Dawa ya kutibu maumivu ya jino
Utaijuwa Dawa ya maumivu ya jino, sababu za maumivu ya jino na njia za kujikinga na maumivu ya jino
Dawa ywa maumivu ya jino.
Maumivu ya jino ma kwa jina lingine hufahamka kama odontalgia, ni maumivu makali yanayoweza kutokea kwenye ufinzi, mdomo na mifupa inayolishika jino. Maumivu haya yanaweza kuwa makali sana kiasi cha mtu kuomba msada. Wakati mwingine maumivu haya hutokea baada ya kula vitu ama kufanya jambo lakini hii sio lazima. Huwenda pia yakatokea bila hata ya sababu yeyote ile.
Je na wewe ni miongoni mwa wanaosumbuliwa na maumivu ya meno. Makala hii ni kwa ajili yako. Utajifunza sababu za maumivu ya jino, yanatokeaje, utakabiliana vipi na dawa gani utumie. Kama ukipenda makala hii usiwache kututupia maoni hapo chini:-
Sababu za kutokea maumivu ya jino:
1.Kuwa na majeraha kwenye jino ama kuzungukia jino. Majeraha ni kawaida sana kusababisha kubenduka na kukatika kwa meno.
2.Maambukizi na mashambulizi ya jino yaliyosababishwa na wadudu.
3.Kusaga ma kugonga meno hasa wakati wa usiku unapolala
4.Kuwa na magonjwa kwenye ufinzi
Dalili za maumivu ya jino
1.Maumivu wakati unapotafuna
2.Kuhisi mabadiliko endapo hali ya hewe itabadilika
3.Kuvimba kwa shavu ama kidevu
4.Mafinzi kutoa damu ama kutoma majimaji
5.Maumivu ya kichwa
6.Homa
7.Maumivu ya sikio
8.Kupotea kwa ladha ya chakula
9.Maumivu ya shingo
Dawa ya maumivu ya jino
Kuna matibabu kadha anaweza kupatiwa mgonjwa kama kung’oa jino, kuuwa bakteria kama ndio sababu. Pia kutumia dawa za kupunguza maumivu. Miongoni mwa dawa za maumivu ya meno ni:-
1.Ibuprofen
2.Naproxen
3.Acetaminophen
NITAJILINDA VIPI MA MAGONJWA YA MENO?
1.Punguza kula vitu vyenye sukari nying kwa wingi kama pipi
2.Safisha kinywa kwa mswaki kara kwa mara
3.Usilale na mabaki ya chakula mdomoni.
Dawa za mitishamba za kutibu meno
1.Kutumia muarobaini, unatafuna vijani vichanga na kuelekeza kwenye jino linalouma
2.Tafuna karafuu kuelekea kwenye jino linalouma
3.Tafuna kitunguu thaumu kuelekea jino linalouma
4.Bandua gome la muembe kish alichune gamba la juu, kisha chemsha hilo gamba kisha kunywa.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Madrasa kiganjani 👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉3 Kitabu cha Afya 👉4 Simulizi za Hadithi Audio 👉5 ai web app 👉6 Kitau cha Fiqh
Post zinazofanana:
Dawa za kutibu ugonjwa wa macho
Somo Hili linakwenda kukuletea dawa za kutibu ugonjwa wa macho
Soma Zaidi...Ijue dawa ya sulphadoxine na pyrimethamine (sp)
Post hii inahusu zaidi dawa ya Sp , kirefu cha dawa hii ni sulphadoxine na pyrimethamine hii dawa ilitumika kutibu malaria kwa kipindi fulani lakini sasa hivi imebaki kutumiwa na wajawazito kama kinga ya kuwazuia kupata malaria.
Soma Zaidi...Fahamu dawa ya haloperidol katika matibabu ya akili
Post hii inahusu dawa ya haloperidol katika matibabu ya magonjwa ya akili, ni mojawapo ya dawa ambayo utumiwa na wagonjwa ambao wamechananyikiwa.
Soma Zaidi...Fahamu kuhusu dawa ya mebendazole
Post hii inahusu zaidi dawa ya mebendazole ni dawa ambayo utumika kutibu minyoo ambayo utokea kwa watoto na watu wazima.
Soma Zaidi...