Fahamu dawa ya cardiac glycoside katika matibabu ya magonjwa ya moyo

Post hii inahusu zaidi dawa ya cardiac glycoside katika matibabu ya magonjwa ya moyo,dawa maalum ambayo imo kwenye kundi hili la cardiac glycoside ni digoxin, ni dawa muhimu ambayo utumika kwenye mfumo wa vidonge mara nyingi.

fahamu kuhusu dawa ya digoxin katika matibabu ya magonjwa ya moyo.

1. Kama tulivyoona hapo juu ya kwamba dawa hii imo kwenye kundi la cardiac glycoside, dawa hizi mara nyingi usaidia pale kama damu imeshindwa kusambaa kwenye sehemu mbalimbali za mwili, ina uwezo wa kupanua mishipa na kueza kuruhusu damu inaweza kupita bila shida yeyote.

 

2. Pia dawa hizi inawezekana juwa na maudhi mbalimbali wakati wa kutumia ikiwemo  kutapika , kichefuchefu, kuharisha hali hizi utokea kwa sababu ya kuwepo kwa sumu ya dawa hasa kwa watumiaji wa dawa kwa mda mrefu.

 

3. Pamoja ha maudhui hayo kuna kipindi wagonjwa au watumiaji uihisi kizunguzungu au pengine kutojielewa kwa kitaalamu huitwa hallusination, hasa hasa kwa wale watu wazima ambao umri umeenda.

 

4. Na kwa walio wachache wanapata shida ya maumivu ya tumbo au pengine choo kinaweza kuwa kigumu au kuharisha mara kwa mara,

 

5. Kwa hiyo tunapaswa kufahamu watu mbalimbali wanaweza kutumia dawa hizi ya cardiac glycoside ila wale walio na presha ya kushuka hawapaswi kabisa kutumia kwa sababu dawa hizi ushusha presha iliyo juu kwa hiyo kwa wenye pressure ya kushuka wakiitumia wanaweza kupata madhara makubwa au pengine presha inashuka kabisa na kusababisha vifo.

 

6. Kwa hiyo dawa hizi tunapaswa kuzitumia kwa kufuata utaratibu wa wataalamu wa afya kwa hiyo kama tulivyoona hapo mwanzoni kwamba magonjwa ya moyo utofautiana kwa hiyo na tiba Nayo ni tofauti, kwa sababu hiyo dawa hizi haitumiki kiholela bali kwa utaratibu wa wataalamu wa afya.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2023/02/02/Thursday - 10:23:19 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 554


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-