13.
13. Dua kabla ya salamu
Ni sunnah kuleta dua kabla ya salamu. Dua hizi ni nyingi ila miongoni mwanzo ni
Dua aliyotufundisha Mtume (s.a.w) kwa msisitizo mkubwa kama tunavyofahamishwa katika Hadithi ya Muslim, iliyosimuliwa na Ibn Abbas, ni hii ifuatayo: Allahumma Inni-audhubika min-โadhaabi-lqabri,Wa-auudhubika min fitnatil masiihi-ddajjaal, Wa-auudhubika min fitnatil-mahyaa wal-mamaati, โEe Allah najikinga kwako kutokana na adhabu ya kabr, na najikinga kwako kutokana na fitina za masiihi Ddajjaal na najikinga kwako kutokana na matatizo ya maisha na mauti.
Sijidat-Sah-wi (Sijda ya kusahau)
Sijdat Sah-wi ni sijidah anayoileta mtu kabla ya kutoa salaam ili kufidia kitendo cha sunnah alicho kisahau kwa mfano kusahau kukaa tahiyaatu ya kwanza.Vile vile mtu akisahau au akikosea jambo lolote ambalo halibatilishi swala kwa mfano akaswali rakaa tano badala ya rakaa nne kwa swala ya Adhuhuri. Kabla hajamaliza swala alete sijidat Sahau. Hivi ndivyo tunavyojifunza kutokana na Hadithi zifuatazo: Abdullah bin Masโud (r.a) amesimulia: Mtume wa Allah alituswalisha Adhuhuri rakaa tano.Tukamuuliza kama pameamrishwa na Mwenyezi Mungu kurefushwa swala akajibu, La! Tukamuambia: โUmetuswalisha rakaa tano. Akasema (Mtume): Mimi ni binaadamu kama nyinyi, nakumbuka kama mnavyokumbuka na nasahau kama mnavyosahau. Kisha akasujudu sijdah mbili zikawa ni fidia kwa kusahau. (Bukhari na Muslim).
Muhimu:
Kumbuka kuwa sijda hii Mtume (s.a.w) aliileta baada ya kutoa salaamu na baada ya kukumbushwa. Abdullah bin Buhaymah (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) aliswalisha swala ya adhuhuri, akasimama baada ya rakaa mbili, alipomaliza swala akasujudu mara mbili huku akisema: โAllah Akbarโ katika kusujudu na katika kuinuka, wakati amekaa kabla ya kutoa salaam, na watu wakasujudu pamoja naye. Hii ilikuwa ni kufidia ile tahiyyatu ya mwanzo aliyoisahauโ. (Muslim)
14. kutoa salamu.
Kutoa salamu ni nguzo katika nguzo za swala. Ukamilifu wa kutoa salamu ni kusema โas-salaamu alykum warahmatullahi wabarakaatuhโ salamu zipo mbili yakwanza utatoa upande wa kulia na ya pili utatoa upande wakushoto. Sifa ya kugeuka kwa kutoa salamu ni kuwa utageuka mpaka mashavu yawze kuonekana kwa mtu aliye nyuma.
Umeionaje Makala hii.. ?
Post hii itakwenda kukugundisha masharti yanayofungamana na kukubaliwa kwa dua.
Soma Zaidi...ุนููู ุฃูู ูู ุงููู ูุคูู ูููููู ุฃูู ูู ุนูุจูุฏู ุงูููููู ุนูุงุฆูุดูุฉู ุฑูุถููู ุงูููููู ุนูููููุงุ ููุงููุชู: ููุงูู: ุฑูุณูููู ุงูููููู ุตูู ุงููู ุนููู ู ุณูู "...
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha maana ya neno sunnah katika Uislamu. Pia utajifunza maana ya neno hadithi katika uislamu
Soma Zaidi...Posti hii inakwenda kukufundisha ni kwa nini dua ya kafiri inawwza kujibiwa wakati ya muumini haijibiwi.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha matamshi ambayo mtu akiyatamka Allah hujibu dua hiyo kwa urahisi.
Soma Zaidi...Historia ya uandishi wa hadithibwakati wa Matabiina, yaani wafuasi wa maswahaba
Soma Zaidi...Soma dua mbalimbali za kila siku ambazo unatakiwa uzijuwe. Dua 120 ambazo muislamu anatakiwa kuzijua
Soma Zaidi...