Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)
5.0. HAKI NA UADILIFU KATIKA UISLAMU.
5.1. Dhana ya Haki na Uadilifu katika Uislamu.
Maana ya Haki kwa Mtazamo wa Uislamu.
Ni muunganiko wa sheria na maadili kwa lengo na madhumuni ya kuilea jamii katika amani, furaha, udugu wa kweli na mahusiano mema kati ya wanaadamu.
Misingi ya Haki na Uadilifu katika Uislamu.
Maisha ya furaha na amani ya kweli hupatikana kwa kusimama misingi ya haki na Uadilifu katika jamii kama ifuatavyo;
Tawhiid.
Haki na Uadilifu wa kweli hupatikana kwa kumuamini na kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w) ipasavyo katika maamrisho na makatazo yake.
Utume.
Katika kumuamini na kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w) ni kufuata misingi ya miongozo ya mitume wake wote kupitia vitabu vyao.
Siku ya Mwisho.
Kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w) katika maisha yetu ni kuzingatia kuwa kila kitendo kitahukumiwa na kulipwa kwa haki siku ya Kiyama.
Umeionaje Makala hii.. ?
Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kujitwaharisha kutokana na najisi.
Soma Zaidi...Hapa utajifinza uharamu wa riba na sababu za kuharamishwa kwake.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukugundisha kuhusu maana halisi ya ibada ya swala.
Soma Zaidi...