Fahamu dawa ya captopril katika matibabu ya magonjwa ya moyo

Post hii inahusu zaidi dawa ya captopril katika matibabu ya magonjwa ya moyo, ni dawa ambayo imo kwenye kundi la vasodilators na ufanya Kazi mbalimbali zinazousu magonjwa ya moyo.

Fahamu dawa ya captopril katika matibabu ya magonjwa ya moyo,

1. Dawa hii hasa usaidia kwa wagonjwa ambao presha zao huwa Iko juu mara kwa mara na pia kwa wagonjwa ambao Wana ugonjwa wa moyo ambapo kwa kitaamu ugonjwa huu wa moyo kwa kitaamu huiitwa heart failure, pia dawa hii utumiwa na watu wengi sana na wanashuhudia kupata unafuu kwenye matibabu yao.

 

2. Tunafahamu kwamba presha Ili iwe juu kwa kawaida mishipa ya damu inakuwa ni myembamba na kusababisha moyo kutumia nguvu katika kusambaza damu kwenye sehemu mbalimbali za mwili ,kwa hiyo katika hali hiyo ya moyo kutumia nguvu kusukuma damu presha kwa kawaida inakuwa juu kwa hiyo kwa matumizi ya dawa hii ya captopril usaidia kupanua mishipa na damu uweza kupitia kwa urahisi na kisukumwa kwenye sehemu mbalimbali za mwili kwa sababu ya shughuli maalumu.

 

3. Kwa hiyo pia dawa hizi pamoja na kufanya kazi vizuri Kuna pia matokeo ambayo Kwa kawaida utokea au kwa lugha nyingine tunaita maudhi madogo madogo ambayo ni pamoja na maumivu ya kichwa ya mara kwa mara hasa kwa wale wanaoanza matibabu mara ya kwanza ila wakizoea maisha uwa ni kama kawaida, pia Kuna Kipindi mapigo ya moyo yanakwenda mbio, maumivu ya kifua na pengine kifua kubana kabisa,na pia mwili wa mtumiaji wa dawa kuwa Mnyonge au kuishiwa nguvu kabisa.

 

4. Kwa hiyo maudhi madogo madogo kama yakitokea na kuisha kwa mda mfupi hakuna shida ila yakitokea kwa mda mrefu na kuleta matokeo mbalimbali ambayo hayaeleweki kwa mgonjwa ni vizuri kutoa taarifa kwa wataalamu wa afya,na vile vile dawa hizi hazitolewi kiholela Bali ni kwa uamuzi wa wataalamu wa afya.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2023/02/04/Saturday - 09:01:45 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 812


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-