Fahamu dawa ya kutuliza mishutuko.

Post hii inahusu zaidi dawa ya phenytoin,ni dawa inayotuliza mishutuko mbalimbali inayoweza kutokea kwenye mwili na kutokana na mishutuko hiyo tunaweza kupata kifafa.

Fahamu dawa ya phenytoin katika kutuliza mishutuko 

1. Dawa ya phynytoin ni mojawapo ya dawa ambayo inasaidia katika kutuliza mishutuko, kutokana na kushutuka kwa mgonjwa ndipo hapo tunaweza kupata kifafa,hii ni dawa ya tatu kwa kupendekezwa baada ya kutumia dawa ya phenobarbitone na diazepam inayofatia ni dawa hii ya phenytoin, kwa hiyo dawa hii usaidia katika mishutuko yote yaani mishutuko modogo, mikubwa na Ile ambayo imekuwa sugu.

 

2. Dawa hii ufanya Kazi kwenye mfumo wa fahamu, hasa kwenye kazi ya neuronsi katika kazi ya neuronsi kusafirisha ujumbe kutoka sehemu Moja kwenda nyingine kwa kufuata maelekezo ya ubongo, Kuna wakati ujumbe unasafiri kiholela bila kufuata maelekezo ya ubongo na kusababisha kuwepo kwa mishutuko, kusafirishwa kwa ujumbe kiholela ni kitu kisicho cha kawaida kwa hiyo hali hiyo isiyo ya kawaida ndio usababisha kuwepo kwa kifafa, degedege na mishutuko, kwa hiyo kazi ya phenytoin ni kuzuia ujumbe huo unaosafiri bila kufuata maelekezo ya ubongo kusimamisha na kusababisha mgonjwa kusinzia na kutulia hatimaye ubongo unajirudisha kwenye hali yake ya Kawaida na maisha yanaendelea.

 

3.Dawa hii kwq kawaida utolewa mara nyingi kweli mfumo wa vidonge, kwa hiyo uenda Moja kwa moja kwenye mfumo wa mmengenyo wa chakula na hatimaye kusafishwa kwenye mzunguko wa damu na kufika kwenye tatizo hatimaye kufanya kazi yake yake ya kuzuia mishutuko mbalimbali inayoweza kupelekea kuwepo kwa degedege au kifafa kwa watoto na watu wazima pia. 

 

4. Kwa kawaida dozi yake ubadilika kulingana na umri na uzito wa mgonjwa, kwa kawaida dozi uanzia kwenye milligrams mia tatu na pia inawezekana dozi ikaanzia mia mbili kadri ya hali ya mgonjwa,na mara nyingi mwisho huwa ni milligrams mia tano,pia  kwa upande wa masaa utegemea utaratibu wa wataalamu wa afya na hali ya mgonjwa kwa ujumla kama hali ni mbaya sana au ni ya Kawaida kwa hiyo watatumia utaratibu wa wataalamu wa Ili kikidhi mahitaji ya mgonjwa.

 

5. Pia kwa baadhi ya wagonjwa Kuna maudhi madogo madogo ambayo uleta shida kadri ya tafiti mbalimbali imeonekana asilimia hamsini ya wagonjwa huwa hawamalizi dawa kwa sababu ya kuwepo kwa maudhi madogo madogo kuwa makali na kupitia kiasi hali inayosababisha kuacha kutumia dawa hii na kuamia kwa nyingine kama diazepam na phenobarbitone ndio maana hii ni dawa ya tatu baada ya diazepam na phenobarbitone,kwa hiyo mgonjwa akishindwa kutumia dawa ya diazepam na phenobarbitone ndipo anaweza kutumia hii na penyewe chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya.

 

6. Maudhi hayo ni pamoja na kuishiwa damu wakati wa kutumia, kuwepo na kizunguzungu,presha kushuka, kupumua kwa shida baada ya kutumia dawa kubadilka kwa tabia inawezekana kuwa ya kutotulia yaani kutoka hapa kwenda pale na mambo kama hayo,kwa na mawazo yasiyo ya Kawaida kwa kitaamu huiitwa hallucinations, kwa watoto kuruka ruka au kutotulia na wazee wanaweza kupata pia  kwa hiyo hali kama hizi zikitokea kwa mgonjwa kwa kawaida kumaliza dozi inakuwa shida ndio maana watu wengi Hawamalizi dawa hizi kwa sababu ya kuwepo kwa maudhi madogo madogo ambayo yanaweza kuleta shida kwa wagonjwa.

 

7. Baada ya kuona maudhi madogo madogo kama haya na yanayoleta wasiwasi mkubwa kwa wagonjwa na ndugu pia ni vizuri kabisa kuwaona wataalamu wa afya na kubadilishiwaa dawa nyingine kama phenobarbitone au diazepam na pia kuhakikisha hali ambazo zimesababishwa na ugonjwa kuwa kwenye hali ya kawa kwa mfano upumuaji kuwa sawa, mapigo ya moyo kuwa kawaida na kuhakikisha damu inakuwa kwenye hali ya Kawaida, kwq hiyo kama hauna shida na dawa ya diazepam na phenobarbitone, mgonjwa asipendelee kutumia dawa hii mara kwa mara.

 

8. Pia dawa hii inaingiliana na dawa nyingine ambapo dawa hii umaliza dawa nyingine kazi, kwa mfano watumiaji wa uzazi wa mpango hasa kwa kutumia vidonge dawa hii umaliza nguvu kwa hiyo kwa upande wa akina Mama wanaweza kuwa wanatumia dawa hii mara kwa mara na wakabeba mimba kwa sababu dawa hii umaliza nguvu dawa za uzazi wa mpango, kwa hiyo akina Mama wanaotumia dawa za uzazi wa mpango wanapaswa kuwa makini katika matumizi ya dawa hii au kuomba ushauri wa wataalamu wa afya wakiwa wanatumia dawa hii.

 

9 . Dawa hii vile vile inaingiliana na dawa mbalimbali kama vile warfarin, carbamazepine, Theophylline, sulphonamide,na cimetidine, kwa hiyo dawa hii inaweza kumaliza nguvu dawa hii na watumiaji wakawa wanafanya kazi Bure katika kumeza dawa au dawa zikawa zinafanya kazi kidogo kwa sababu ya kuwepo kwa dawa ya phenytoin kwenye mwili.

 

10. Kwa hiyo dawa hii haiitumiki kiholela ni kutumia kwa utaratibu wa wataalamu wa afya kwa sababu matokeo yake mengine ni makali au wakati wa kutumia ni vizuri kabisa kuitumia dawa kwa utaratibu wa wataalamu wa afya na pia dawa hii inapaswa kutumiwa kwa uangalifu kwa sababu Kuna wengine wakiitumia wanaweza kupata matatizo wakiitumia wakiwa nyumbani , ni vizuri kabisa kuitumia wakiwa hospitalini.

 

ANGALIZO.

Kama Kuna mtu Hana shida na ya phenobarbitone na diazepam ni vizuri kabisa kutumia hizo kuliko kukimbilia dawa ya Phynytoin, kwa sababu ni dawa ya tatu kwa kupendekezwa baada ya diazepam na phenobarbitone.

 

 

 

 

 

 

 Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/12/29/Thursday - 05:36:24 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 772


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-