Fahamu dawa ya aminophylline kutibi maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji

Post hii inahusu zaidi dawa ya aminophylline katika kutuliza maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji.

Fahamu dawa ya kutibu au kutuliza maumivu kwenye mfumo wa upumuaji.

1. Aminophylline ni mojawapo ya dawa ambayo ufanya kazi katika mfumo wa upumuaji kwa matibabu hasa ya asthma na pia kwa watu wenye tabia ya kubanwa na vifua wakati hali ya hewa inapobadilika na matatizo ya upumuaji kwa ujumla pia dawa hii utolewa kwa kupitia kwenye mishipa ya damu Ili kuweza kufanya kazi kwa haraka kwa mgonjwa.

 

2. Pia kwa mara chache huwa kwenye mfumo wa vidonge na pia wakati mwingine uweza kutolewa kwa kupitia kwenye matako na paja ila kwa upande wa matako na paja usababisha maupeke na maumivu na pia kwa kupitia kwenye damu utolewa taratibu walau kwa mda wa dakika ishilini au zaidi kidogo.

 

3. Dawa hii Ina kuwa na milligrams mia mbili hamsini na pia mills kumi na utolewa kwa utaratibu na pia dozi ubadilika kulingana na umri pamoja na Uzito.

 

4. Dawa hii huwa na maudhi madogo madogo kama vile kichefuchefu na kutapika, kizunguzungu, mapigo ya moyo kwenda mbio na pia inawezekana kuwepo kwa degedege hasa kwa watoto wadogo na kwa watu wazima ni mara chache sana 

 

 5. Iwapo kama Kuna matokeo ya kuwepo kwa degedege ni vizuri kutumia dawa ya diazepam Ili kuweza kutuliza hiyo degedege, kwa hiyo dawa hii inapaswa kueleweka kwamba Kuna watu ambao hawapaswi kutumia dawa hii ni wale wenye aleji na dawa hii na pia kwa wale wenye tatizo la kifafa wanapaswa kuitumia dawa hii kwa uangalizi maalumu na ikibidi wanapaswa kuitumia kwa uangalizi Fulani.

 

6. Pia dawa hii haipaswi kutumiwa kiholela au kwa mazoea Bali kwa utaratibu wa wataalamu wa afya Ili kuepuka madhara zaidi ambayo yanaweza kutokea.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/12/23/Friday - 03:26:52 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1118


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-