FAHAMU AINA MBALIMBALI ZA MAGONJWA NYEMELEZI YA MOYO


image


Posti hii inahusu zaidi aina mbalimbali za Magonjwa ya moyo,kwa kawaida tunajua wazi kuwa kuna moyo mmoja lakini moyo huo unaweza kushambuliwa na magonjwa kwa kila aina kwa mfano kuna Maambukizi kwenye mishipa ya moyo,au kubadilika kwa mapigo ya moyo na mambo mengine kama hayo kwa hiyo hayo yote ushambulia moyo mmoja.kwa hiyo aina ya magonjwa ya moyo ni kama ifuatavyo.


1. Kuathirika kwa mishipa ya moyo.

Kwa wakati mwingine kuna kuathirika kwa mishipa ya moyo ambayo kwa kitaalamu huitwa coronary artery, mishipa hii inaweza kupata Maambukizi na kushindwa kusafilisha damu kutoka kwenye moyo na kupeleka sehemu mbalimbali za mwili. Pengine mishipa inaweza kushindwa kusafilisha damu kwa sababu ya kuwepo kwa uchafu na mafuta kwenye mishipa hali hii usababisha moyo kusukuma damu kwa nguvu ili kuweza kukidhi mahitaji ya mwili hali hii usababisha kuaribika kwa mishipa ya moyo.

 

Kwa hiyo tunapaswa kupunguza vyakula vyenye mafuta mengi na kuhakikisha kuachana na vyakula vyenye sumu ambavyo Usababisha kuwepo kwa mafuta kwenye mishipa na kuwepo kwa uchafu kwenye mishipa kwa kuepuka mambo hayo tutaweza kuruhusu damu kusafili zaidi na kuepuka na kuaribika kwa mishipa ya damu.

 

3.Aina nyingine ya ugonjwa wa moyo ni mapigo ya moyo kwenda tofauti.

Kwa wakati mwingine mapigo ya moyo uenda haraka na kusababisha mtu kuwa  na jasho na pengine mtu anakuwa hatulii sehemu moja . Na pia kwa wakati mwingine kuna kipindi mapigo ya moyo yanaenda taratibu sana kwa hali hii umfanya mtu kupumua kwa shida . Na kuna kipindi kingine mapigo ya moyo uenda ovyoovyo bila mpangilio hali hii ni mbaya sana inaweza kusababisha matatizo mengine makubwa kama vile kupoteza maisha.

 

4.Kwa wahudumu na ndugu wa mgonjwa baada ya kuona dalili kama hizi wanapaswa kumpeleka mgonjwa hospitalini ili aweze kupata matibabu kwa sababu hali ya kubadilika ki mapigo huwa sio nzuri hasa kwa mgonjwa yule ambaye ni mara yake ya kwanza kwa sababu anaweza kupanic na kuona kuwa ndio mwisho basi tuwafariji na kuwa pamoja nao ili waweze kupata huduma za muhimu.

 

5. Aina nyingine ni ile ya moyo kushindwa kufanya kazi.

Kuna kipindi ambapo moyo unashindwa kufanya kazi kwa sababu mbalimbali kama vile kuwepo kwa kiasi kidogo cha damu kwenye mwili au Maambukizi kwenye valve za mishipa.kwa hiyo hali  hii isipogunduliwa mapema Mgonjwa anaweza kupoteza maisha kwa watu wenye tatizo kama hili wanaweza kutumia kifaa maalum ambacho usaidia moyo ili uweze kufanya kazi na pia kifaa hicho kwa kawaida huwa kinabadilika mara kwa mara kadri ya maoni ya wataalamu wa afya.

 

6.Kuna wakati mwingine moyo ushindwa kufanya kazi kwa ghafla kwa sababu ya matukio mbalimbali na kuna huduma ambayo utolewa kwa ajili ya kushutua moyo huduma hiyo uitwa cardiopulmonary Resuscitation, hii huduma utolewa kwa wale wenye utamaalamu na mafunzo maalum kwa ajili ya kushutua moyo uliosimama ghafla.

 

7. Kuna aina nyingine t Magonjwa ya moyo ambayo huwapata watoto

Kwa wakati mwingine watoto wanaozaliwa na ugonjwa huo kwa sababu kuna kesi mbalimbali zinazoonyesha kuwa mtoto amezaliwa na tundu kwenye moyo, hali hii utokea kwa sababu ya mtindo wa maisha kwa Mama wajawazito kama vile uvutaji wa sigara, utumiaji wa madawa ya kulevya wakati wa ujauzito na pia kutumia vileo vikali wakati wa ujauzito hayo yote usababisha watoto kuzaliwa na matundu kwenye Aorta.

 

8.Kwa hiyo ili kuepuka na matatizo haya wanawake wakati wa ujauzito wanapaswa kufuata mashariti ya wataalamu wa afya na kuachana na vileo, madawa ya kulevya, pombe kali na mambo kama  hayo ili kuweza kuepuka matatizo kama hayo wakati wa ujauzito, kwa hiyo akina Mama pia wahudhuria maudhurio yote ya kliniki ili kuweza kusikiliza mafundisho kwa sababu hayo mafundisho utolewa kila mwezi kipindi mama akiwa kwenye mahudhurio ya kawaida.

