image

Fahamu dawa ya tetracycline katika kupambana na bakteria

Post hii inahusu zaidi dawa ya tetracycline katika kupambana na bakteria,ni mojawapo ya antibiotics au anti bacteria ambayo upambana na bakteria kama tutakavyoona hapo mbeleni.

Fahamu dawa ya Tetracycline katika kupambana na bakteria.

1 . Tetracycline ni mojawapo ya dawa ambazo usaidia katika matibabu ya kupambana na bakteria ni  muunganiko wa dawa tatu zikiwemo penicillin na streptomycin na zikiungana ndio zinaitwa tetracycline, muunganiko wa dawa hizi tatu huwa na sifa sawa na zinazofanana na mara nyingi utolewa kwa kumezwa mdomoni na pia uingia kwenye mmengenyo wa chakula na baadae kupitia kwenye mzunguko wa damu  hatimaye  kupambana na bakteria sehemu yoyote walipo.

 

2. Kwa upande mwingine aina ya dawa ya Tetracycline hydrochloride uweza kupitia kwenye mishipa ya damu na kufanya kazi kama zile ambazo hazijapitia kwenye mishipa ya damu, dawa hizi za tetracycline zikifika kwenye mwili na kukutana na bakteria zinazuia kutengenezwaa kwa protini ndani ya bakteria kitendo ambacho ufanya bakteria huyo kushindwa kuishi kwa sababu hawezi kuishi bila kuwepo kwa protein hiyo.

 

3. Kwa kawaida dawa hizi za tetracycline utibu magonjwa mbalimbali kama vile Chlamydia, kaswende na kisonono kwenye watu walio na aleji na penicillin kwa kawaida dawa ambayo imependekezwa kutibu kaswende na kisonono ni benzyl penicillin lakini Kuna watu wenye magonjwa haya kaswende na kisonono na Wana aleji na penicillin kwa hiyo dawa yao ni tetracycline ambayo na yenyewe utibu magonjwa hayo ya kaswende na kisonono,.

 

4. Dawa hii inaweza kutumiwa na watu mbalimbali ila haipaswi kutumiwa na wote wenye aleji na tetracycline , watoto chini ya miaka minane nao hawapaswi kutumia kwa sababu Ina tabia y kuharibu meno kwa sababu uingia hata kwenye fizi,wakiona mama wenye mimba changa hawapaswi kutumia dawa hii na kwa wale wanaonyonyesha hawaruhusiwi kutumia dawa hii mpaka waache kumnyonyesha hapo wanaweza kutumia dawa hii.

 

5. Pia Kuna wale wenye matatizo ya Figo, matatizo ya moyo na pia kwa wenye matatizo ya sukari yote ya kupanda na kushuka wanapaswa kutumia dawa hii ila wawe chini ya uangalizi ikiwa mtu Hana uangalizi asitumie dawa hii kwa sababu Ina tabia ya kuongeza tatizo au ikiwezekana watumie dawa za antibiotics nyingine tofauti na hizo.

 

6. Pia dawa hii uingiliana na dawa nyingine na kumaliza dawa nyingine  nguvu kwa mfano kwa wale wanaotumia uzazi wa mpango hasa ule wenye homoni au kichocheo cha estrogen, dawa hizi za tetracycline umaliza nguvu estrogen na mama anaweza kubeba mimba huku anatumia njia ya uzazi wa mpango kwa hiyo basi kwa watumiaji wa uzazi wa mpango ni vizuri kabisa kupata ushauri wa wataalamu wa afya kabla ya kutumia dawa hii Ili kuepukana na mimba zisizotarajiwa .

