image

Fahamu dawa ambazo uchangia kupungua kwa nguvu za kiume

Post hii inahusu zaidi dawa mbalimbali ambazo uchangia katika kupunguza nguvu za kiume , hii ni kwa sababu ya wataalamu mbalimbali wanavyosema

Dawa zinazochangia kupungua kwa nguvu za kiume.

1. Kutokana na kuwepo kwa tatizo kubwa la kupungukiwa na nguvu za kiume, Kuna wataalamu mbalimbali ambao wamefanya utafiti na kugundua kwamba, pamoja na mambo mbalimbali au mtindo wa maisha Kuna na baadhi ya madawa ambayo yanasababisha kupungua kwa nguvu za kiume, kwa hiyo kwa sababu ya matumizi ya mara kwa mara au pengine ni dawa za maisha kwa mtumiaji unakuta nguvu za kiume zinapungua hali ambayo usababisha mafarakano na kitoelewana kati ya wanandoa au wakati mwingine ndoa kuvunjika kabisa.

 

2.Kwa kawaida tunafahamu kabisa kwamba dawa inapoingia mwilini ni lazima kutibu na kwa wakati mwingine uingiliana na mfumo mwingine wa mwili ndio maana Kuna wakati watumiaji wa dawa wanaweza kutumia dawa Fulani na kuisi kizunguzungu, kutapika, kuharisha na mambo mengine kama hayo au kwa wakati mwingine mwili mzima unakuwa na viupele ,kwa hiyo hata na pengine dawa uingiliana na seli na homoni hali inayosababisha kubadilka kwa baadhi ya mifumo ya mwili.

 

3. Kwa hiyo kama dawa zinaweza kuingiliana na mifumo ya mwili pia uingia seli na homoni za kiume na kusababisha kupungua kwa nguvu za kiume kwa hiyo basi kwa watumiaji wa dawa ambazo nitaenda kuziongelea wakipatwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume wasishangae au kutafuta mchawi wajue kwamba ni matokeo ya dawa na pia sio wote wanaotumia dawa hizi wanapatwa na tatizo hili hapana ni wachache na pia kama dawa ni za kila siku na kwa maisha ni lazima kuzitumia Ili kuweza kuendelea na matibabu.

 

4 Dawa za kupunguza maumivu.

Hizi ni mojawapo kati ya dawa za kupunguza nguvu za kiume kadri ya utafiti mbalimbali wa wataalamu wa afya, kwa kawaida hizi dawa utumika sana na kila mtu huwa anazikimbilia, ila Kwa upande wa wanaume zinaleta matokeo Hasi ambayo ni upungufu wa nguvu za kiume, baadhi ya dawa hizi ni pamoja na aspirin , Panadol, pethidine, ibuprofen, Diclofenac na nyingine zota za maumivu, kwa hiyo matumizi ya dawa hizi kwa mara kwa mara sio Vizuri na maumivu kama yanaweza kuvumilika kunywa maji mengi na pumzika na maumivu ya Kawaida upungua .

 

5. Sio kwamba dawa hizi zisitumike kwa wanaume zitumike kama Kuna shida ila sio Mara kwa mara na kwa mazoea kwa sababu Kuna watu wanazozitumia na bado Wana nguvu zao za kiume kawaida, dawa hizi upunguza nguvu za kiume kwa sababu zikitumika uingiliana na homoni za uzazi na kuathiri nguvu za kiume hali inayopelekea wanaume wengi kushindwa kushiriki tendo la ndoa au kukosa kabisa hamu ya tendo la ndoa au anafanya tendo la ndoa kwa mda  mfupi sana kwa hiyo hali hii usababisha kuvunjika kwa ndoa au kitoelewana kwenye familia.

 

6. Vile vile dawa za kuzuia wasiwasi au kwa kitaamu kuzuia anxiety.

Kwa sababu ya kuwepo kwa matatizo mbalimbali kwenye jamii watu wengi wanakuwa na wasiwasi uliopitiliza kiasi, hali inayowafanya kutumia dawa za kupunguza wasi wasi bila dawa hizo hawawezi kuishi ila wengine kuchanganyikiwa kabisa, kwa hiyo dawa hizo utumika mara kwa mara wengine ni kila siku, kwa upande wa wanawake hamna shida ila kwa wanaume dawa hizi uingiliana na seli za uzazi pamoja na homoni za uzazi na kusababisha kupungua kwa nguvu za kiume kwa hiyo kwa watumiaji wa dawa hizi ikitokea wakapatwa na tatizo hili wasishangae.

