matibabu yeke na njia za kukabiliana nao
Dawa ya fangasi kwenye mdomo na ulimi
Fangasi wanaweza kuathiri sehemu yeyote kwenye ngozi ya mtu. Kuanzia vidole, kichwa, kwapa, sehemu za siri na mapajani. Hutokea fangasi wakaathiri mdomo na ulimi. Hapa hali inaweza kuwa mbaya pale mtu akishindwa kula. Bila shaka ni maumivu, lakini leo nitakwenda kukutajia tiba yake.
Nini sababu ya fangasi wa mdomo na ulimi?
Fangasi hawa husababishwa na aina ya fangasi inayoitwa Candida albicans (C.albicans). hawa fangasi ni kawaida kupatikana kwenye mdomo. Kwa mtu ambaye kinga yake ipo imara hakuna shida yeyote anaweza kuipata kwa kuwa na fangasi hawa. Ila endapo watazidi kupitiliza ndipo inaweza kuleta shida.
Dalili za fangasi kwenye mdomo na ulimi
1.Vijidoma vyeupe au njano kwenye shavu kwa ndani, finzi, midomo na kwenye ulimi
2.Kuvuja kwa damu wa finzi
3.Vidonda kwenye mdomo
4.Kuhisi kama kuna pamba kwenye mdomo (vinyuzinyizi)
5.Ukavu wa kona za mdomo pamoja na mipasuko
6.Taabu katika kumeza
7.Mdomo kuwa na ladha mbaya
8.Kupotesa ladha ya unachokila.
Fangasi wa mdomoni wanaweza kuambukiza?
Yes wanaweza kuambukizwa kwa mfano ukimkisi (denda) mtu anaweza kupata fangasi hawa kama na wewe unao.
Dawa ya fanasi kwenye mdomo na ulimi
1.Fluconazole hiini ya kumeza
2.Clotrimazole (Mycelex Troche) ni kidonge pia cha kumumunyikia mdomoni
3.Nystatin (Nystop, Nyasta) ni ya kuosha mdomo
4.Itraconazole (Sporanox) ni ya kumeza, hupewa wale wenye usugu ama wenye HIV
5.Amphotericin B (AmBisome, Fungizone) hutumika kutibu hali mbaya zaidi ya fangasi wa mdomoni.
Nini ufanye ukiwa unatumia dawa hizi
1.Piga mswaki kwa mswaki ulio mlaini
2.Badili mswaki baada ya kumaliza dozi
3.Usitumie dawa za kuosha mdomo mpaka daktari akuambie.
4.Osha mdomo kwa maji ya chumvi
5.Changanya maji na juisi ya limao kisha knywa
Umeionaje Makala hii.. ?
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa ya chango na maumivu ya hedhi
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya griseofulvin ni dawa inayotumika kutibu fangasi za kwenye ngozi ambazo usababisha mabaka mabaka kwenye ngozi.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ibuprofen katika kutuliza maumivu, ni aina mojawapo ya dawa na yenyewe ufanya kazi kama aspirin na paracetamol
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa za fangasi na matumizi yake kwa kutumia dawa ya fluconazole kama dawa mojawapo ya fangasi.
Soma Zaidi...Nitakujuza dawa ya kutibu vidonda vya tumbo, na kutibu vidonda vya tumbo sugu
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dawa ya Albendazole katika kutibu Minyoo, ni Aina mojawapo ya dawa ambayo usaidia kutibu Minyoo inayosababishwa na bakteria mbalimbali.
Soma Zaidi...Zijuwe aina za minyoo na tiba yake. Dawa 5 za kutibu minyoo ya aina zote
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dawa ya lignocaine kama mojawapo ya Dawa ambayo utumika wakati wa upasuaji.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi madhara ya Tiba mionzi kwa wagonjwa wa saratani, ni madhara yanayotokea kwa wagonjwa wanaotumia mionzi katika matibabu ya saratani.
Soma Zaidi...