 

7. Pia kwa wale watumiaji wa madawa ya kupunguza asidi mwilini hasa we ye vidonda vya tumbo pia dawa hizi uingiliana sana na kalsium pamoja na magnesium na pia kwa watumiaji wa dawa za kuongeza madini ya chuma na wenyewe dawa hizi uingiliana na dawa za tetracycline kwa hiyo kabla ya kutumia dawa hii ya tetracycline ni vizuri kabisa kupata ushauri wa wataalamu wa afya Ili kuepuka madhara zaidi au kwa wakati mwingine unaweza kutumia dawa nyingine na unatumia tetracycline unakuwa unafanya kazi Bure.

 

8. Vile vile na dawa hizi za tetracycline huwa na maudhi madogo madogo kama vile kuongeza spidi ya majimaji yaliyo kwenye ubongo na kusababisha kizunguzungu na pengine kuona maruwe ruwe, kwa sababu dawa hii uweza kupitia kwenye mmengenyo wa chakula mgonjwa uweza kuhisi kichefuchefu na kutapika, maambukizi kwenye Koo na pia mgonjwa anaweza kuwa na miwasho pamoja na kujikuna pia kwa watumiaji wa mda mrefu wanaweza kuwa na matatizo katika kuona.

 

9. Haya ni baadhi ya maudhi madogo madogo ambayo yanaweza kutokea ikiwa maudhi haya yamepita kiasi ni vizuri kuwaona wataalamu wa afya Ili kuweza kutafuta tiba na kuepuka matatizo zaidi, pia dawa hizi zibatibu magonjwa mengi na kwa wakati mwingine zinapatikana kwenye maduka au famasi zetu ni vizuri, ila kwa sababu Zina maudhi mengi na zinaingiliana na dawa nyingi ambazo watu wanazozitumia mara kwa mara kwa mfano uzazi wa mpango na vidonda vya tumbo ni vizuri kabisa kuwaona wataalamu wa afya kabla ya kutumia dawa hii.

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2049


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kulia
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo chini upande wa kulia Soma Zaidi...

Maumivu ya uume baada ya tendo la ndoa
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maumivu ya uume baada ya tendo la ndoa Soma Zaidi...

Maumivu ya tumbo kabla ya kupata hedhi
Je unasumbuliwa na maumivu ya tumbo. Unadhani ni dalili za mimba na ukapima hakuna mimba. Soma Zaidi...

Dalili za mwanzo za ujauzito katika wiki ya kwanza
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mwanzo za ujauzito katika wiki ya kwanza Soma Zaidi...

Nini husababisha upungufu wa nguvu za kiume
Post hii itakujulidha mambo ambayo hupunguza nguvu za kiume Soma Zaidi...

Nikiwa katika siku zangu siumwi ila tatizo Ni kwamba najisikia kichefu chefu
Soma Zaidi...

mambo HATARI KWA UJAUZITO (MIMBA) mambo yanayopelekea kujauzito kuwa hatarini kutoka
Tofauti na mambo matano yaliyotajwa hapo juu kuwa yanapelekea ujauzito kutoka, kuna mambo mengine ambayo yanaweza kuuweka ujauzito kuwa hatarini. Soma Zaidi...

Madhara ya kiafya ya kupiga punyeto
Post hii inakwenda kukutania madhara ya kuoiga punyeto kwa afya yako. Soma Zaidi...

Dawa hatari kwa mwenye ujauzito
Hii ni orodha ya dawa ambazo hutumiwa sana na watu kutoka maduka ya dawa lakini sio salama kwa wajawazito. Soma Zaidi...

Nina vidonda kwenye uume wangu, je ni dalili ya nini?
Soma Zaidi...

Sababu za mama kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua.
Posti hii inahusu zaidi sababu za mama kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua, hili ni tatizo ambalo uwapata akina Mama wengi wanapomaliza kujifungua kwa hiyo tutaweza kuziona sababu zinazosababishwa na tatizo hili. Soma Zaidi...

Kazi na mdalasini katika kutibu matatizo ya homoni.
Posti hii inahusu zaidi kazi ya mdalasini katika matibabu ya homoni kwa wanawake. Soma Zaidi...