picha

Dawa ya kutibu minyoo

Zijuwe aina za minyoo na tiba yake. Dawa 5 za kutibu minyoo ya aina zote

Dawa ya kutibu minyoo

DAWA YA MINYOO
Minyoo ni wadudu aina ya parasite ambao wanaingia kwenye miili ya kiumbe hai kama wanyama na binadamu, na wanajipatia chakula chao humo na kuishi. Kwa binadamu kuna minyoo aiina nyingi sana inayo weza kuwaathiri. Ila zipo aina tatu ambazo zinaonekana ni zaidi kuathiri binadamu. Nazo ni kama:-



1.Minyoo aina ya Roundworms hawa wanaingia kwenye miili yetu kupitia vyakula tunavyokula ama vinywaji endapo hivyo vyakula ama vinywaji vitakuwa na mayai yao. Minyoo hawa wanataga na kuishi kwenye utumbo. Minyoo hawa ni pamoja na threadworm, ascaris, hookworm na trichuris.



2.Minyoo aina ya tapeworm, hawa hishi kwenye tumbo, mara nyingi tunaweza kuwapata minyoo hawa kwa kula chakula ambacho hakikupikwa ama hakikuwiva vyema kama nyama, mihogo mibichi n.k



3.Flukeworms, minyoo hawa huingia mwilini mwetu na kuishi kwenye damu, tumbo, mapafu ama kwenye ini. Unaweza kuwapata minyoo hawa kwa kuogelea ama kuoga kwenye maji yenye minyoo hawa. Mimnyoo hawa husababisha pia ugonjwa ujulikanao kama kichocho (schistosomiasis).



Ni dawa gani hutibu minyoo?
Kwa ufupi tiba ya minyoo hutofautiana kulingana na aina ya minyoo na kiasi cha athari ndani ya mwili. Kwa kiasi kikubwa dawa aina ya Mebendazole imekuwa ikitumika kwa kiasi kikubwa sana maeneo mengi. Na hii ni kwa sababu dawa hii inatumika sana kutibu minyoo aina ya threadworm ambao minyoo hawa ndio wanaathiri watu zaidi. Pia inaweza kutibu aina nyinginyingi za minyoo. Dawa nyingine za kutibu minyoo ni:-



1.Levamisole
2.Tiabendazole
3.Ivermectin
4.Niclosamide
5.Praziquantel
6.Albendazole
7.Diethylcarbamazine



Dawa hizi zinafanyaje kazi?
Yes hili ni swali zuri sana. Sasa inakupasa ujuwe namna ambavyo dawa hizi zitakusaidia kutibu minyoo. Dawa hizi zinafanya kazi kama ifuatavyo:-



A.Mebendazole, albendazole na tiabendazole hizi kuzuia minyoo isifyonze chakul (sugar) kutoka kwenye miili yetu. Hivyo wanaweza kufa kwa njaa. Ila dawa hii itauwa minyoo lakini sio mayai yao ambayo wameyataga tayari.



B.Praziquantel na ivermectin, dawa hizi husaidia kuwazubaisha minyoo kwenye utumbo, hivyo wanaweza kutolewa kwa njia ya haja kubwa.





                   



Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Dawa Main: Afya File: Download PDF Views 6047

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 ai web app    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉4 Simulizi za Hadithi Audio    👉5 web hosting    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Dawa za kutibu ugonjwa wa macho

Somo Hili linakwenda kukuletea dawa za kutibu ugonjwa wa macho

Soma Zaidi...
Dawa za fangasi ukeni

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za fangasi ukeni

Soma Zaidi...
Miungurumo haiishi tumboni nikishika upande wa kushoto wa tumbo kuna maumivu kwa mbali je mm nitumie dawa gan kuondoa tatizo hilo

Kukawa na gesi tumboni kunaweza kuwa ni dalili ya shida kwenye afya, hasa katika mfumo wa chakula. Hali itakuwa sio nzuri endapo utakosea hamu ya kula na kuhisivkushiba muda wowote.

Soma Zaidi...
Dawa ya fangasi ukeni

Usisumbuliwe tene na fangasi ukeni, zijuwe hapa dalili za fangasi ukeni, tiba yake na njia za kukabiliana na fangasi ukeni

Soma Zaidi...
Ijue Dawa ya lignocaine

Posti hii inahusu zaidi dawa ya lignocaine kama mojawapo ya Dawa ambayo utumika wakati wa upasuaji.

Soma Zaidi...
Dawa ya quinenes katika kutibu Malaria

Post hii inahusu zaidi dawa e quinine katika kutibu Malaria ni dawa inayotibu Ugonjwa wa Malaria ikiwa dawa nyingine zimeshindwa kufanya kazi.

Soma Zaidi...
Kazi za Dawa ya Artesunate katika kutibu Malaria

Posti hii inahusu zaidi kazi za dawa ya Artesunate katika kutibu Malaria kali, ni dawa ambayo inatumika sana kutibu Malaria kali.

Soma Zaidi...
Fahamu kazi ya dawa ya ampicillin inayopambana na maambukizi ya bakteria

Post hii inahusu zaidi dawa ya ampicillin, ni mojawapo ya dawa za kutibu maambukizi ya bakteria kwenye mwili wa binadamu ba pia ni dawa ambayo IPO kwenye kundi la penicillin kundi hili kwa kitaa huitwa broad spectrum penicillin

Soma Zaidi...
Tiba mbadala za vidonda vya tumbo

Somo hili linakwenda kukuletea tiba mbadala za vidonda vya tumbo

Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu dawa ya propranolol ambayo hutibu magonjwa ya moyo

Post hii inahusu zaidi dawa ya propranolol katika matibabu ya magonjwa ya moyo, dawa hii ipo kwenye kundi la beta blockers na ufanya Kazi mbalimbali hasa kwa wagonjwa wa moyo.

Soma Zaidi...