image

Dua ambazo hutumiwa katika swala

Post hii inakwenda kukugundisha dua ambazo itazitumia katika swala yako.


DUA ZA SWALA
1.Dua ya kufungulia swala (Duau al-iftitah)
Kusoma dua ya kufungulia swala ni sunnah. Katika Hadithi ya Bukhari na Muslim iliyosimuliwa na Abu Hurairah (r.a), baada ya kuhirimia swala Mtume (s.a.w) alikuwa akileta dua ifuatayo:

“wajahtu wajhi lilladhi fatwaras-samaawat wal-ardha hanifam-muslima wamaa kaana minal-mushrikina. Inna swalatiy wanusukii, wamah-haya, wamaamatiy, lillahi rabil-alamiina laa sharikalahu wabidhalika umirtu wa-ana minal-mushrikiina.”

Tafsiri:
“Nimeuelekeza uso wangu kwa yule aliyeziumba mbingu na ardhi. Nimeacha dini za upotovu. Mimi si miongoni mwa washirikina. Hakika swala yangu (na ibada zangu zote) na uzima wangu na kufa kwangu (yote) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, bwana (Rabbi) wa walimwengu wote. Hana mshirika wake. Na haya ndio niliyoamrishwa na mimi ni wa kwanza walio jisalimisha kikamilifu kwa Mwenyezi Mungu. (6:79, 162-163)

2.Kusoma al-hamdu (surat al-fatiha)
Baada ya kusoma dua ya kufungulia swala mtu atasoma alhamdu. Na kusoma al-hamdu ni nguzo ya swala.Tunasoma suratul-Fatiha kama ifuatavyo:- Bismillahir Rahmaanir Rahiim (1) Alhamdu liLLahi rabbil-’Aalamiin (2). Rrahmaanir Rahiim (3) Maaliki yaumiddiin (4) Iyyaakana‘abudu waiyyaaka nasta‘iin (5) Ih dinasw-swiraatwal mustaqiim (6) Swiraatwa lladhiina an ‘amta ‘alaihim; ghairil maghdhuubi ‘alaihim wala dhw-dhwaaliin (7)

Tafsri:
(1) Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na mwenye kurehemu: (2) Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu, Mola wa Walimwengu wote: (3) Mwingi wa Rehema mwenye kurehemu (4) Mwenye kumiliki siku ya malipo: (5) Wewe tu ndiye tunayekuabudu, na wewe tu ndiye tunaye kuomba msaada: (6) Tuongoze njia iliyonyooka: (7) Njia ya wale uliowaneemesha; siyo (ya wale ) waliokasirikiwa, wala ya wale waliopotea.

3.Kurukuu.
Katika rukuu ni sunnah kusoma dua hii Katika rukuu ni sunnah kumsabihi Allah (s.w) kwa kusema kimya kimya mara tatu au zaidi
“Subhana Rabbiyal’Adhiim”

Tafsiri:
“Utukufu ni wako Ee Bwana (Mlezi) wangu Uliye mkuu”

4.Kuitidali (kusimama wima kutoka kwenye rukuu)
wakati wa kunyanyuka maneno haya:“sami’a llahu liman hamidahu” Mwenyezi Mungu anamsikia kila mwenye kumhimidi. Na baada ya kusimama sawa ni sunnah kusema “rabbanaa walakal-hamdu”ewe mola wetu sifa zote za ukamilifu ni zako. Pia ni sunnah kusema maneno haya
“rabbanaa walakal-hamdu mil-as-samaawati wamil-al-ardhi wamil-amashi-ita minshai-in ba’adah”
Tafsiri:
Ewe Mola wetu sifa zote za ukamilifu ni za kwako, kutoka mbinguni, kutoka ardhini na katika vitu vyote vilivyo baina yao (mbingu na ardhi) na kutoka katika vinginevyo unavyo viridhia

5.Kusujudi utasema kwenye sijda:-
“subhaana rabbiyal-a’alaa”
Tafsiri:
utukufu ni wa kwako Mola uliye tukuka. (mara tatu au zaidi)

