DAWA YA MAPUNYEMatibabu ya mapunye inategemea ni wapi mapunjye yapo.
DAWA YA MAPUNYE
Matibabu ya mapunye inategemea ni wapi mapunjye yapo. Mapunye yanaweza kuota kichwani, mikononi, mgongoni na maeneo mengine. Pia matibabu yatategemea ni kiasi gani mmtgu ameathiriwa na hayo mapunye. Mapunye yanayweza kibiwa na dawa za kupaka kama losheni za fangasi na poda zake. Miongoni mwazo ni:-
Dawa ya mapunye ya kupaka:
1.Clorimazole
2.Miconazole
3.Terbinafine
4.Ketoconazole
Endamp dawa hisi hazitaweza kumaliza mapunye, daktari anaweza kukuandikia dawa za kumeza amasindano. Katu dawa hizi usimeze kiholela bila ya kupata ushauri wa daktari. Dozi ya dawa hizi inaweza kwisha ndani ya mwezi mmoja ama ikaendelea mpaka miezi mitatu. Dawa hizi za mapunye za kumeza ni pamoja na:-
Dawa ya mapunye ya kumeza.
1.Terbinafine. Dawa hii inaweza kunywewa ndani ya wiki nn4. hata hivyo inaweza kukuletea mabadiliko kwenye mwili wako kama kichefuchefu, kuhara, kukosa choo na ukurutu. Si lazima mabadiliko haya uyaone kuna wengine hawaoni chochote.
2.Griseofulvin. Dawa hii inaweza kutumiwa kuanzia wiki 8 mpaka 10. Pia inaweza lupatikana katika mtindo wa kupulizia. Nayo inaweza kulete mabadiliko kama kuhara, kutapika, kichefuchefu, maumivu ya kichwa na kukosa choo. Dawa hii sio salama kwa wajawazit, ama kama upo katika harakati za kubeba mimba ama kama unanyonyesha.
3.Itraconazole. Dawa hii humezwa ndani ya siku 7 mpaka 15. si nzuri dawa hii kutumiwa na watoto wadogo, wazee na walio na maradhi ya ini. Dawa hii pia inaweza kukuletea mabadiliko kama maumivu ya kichwa, kichefuchefu, kutapika, kuhara na kukosa choo.
Njia za kujilinda dhidi ya mapunye.
1.Osha mikono yako kila unapogusa punye
2.Osha nguozako za kuvaa, kutandika na kujifunika na taulo.
3.Oga kila unapotoka kufanya kazi
4.Kama upo karibu na wanyama kama mbwa na paka hakikisha wapo salama na mapunye.
5.Usishiriki nguo zako na mwenye mapunye.
Umeionaje Makala hii.. ?
Post hii inahusu zaidi dawa ya propranolol katika matibabu ya magonjwa ya moyo, dawa hii ipo kwenye kundi la beta blockers na ufanya Kazi mbalimbali hasa kwa wagonjwa wa moyo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu dawa za kutibu mafua ambazo ni cough seppessants na nasal congestion ni dawa ambazo zimependekezwa kwa ajili ya kutibu mafua.
Soma Zaidi...kama unasumbuliwa na fangasi uumeni, nitakujuza dawa yake, sababu za fangasi uumeni, matibabu yake na njia za kuwaepuka
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa mbadala za vidonda vya tumbo
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya aminophylline katika kutuliza maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi mgawanyiko wa tiba ya kifua kikuu, kwa kawaida tiba hii imegawanyika katika sehemu kuu mbili.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya Prednisone ambayo usaidia katika kupambana na aleji.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya ampicillin, ni mojawapo ya dawa za kutibu maambukizi ya bakteria kwenye mwili wa binadamu ba pia ni dawa ambayo IPO kwenye kundi la penicillin kundi hili kwa kitaa huitwa broad spectrum penicillin
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya Sp , kirefu cha dawa hii ni sulphadoxine na pyrimethamine hii dawa ilitumika kutibu malaria kwa kipindi fulani lakini sasa hivi imebaki kutumiwa na wajawazito kama kinga ya kuwazuia kupata malaria.
Soma Zaidi...