Post hii inahusu zaidi dawa ya diazepam katika kutuliza kifafa, ni dawa ambayo matumizi yake yanaweza kuingilia pote kwenye kutuliza kifafa na pia kwa wagonjwa wa akili.
1. Dawa hii ya diazepam kazi yake ni kutuliza mtu mwenye kifafa aweze kusinzia ila akili yake iweze kutulia na kufanya kazi vizuri, pia dawa hii ufanya Kazi Ile Ile kwa wagonjwa wa akili ambapo kama mtu amecharuka na kwa kukosa kutulia tunaweza kumpatia dawa hii Ili akaweza kulala na kutulia na baadae akiamka akili inakuwa sawa kabisa.
2. Dawa hii inaweza kutumiwa pia na watu wenye akili sawa ila kwa sababu ya matatizo ya maisha wanaweza kuwa na wasiwasi na kutotulia kwa hiyo watu was hivi tunawapatia dawa hii , na pia hali ya kutotulia utofautiana Kuna wale wenye wasiwasi mkubwa Wana dozi yao na wale wenye wasiwasi ila sio mkubwa na wenyewe wanapewa dozi yao lengo na kazi ya diazepam ni kumfanya mgonjwa atulie na baadae akiamka anaamka akiwa sawa na akili inakuwa imeshajitengeneza sawa.
3. Kwa wale wenye wasiwasi wa kawaida usio mkubwa wanapewa kuanzia dozi kuanzia milligrams mbili na pia dozi inawezekana kuongezewa kulingana na hali ya mgonjwa, dozi hii inaweza kuendelea mpaka milligrams kumi na tano mpaka ishilini na pia mgonjwa upata dawa ndani ya masaa manane na pamoja na dawa hii kuleta usingizi Ili kufanya ubongo kuwa sawa na Kuna dozi ya wale watu wenye usingizi unaopita kiasi wenyewe wanapewa dozi tofauti kuanzia milligrams tano na mwisho ni kumi na tano.
4. Dozi ya wasiwasi wa usio mkubwa utofautiana na dozi ya wasiwasi mkubwa.
Mgonjwa akiwa na wasiwasi mkubwa na kutotulia kwa kawaida huwa na maumivu kwa namna Moja au nyingine, kwa hiyo anaweza akapewa dawa hii kwa njia ya matako na pajani na pia dawa inawezekana kupitia kwenye mishipa ya damu na milligrams ubadilika kulingana na hali ya mgonjwa na badala ya masaa manane dozi yake huwa ndani ya masaa manane, kadri ya umri na uzito wa mgonjwa.
5. Pia na wale wenye kifafa dozi yao utofautiana na wale wenye wasiwasi pamoja na magonjwa ya akili kwa wenye kifafa dawa yao kwa mara nyingi upitia kwenye mishipa ya damu na kwa kawaida mgonjwa uanza kupewa dawa kuanzia milligrams kumi mpaka ishilini baada ya dakika telathini mpaka dakika sitini kwa kupitia kwenye mishipa ya damu, milligrams kwa kawaida zinaweza kuanzia mia mbili mpaka mia tatu kwa kulingana na uzito na umri wa mgonjwa.
6. Pia dawa hii kwa wagonjwa wa kifafa na degedege kwa watoto inawezekana kutolewa kwa njia ya mishipa ya damu ila inawezekana kupitia kwenye paja na kweye matako pia ila njia inayopendekezwa ni kwa njia ya mishipa ya damu kwa hiyo kama mgonjwa anapata shida kwenye mishipa ya damu njia ya matako au kwenye paja inawezekana kutumika kwa kadri ya maelekezo maalumu.
7. Dawa hii inawezekana kutumiwa na watu mbalimbali ila Kuna watu wanaopaswa kuitumia kwa taahadhari watu Hawa ni wale wenye matatizo katika upumuaji,walevi wa pombe, na pia epuka kutumia dawa hii mara kwa mara, pia wale wenye matatizo ya Figo na magonjwa ya ini wanapaswa kuitumia kwa taahadhari pia au kama Kuna dawa nyingine wasitumie kabisa.
