Dua za kuomba wakati unapokuwa na maumivu kwenye mwili
Posti hii inakwenda kukufundisha dua za kuomba wakati wa kuwa na maumivu kwenye mwili wako.
DUA ZA KUONDOA MAUMIVU MWILINI
Katika uislamu Allah amejaalia dawa katika kufuata sunnah. Hakuna haja ya kumeza dawa za kupunguza maumivu kwa mwenye kumuamini Allah. Ila watu wasielewe vibaya maneno haya, maaana Mtume (s.a.w) amesisitiza watu wajitibu, ila pia ieleweke Allah amejaalia kuwa qurani ni dawa na ni ponyo kwa maradhi na mabo mengine. Leo hapa nimewaandalia dawa ya kuondowa maumivu katika sunnah nayo ni dua ambayo mtume (s.a.w) alikuwa akiwafundisha masahaba waombe pindi wakiwa na maumivu na maradhi.
1.Mtume (s.a.w) alimwambia swahaba kuwa: “weka mkono wako pale unaposikia maumivu katika mwili wako kisha sema “BISMILLAHI” mara tatu kisha useme mara saba (maneno haya): “A’UDHU BILLAHI WAQUDRATIHI MIN-SHARI MAA AJIDU WA-UHAADHIRU”. Hadithi hii ni sahihi na amepokea Muslim, Abu Daud na Ibn Maajah kutokana na masimulizi ya ‘Uthman Ibn Abil-”As.
2.Mtume (s.a.w) alimwambia Mainuna bint Abi Ubay kuwa :”weka mkono wako wa kulia pale panapokupatia maudhi (maumivu) kisha sema “BISMILLAHI ALLAHUMMA DAAWINI BIDAWAAIKA WASHFINII BISHAAIKA WAGHANII BIFADHLIKA ‘AN-MAN SIWAAKA WAHDHUR ‘ANII ADHAAKA” (Amepokea Tabrany)
3.Mume (s.a.w) alimwambia Asmaa bint AbuBakar kuwa: “weka mkono wako (pende maumivu) na useme mara tatu “BISMILLAHI ALLAHUMMA ADH-HAB ‘ANNI SHARRA MAA AJIDU BIDA’AWATIKA NABIYYIKA TWAYYIBIL-MUBAARAKIL-MAKIIN ‘INDAKA. BISMILLAHI “ (Amepokea ibn “Asakir)
4.amesimulia Ibn ‘Abas (r.a) kuwa : “alikuwa Mtume (s.a.w) akitufundisha dua kwa ajili ya maradhi na maumivu yote tunayoyapata kuwa Mtu aseme: ‘BISMILLAHI, A’UDHUBILLAHIL-’ADHIIM MINSHARRI KULLI ‘ARQIN-NA’AARI, WAMINSHARRI HARRIN-NAHAARI” (Amepokea Ahmad, tirmidh na Alhaakim).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 kitabu cha Simulizi π2 Madrasa kiganjani π3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) π4 Bongolite - Game zone - Play free game π5 Kitau cha Fiqh π6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
Faida za Kusoma Surat Al-Mulk
Surat Al-Mulk (Sura ya 67 katika Qurβan) inajulikana kama sura yenye baraka nyingi na kinga kubwa kwa msomaji wake. Katika makala hii, tunaangazia siri za kiroho, faida za kusoma sura hii kila usiku, na jinsi inavyomkinga Muislamu na adhabu za kaburi. Pamoja na hayo, tutaangazia mafunzo ya kimaadili yanayopatikana ndani ya sura hii yenye aya 30.
Soma Zaidi...Jinsi ya kutoa salamu katika uislamu
MAkala hii itakwenda kukufundisha jinsi ya kutoa salamu kwenye uislamu
Soma Zaidi...DUA ZA KUONDOA WASIWASI
DUA ZA KUONDOA MAUMIVU MWILINI Katika uislamu Allah amejaalia dawa katika kufuata sunnah.
Soma Zaidi...Mzazi na msafiri na mwenye kudhulumiwa dua zao hujibiwa kwa haraka
Wapo watu kadhaa ambao waliomba dua hazirudi. Hapa nitakueleza wawili ambao ni mzazi na msafiri.
Soma Zaidi...