 

7. Kwa hiyo hamu ya tendo la ndoa ukosa kabisa a Wala huwa hamfilikii mwenzake hali inayosababisha kupunguza mapendo kwenye ndoa na pengine mmoja asipokuwa na busara uweza kutoka nje ya ndoa, kwa hiyo kwa watumiaji wa madawa haya ya kupunguza wasiwasi wanapaswa kwanza kujifahamu na kujitahidi Ili kuwajali wenzao ingawa hawana hamu ya tendo la ndoa, na pia tunapaswa kufahamu kwamba sio kila watumiaji wa dawa hizi za kupunguza wasi wasi wanapatwana shida hii ila ni wachache kwa hiyo ni lazima kuendelea kutumia dawa ila nafuu ikipatikana ni vizuri kuachana na dawa hizi.

 

8. Watumiaji wa kutumia dawa za kuganda kwa damu,

Kuganda kwa damu mwilini ni tatizo ambalo huwakumba watu wengi mno , pia ni watu wengi wanaotumia dawa hizi na pia pasipokuwepo na dawa hizi ni matatizo kwoa, kadri ya wataalamu mbalimbali wamegundua kwamba Kuna asilimia sitini ya watumiaji wa dawa za kuzuia kuganda kwa damu wanakoswa nguvu za kiume, kwa hiyo kwa watumiaji wa dawa hizi ni vizuri kujifahamu Ili kuweza kupambana na tatizo hili, na pia kujilazimisha kuwarithisha wenzao hata kama hawahisi chochote Ili mradi kuendelea kutunza ndoa zao.

 

9. Dawa hizi za kuzuia kuganda kwa damu uingiliana na mfumo mzima wa via vya uzazi na kupunguza taratibu nguvu za kiume ila matumizi yakiwa ya mda mrefu na tatizo pia uongezeka,ila sio wote wanaotumia dawa hizi upatwa na tatizo hili la kupungukiwa na nguvu za kiume kwa hiyo watumiaji waendelee kutumia dawa zao kama kawaida Ili kuweza kupona vizuri na pia hata kama hawana hu ya kushiriki tendo la ndoa wanapaswa kujitahidi kuwarithisha wenzao kwa kuepuka hali ya kutoka nje ya ndoa.

 

10. Watumiaji wa dawa za kutibu kifua kikuu.

Watumiaji wa dawa za kutibu kifua kikuu nao pia wako kwenye risk kubwa ya kupungukiwa na nguvu za kiume kwa sababu ya dawa ambazo wanatumia na zenyewe ufanya Kazi kama dawa nyingine yaani uingiliana na mfumo wa via vya uzazi pamoja na homoni ambazo usaidia katika mfumo mzima unohiusika na nguvu za kiume kwa hiyo ni vizuri kuendelea kutumia dawa hizi za kifua kikuu kwa sababu katika uaminifu wa kutumia dawa vizuri na kwa maelekezo yake kupona ni kigusa,kwa hiyo ni vizuri kutumia dawa kwa uaminifu Ili kuweza kupata uponyaji wa haraka na kuepuka na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

 

11. Kwa hiyo watumiaji wa dawa za kifua kikuu sio watu wote wanaotumia dawa hizi za kifua kikuu wako kwenye risk ya kupungua kwa nguvu za kiume ila ni vizuri kuendelea kutumia dawa hizo na pia kama mtu amepatwa na janga hili ni vizuri kabisa kuelewa kwamba hatakuwa na hamu ya tendo la ndoa kwa hiyo ni vizuri kumrithisha mwenzake na kuepuka hali ya kutoka nje ya ndoa.

 

13. Vile vile na watumiaji wa dawa za shinikikizo la damu au kwa lugha ya kawa wagonjwa wa presha yaani zote za kupanda na kushuka nao wako kwenye hatari ya kupatwa na upungufu wa nguvu za kiume, kwa sababu ya mwingiliano wa dawa za presha na seli za uzazi pamoja na homoni za uzazi,kwa hiyo kwa watumiaji wa dawa hizi wanapaswa kuelewa hili ingawa sio wote wanaotumia dawa hizi za presha upatwa na tatizo hili ila waendelee kutumia ikitokea wamepatwa na hali hiyo wasishangae.