8. Pia dawa hii Kuna wale ambao hawapaswi kuitumia kabisa,wale wenye aleji na dawa hii,wanaopumua vibaya au wenye athma kwa mda huo , wale walio na magonjwa sugu ya Figo,au ugonjwa wa ini umwkuwa kwenye hali ya usugu hawapaswi kuitumia kabisa.
9. Dawa hii pia Ina maudhi madogo madogo kama vile uchovu na kukosa nguvu,kusikia kama vile umevurugwa kwenye akili,hasa kwa wenye umri mkubwa, maumivu kwenye misuli, maumivu ya kichwa, maumivu kwenye tumbo, mkojo kushindwa kutoka kwa wakati hasa kupata mkojo kwa mda mrefu ukomu akunywa na kula Kawaida, magonjwa ya damu kama vile upungufu wa damu, kuwepo kwa njano,pia na matatizo kwenye ngozi kama vile upele na ngozi kuwasha,
10. Baada ya kuona Dalili kama hizi na mgonjwa anatumia dawa ya diazepam ni vizuri kufahamh kwamba hii ni kazi ya dawa,ila maudhi haya yakizidi ni vizuri kabisa kuwaona wataalamu wa afya kwa sababu Maudhi mengine ni hatari kwa afya hasa kupungukiwa damu na mengine,kwa hiyo dawa hii ni vizuri kabisa kutolewa hospital sio nyumbani.
11. Kwa hiyo dawa hii inapaswa kutolewa kulingana na wataalamu wa afya na pia ni vizuri kabisa kutolewa hospital kwa sababu ya maudhi madogo madogo na kwa sababu ya matokeo yake sio Vizuri kabisa dawa hii kutolewa kienyeji kienyeji na wagonjwa wa akili pamoja na degedege,kwa sababu Kuna watu ambao hawapaswi kutumia dawa hii unaweza kuwapatia kumbe hawapaswi kuitumia kabisa dawa hii na ukakuta unaleta madhara badala ya kutibu.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukuletea dawa ya kuzuia kuathirika kwa watu walio hatarini kupata VVU
Soma Zaidi...Usisumbuliwe tene na fangasi ukeni, zijuwe hapa dalili za fangasi ukeni, tiba yake na njia za kukabiliana na fangasi ukeni
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya isoniazid katika mapambano na kifua kikuu, tunafahamu kabisa kwamba kifua kikuu ni hatari katika jamii kwa hiyo dawa ya isoniazid ni mkombozi katika mapambano na kifua kikuu.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ambazo zinatumika kwenye matibabu ya kansa, dawa hizi usaidia kuharibu seli ambazo ambazo hazistahili kwa kitaalamu huitwa malignant seli.
Soma Zaidi...Digoxin ni nini? Digoxin inatokana na majani ya mmea wa digitalis. Digoxin husaidia kufanya mapigo ya moyo kuwa na nguvu na kwa mdundo wa kawaida zaidi. Digoxin hutumiwa kutibu kushindwa kwa moyo. Digoxin pia hutumiwa kutibu mpapatiko wa atiria, ugonjw
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya captopril katika matibabu ya magonjwa ya moyo, ni dawa ambayo imo kwenye kundi la vasodilators na ufanya Kazi mbalimbali zinazousu magonjwa ya moyo.
Soma Zaidi...Nitakujuza dalili za UTI na dawa za kutibu UTI. Pia tutaona njia za kujikinga na UTI pamoja na dalili za UTI
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa e quinine katika kutibu Malaria ni dawa inayotibu Ugonjwa wa Malaria ikiwa dawa nyingine zimeshindwa kufanya kazi.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya sulphonamide ni mojawapo ya dawa ambayo usaidia kutibu magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na bakteria ni dawa au antibiotics ya mda mrefu na pia matumizi yake sio makubwa sana kwa sababu ya kuwepo kwa antibiotics zenye ngu
Soma Zaidi...