6.Kukaa kati ya sijida mbili.
Katika kikao hiki utasema:-
“rabbigh-firliy warhamnii wa’afinii warzuqniy”
Tafsiri:
Ewe Mola wangu nisamehe, na unirehemu, na unipe afya na uniruzuku

7.Tahiyyatu (maamkizi)
Haya ni maneno yanayosemwa katika kikao cha tahiyatu. Maneno haya ni:- “Attahiyyaatu lillaah, wasw-swalawaatu, watwa-yyibaatu, assalaamu ‘alaika ayyuhannabiyyu, warahmatullaahi wabarakaatuhu, assalaamu ‘alay-naa wa-’alaa ‘ibaadillaahi swswaalihiina. Ash-hadu an-llaailaaha illallaahu wa-ash-hadu anna Muhammadan ‘abduhuu warasuuluhu”.

Tafsiri:
“Maamkizi yote ni ya Allah, na swala zote na yote mazuri, Amani iwe juu yako, ewe Mtume na Rehma na Baraka za Allah. Na amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Allah. Ninashuhudia kuwa hapana Mola ila Allah. Na ninashuhudia kuwa Muhammad ni Mja na, ni Mtume wake”. (Muslim).

8.Kumswalia Mtume (s.a.w) kwenye tahiyyatu ya mwisho. Zipo aina nyingi za kumswalia Mtume (s.a.w). Hapa utasema maneno yafuatayo:-

“Allahumma swalli ‘alaa muhammad wa’alaa aliy Muhammad kamaa swallaita ‘alaa ibraahima wa’alaa ali ibraahim innaka hamiidum-majid. Wabaaik ‘alaa muhammad wa’alaa ali muhammad kamaa barakta ‘alaa ibraahima wa’alaa ali ibraahima innaka hamiidum-majid”

Tafsiri:
Ewe Mola mrehemu Muhammad na wafuasi wake kama ulivyomrehemu Ibrahim na wafuasi wake hakika wewe ni mtukufu na msifiwa wa haki. Ewe Mola mbariki Muhammad na wafuasi wake kama ulivyombariki Ibraahim na wafuasi wake hakika wewe ni wewe ni mtukufu na msifiwa wa haki.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1804


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Dua sehemu 03
Zijuwe njia ambazo Allah hujibu Dua yako. Tambua kama umejibiwa dua yako au bodo, soma darsa za dua hapa. Soma Zaidi...

AINA ZA HADITHI
Aina za HadithKuna aina kuu mbili za Hadith- (a) Hadith Nabawiyyi. Soma Zaidi...

Namna ambazo Allah hujibu dua ya mwenye kuomba.
Post hii inakwenda kukufundisha namna ama staili ambazo Allah hujibu dua za watu. Soma Zaidi...

DUA 85 - 93
SWALA YA MTUME 85. Soma Zaidi...

NYAKATI AMBAZO DUA HUJIBIWA
NYAKATI AMBAZO DUA HUJUBIWA. Soma Zaidi...

HADITHI NA SUNNAH
1. Soma Zaidi...

DUA 113 - 126
DUA ZA WAKATI WA SHIDA Dua ya wakati wa taabu “LAA ILAAHA ILLA-LLAHUL-’ADHIMUL-HALIIMU. Soma Zaidi...

Darsa za Dua
Download kitabu hiki na upate kusoma zaidi ya dua 120, pamoja na darsa mbalimbali za dini ya kiislamu. Soma Zaidi...

DUA ZENYE MANENO HAYA HUJIBIWA
SIFA ZA (MANENO NA MATAMSHI YA) DUA YENYE KUJIBIWA. Soma Zaidi...

Hadithi Ya 40: Kuwa Duniani Kama Vile Mgeni Au Mpita Njia
Soma Zaidi...

Matendo ('amal) hulipwa kutokana na nia (makusudio)
Soma Zaidi...

Hadithi Ya 27: Uadilifu Ni Tabia Nzuri
Soma Zaidi...