 

14. Pia watumiaji wa dawa za msongo wa mawazo pia na dawa za kuleta usingizi,

Kutokana na hali ya maisha Kuna watu wengine wanapatwa na tatizo la kuwepo na msongo wa mawazo na bila matumizi ya dawa wanaweza kuwa wehu na pia Kuna wengine hawawezi kusinzia mpaka watumie ndipo wasinzie, kwa sababu ya matumizi ya mara kwa mara ya dawa hizo , dawa uingiliana na mfumo wa uzazi pamoja na homoni za uzazi na kusababisha kupungua kwa nguvu za kiume,kwa hiyo kwa watumiaji waendelee kutumia dawa ila wakipatwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume wasishangae na wafahamu kwamba sio wote watumiaji wa dawa hizi wanakoswa nguvu za kiume.

 

15. Kwa hiyo kwa sababu ya kuongeza kwa magonjwa mbalimbali na pia dawa za kila siku hutumika hali ambayo usababisha upungufu wa nguvu za kiume na kusababisha madhara katika ndoa, kwa hiyo watumiaji wa madawa wanapaswa kuendelea kutumia dawa zao wakifahamu kwamba sio watu wote wanaotumia dawa wanapatwa na tatizo hili ila hali ikitokea wafahamu kwamba ni kwa sababu ya dawa.

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Dawa Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1022


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Fahamu dawa ya captopril katika matibabu ya magonjwa ya moyo
Post hii inahusu zaidi dawa ya captopril katika matibabu ya magonjwa ya moyo, ni dawa ambayo imo kwenye kundi la vasodilators na ufanya Kazi mbalimbali zinazousu magonjwa ya moyo. Soma Zaidi...

Fahamu dawa ambazo uchangia kupungua kwa nguvu za kiume
Post hii inahusu zaidi dawa mbalimbali ambazo uchangia katika kupunguza nguvu za kiume , hii ni kwa sababu ya wataalamu mbalimbali wanavyosema Soma Zaidi...

Ni dawa gani hatari kwa mjamzito?
Ukiwa mjamzito uwe makini sana katika kuchagua matumizi ya dawa. Vinginevyobinawwza kuwa hatari. Hapa nitakujuza dawa ambazo ni hatari kutumia kwa ujauzito wako. Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu dawa ya fluconazole.
Post hii inahusu zaidi dawa ya fluconazole ni dawa ya kutibu fangasi za aina au za sehemu mbalimbali, Soma Zaidi...

Fahamu dawa za kutuliza aleji au mzio
Post hii inahusu zaidi dawa hydrocortisone kwa kutuliza aleji au mzio, kwa kawaida Kuna mda mtu anapotumia dawa Fulani anakuwa na mabadiliko mbalimbali kama vile kifua kubana , viupele na mambo kama hayo. Soma Zaidi...

Dawa ya Rifampicin na kazi zake
Posti hii inahusu zaidi Dawa ya Rifampicin na kazi zake, hii ni dawa mojawapo inayotibu kifua kikuu kati ya Dawa zilizoteuliwa kutibu ugonjwa wa kifua kikuu. Soma Zaidi...

Chini ya Tumbo langu Kuna uchungu lakini si sana shinda ni ni?
Nini kinasababisha maumivu ya tumbo chini ya kitovu? Soma Zaidi...

Ijue Dawa ya lignocaine
Posti hii inahusu zaidi dawa ya lignocaine kama mojawapo ya Dawa ambayo utumika wakati wa upasuaji. Soma Zaidi...

Umuhimu wa kutumia dawa za ARV
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kutumia dawa za ARV kwa wathirika wa virusi vya ukimwi .pia tutangalia kwa undani mambo ya kuzingatia kwa wathirika wanaotumia ARV .pamoja na kujali watu wanaotumia dawa hizo . Soma Zaidi...

Dawa ya Vidonda vya tumbo
Nitakujuza dawa ya kutibu vidonda vya tumbo, na kutibu vidonda vya tumbo sugu Soma Zaidi...

dawa ya minyoo, dalili za minyoo na sababu na vyanzo vya minyoo
MWISHO Mwisho tunapenda kusema kuwa unapohisi una minyoo kutokana na dalili ambazo tumezitaja humu, nenda kituo cha afya ukapate ushauri zaidi. Soma Zaidi...

Tiba ya minyoo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu tiba ya minyoo Soma Zaidi...