Dawa ya Vidonda vya tumbo
Nitakujuza dawa ya kutibu vidonda vya tumbo, na kutibu vidonda vya tumbo sugu
DAWA YA VIDONDA VYA TUMBO
Dawa za vidonda vya tumbo zinategemea aina za vidonda alivyo navyo, mahala vilipo na sababu za vidonda hivyo. Kitu cha kwanza kuangalia ni sababu gani zilizopelekea vidonda hivyo?. kisha baada ya kuijuwa sababu ndipo maibabu yatafuata. Kama tulivyokwisha jifunza kuwa sababu kuu za vidonda vya tumbo ni bakteria aina ya Hypylori. Hivyo kama sababu ni hii mgonjwa atapewa dawa ya kuwauwa hawa bakteria. Pia kama sabau ni asidi tumboni atapewa dawa za kupunguza uzalishwaji wa hizi asidi. Dawa za vidonda vya tumbo ni kama zifuatazo:-
1.Dawa kwa ajili ya kuuwa bakteria. Hapa mgonjwa atapewa dawa kama:-
A.Amoxicillin (amoxil)
B.Clarithromycin (Biaxin)
C.Metronidazole (flagyl)
D.Tinidazole (tindamax)
E.Tetracyline
F.Levolaxacin
2.Dawa za kuzuia uzalishwaji wa asidi mwilini (proton pump inhibitors (PPIs))
A.Omeprazole (Prilosec)
B.Lansoprazole (Prevacid)
C.Rabeprazole (Aciphex)
D.Esomeprazole (Nexium)
E.Panztoprazole (Protonix)
3.Dawa za kupunguza uzalishwaji wa asidi tumboni (Acid blockers (histamine (H-2))
A.Famoditine (Pepcid AC)
B.Cimetidine (Tagamet HB)
C.Nizatidine (Axid AR)
4.Dawa zinzzolinda ukuta wa utumbo na tumbo
A.Cytoprotective agents
B.Sucralfate (Carafate)
C.Misoprostol (Cytotec)
TIBA MBADALA ZA VIDONDA VYA TUMBO.
Wataalamu wa afya pia wanakubali uwepo wa tiba mbadala katika kutibi vidonda vya tumbo. Zipo nyingi sana, miongoni mwazo ni:-
A.Bamia
B.Kitunguu thaumu
C.Asali
Kwa nini vidonda haviponi hata baada ya kutumia dawa?
Hii hutokea endapo:-
A.Kama mgonjwa hakutumia dawa kwa kufuata masharti vyema
B.Haswa kuna baadhi ya bakteria wa vidonda vya tumbo wana usugu wa kufa na dawa
C.Kama unatumia tumbaku
D.Kama unatumia dawa za NSAIDs
Pia mara chache vidonda vya tumbo vinaweza kusababishwa na:-
A.Uzalishwaji wa asidi kupitiliza
B.Mashambulizi mengie yasiyo ya H.pylori
C.Saratani ya tumbo
D.Kuwa na maradhi mengine
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 web hosting 👉2 Bongolite - Game zone - Play free game 👉3 Simulizi za Hadithi Audio 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
Neno la awali
Asalaamu alykum warahmatullah wabarakaatuh Sifanjema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe, muumba wa mbingu na ardhi na vilivyomo.
Soma Zaidi...Ijue dawa ya sulphadoxine na pyrimethamine (sp)
Post hii inahusu zaidi dawa ya Sp , kirefu cha dawa hii ni sulphadoxine na pyrimethamine hii dawa ilitumika kutibu malaria kwa kipindi fulani lakini sasa hivi imebaki kutumiwa na wajawazito kama kinga ya kuwazuia kupata malaria.
Soma Zaidi...Fahamu tiba ya jino
Post hii inahusu zaidi tiba ya jino,ni tiba ya kawaida kwa watu walio na matatizo ya meno, kwa kawaida tunafahamu kwamba jino huwa halina dawa ila dawa yake huwa ni kungoa lakini Leo nawaletea habari njema kwamba jino sio kungoa tena ila Kuna tiba ambayo
Soma Zaidi...dawa ya minyoo, dalili za minyoo na sababu na vyanzo vya minyoo
MWISHO Mwisho tunapenda kusema kuwa unapohisi una minyoo kutokana na dalili ambazo tumezitaja humu, nenda kituo cha afya ukapate ushauri zaidi.
Soma Zaidi...Fahamu dawa za kutibu mafua
Post hii inahusu dawa za kutibu mafua ambazo ni cough seppessants na nasal congestion ni dawa ambazo zimependekezwa kwa ajili ya kutibu mafua.
Soma Zaidi...