 

9. Aina nyingine ya Magonjwa ya moyo ni pamoja na moyo kutanuka.

Kuna kipindi ambapo moyo unataka  kusiko kwa kawaida kwa sababu ya kutanuka kwa misuli ambayo imeuzunguka moyo au kwa sababu ya kutanuka kwa kuta za moyo, kwa hiyo moyo unatumia nguvu sana kusukuma damu na kusababisha misuli yake kutanuka. Sababu kuu ambazo Usababisha moyo kutanuka ni kuwepo kwa presha kubwa juu. Kuwepo kwa Maambukizi kwenye mishipa ya moyo na mambo mengine kama hayo.

 

10. Aina nyingine ya magonjwa ya moyo ni kuwepo kwa Shinikizo la damu kwa kitaalamu huitwa blood pressure, ni hali ambayo utokea kama kuna presha iko juu kwa sababu ya moyo kutumia nguvu katika kusukuma damu au pengine kama mwili una Maambukizi vile usababisha kuwepo kwa shinikizo la damu au pengine ni kwa  sababu ya kuwepo kwa mafuta kwenye mishipa ya damu ambapo damu kidogo uruhusiwe kupita na hapo mwili unahitaji kiwango kikubwa cha damu, kwa hiyo moyo usukuma damu kwa nguvu na kusababisha shinikizo la damu.

 

11. Chembe ya moyo. Pia hii nayo ni aina ya magonjwa ya moyo kwa kawaida mgonjwa uhisi maumivu kwenye kifua hali hii inaweza kutokea kama mtu anafanya kazi au amekataa,  Maumivu pia uendana pamoja na kutokwa na jasho pia kukosa hewa safi, hasa hasa tatizo hili utokea kama mgonjwa hana damu ya kutosha mwilini.

 

12.Aina nyingine ni kufa kwa  sehemu ya misuli ya moyo.

Kuna wakati mwingine sehemu za misuli ya moyo zinakufa hali ambayo Usababisha moyo kushinwa kufanya kazi zake za kila siku na  tatizo kama halijulikana moyo unaweza kushindwa kufanya kazi zake kwa kila siku.

 

13. Aina nyingine ni damu kushindwa kusambaa.

Kuna kipindi moyo inasukuma damu na damu inashindwa kusambaa kwenye sehemu mbalimbali za mwili kwa sababu ya Maambukizi kwenye mishipa ya damu. Hali hii utokea kwa sababu ya kuwepo kwa mafuta kwenye sehemu mbalimbali za mishipa ya damu.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    2 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    3 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    4 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    5 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    6 Maktaba ya vitabu    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Mambo yanayohitajika kabla ya kuanza upasuaji
Posti hii inahusu zaidi mambo yanayohitajika kabla ya kuanza upasuaji ni mambo muhimu ambayo yanapaswa kufanyika kwanza na baadaye upasuaji unaweza kuendelea. Soma Zaidi...

image Dalili za ugonjwa wa upele
Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa upele, ni dalili au mwonekano wa mgonjwa wa upele. Soma Zaidi...

image Chakula cha minyoo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya minyoo Soma Zaidi...

image Huduma kwa wasioona hedhi
Posti hii inahusu zaidi msaada au namna ya kuwahudumia wale wasioona hedhi na wamefikiwa kwenye umri wa kuweza kuona hedhi. Soma Zaidi...

image Mambo muhimu ambayo mama mjamzito anatakiwa kuzingatia.
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Mambo ambayo mama mjamzito anatakiwa kuzingatia katika kipindi Cha ujauzito au mimba Soma Zaidi...

image Sababu za mtu kuwa na mfadhaiko au wasiwasi
Post hii inahusu sababu za mtu kuwa na mfadhaiko na wasiwasi, mfadhaiko ni nguvu fulani anayoisikia ndani mwake kwa sababu ya tukio la kushutushwa linalomfanya afikilie sana, Soma Zaidi...

image Dalili za ngozi kuwasha.
Posti hii inaonyesha kiufupi kabisa kuhusiana na dalili za ngozi kuwashwa. Soma Zaidi...

image Kuwepo kwa mabonge ya damu wakati wa hedhi
Posti hii inahusu zaidi kuwepo kwa mabonge ya damu wakati wa hedhi, tunajua kabisa wakati wa hedhi damu inapaswa kuwa nyepesi na ya kawaida ila kuna wakati mwingine inakuwa na mabonge zifuatazo ni sababu za kuwepo kwa mabonge ya damu wakati wa hedhi. Soma Zaidi...

image Dalili za fangasi Mdomoni.
Posti hii inaelezea kuhusiana na dalili za fangasi Mdomoni kwa watoto, vijana, watu wazima na mama wanaonyonyeshwa. Soma Zaidi...

image dalili za Uvimbe kwwnye jicho (sty)
Sty ni uvimbe mwekundu, chungu karibu na ukingo wa kope ambalo linaweza kuonekana kama jipu au chunusi. Sties mara nyingi hujazwa na usaha. Mtindo kawaida huunda nje ya kope lako. Lakini wakati mwingine inaweza kuunda kwenye sehemu ya ndani ya kope lako. Soma Zaidi...