image

Fahamu dawa zinazotumika kwenye matibabu ya kansa

Post hii inahusu zaidi dawa ambazo zinatumika kwenye matibabu ya kansa, dawa hizi usaidia kuharibu seli ambazo ambazo hazistahili kwa kitaalamu huitwa malignant seli.

Dawa zinazotumika katika matibabu ya kansa.

 

1. Kwa kawaida tunavyofanyami jinsi kansa inavyotokea ni matokeo ya kuzalishwa kwa seli ambazo hazihiitajiki mwilini kwa kawaida, dawa hizi za kansa zimegawanyika katika makundi makuu matano ambayo kwa kitaalamu huitwa, Alkylating,ni kundi la kwanza, kundi la pili kwa kitaalamu huitwa Ant- metabolites, kundi la tatu kwa kitaalamu huitwa cytotoxic antibiotics, kundi la nne kwa kitaalamu huitwa vinca alkaloid na kundi la tano kwa kitaalamu huitwa hormones, makundi haya matano usaidiana katika matibabu ya kansa.

 

2. Kwa kawaida na ugonjwa huu wa kansa nao huwa kwenye makundi makuu manne, au kansa yenyewe utokea kwenye mfumo tofauti tofauti au upitie kwenye ngazi tofauti,kuna kansa ya mwanzoni au inayoanza kwa kitaalamu huitwa stage one, Kuna Kansa inayoendelea kutoka kwa ile inayoanza ambayo kwa kitaalamu huitwa stage two, na kuna kansa inayoendelea kutoka sehemu ya pili ambayo kwa kitaalamu huitwa stage three na kansa ngazi ya mwisho ambayo kwa kitaalamu huitwa stage four, kadri kansa inavyoongezeka na kutibiwa kunakuwa kugumu ,kwenye ngazi ya kwanza na ya pili kupona nakwo kunakuwa rahisi na mgonjwa upona kabisa.

 

 

3.Kwa hiyo ni vizuri kabisa kuwahi matibabu mapema ili kuweza kupona ugonjwa huu kwa sababu ni hatari, kwa hiyo tutaenda kufafanua kidogo kundi moja kwa lingine, kwa upande wa kundi la Alkylating ni kundi ambalo uua seli za kansa kwa kuvamia nuclear ya seli ambayo kwa kitaalamu huitwa DNA na kwa hiyo hakuna kuzaliwa kwa seli nyingine na mgonjwa kama yupo kwenye ngazi ya kwanza na ya pili anaweza kupona na kuendelea na maisha kama kawaida.kwa hiyo kuwahi matibabu ni jambo la msingi.

 

4. Kundi hili ni kundi la pili katika kupambana na kuanza kwa kitaalamu huitwa antimetabolite.

Ni miongoni mwao dawa ambazo usaidia katika matibabu ya kansa dawa hizi ufanya kazi kwa kuingilia nuclear ambayo kwa kitaalamu huitwa DNA na kuzuia kuzalishwa kwa wadudu ambao usababisha kuwepo kwa kansa na pia kuzuia kitendo cha kuzaliwa na kuongezeka kwa wadudu wanaosababisha kansa.kwa hiyo kwa kansa kwenye ngazi ya kwanza na ya pili ni rahisi kabisa kupona ila kwa ngazi ya tatu na nne kupona uchukua mda na hali yao kwa namna moja au nyingine uwa sio nzuri.kwa hiyo matibabu ya mapema ni muhimu.

 

5. Kundi lingine la dawa za kupambana na kansa kwa kitaalamu huitwa anti tumor antibiotics au kina jingine ni cytotoxic drug.

 

 Dawa hizi utengenezwa kutokana na vitu au material yaliyotokana na fungi kutoka kwenye udongo,dawa hizi ufanya kazi kwa kuzuia kazi ya nuclear ambayo kwa kitaalamu huitwa DNA isiendelee kuzaliana na pia kuingilia protein ya DNA kwa hiyo kuzaliana na kuongezeka kwa seli ambazo hazihiitajiki kuzuiliwa, kwa hiyo kwa matumizi mazuri ya dawa hizi usaidia kabisa kuangamiza kazi ya DNA ya kuendelea kuzaliana kutoka sehemu moja kwenda nyingine, na kama kuna seli ambazo hazihiitajiki zimeshaanza kuzaliwa kama mgonjwa ataendelea kutumia dawa hizi na seli ambazo hazihiitajiki zitatosha na kuwepo kwa seli za kawaida.

 

6. Dawa nyingine ya kupambana na kansa kwa kitaalamu huitwa vinca alkaloid au antimicrotubule agent.

 

 Microtubules ni sehemu mojawapo ya seli , kwa hiyo dawa hizi ya vinca alkaloid usaidia kuvamia microtubules za seli ambazo hazihiitajiki na pia kuhakikisha kwamba kazi yake yote imeharibika na kwa hiyo seli hizo haziwezi kuendelea na kazi ya kuzaliana kwa sababu ya kudhoofika kwa microtubules,kwa hiyo hata kama seli ambazo hazihiitajiki zimeshakuwa na microtubules wengi kwa matumizi ya dawa hizi za vinca alkaloid mgonjwa anaweza kupata nafuu na kuendelea kuishi hasa kwa wagonjwa walioko kwenye kansa ngazi ya kwanza na ya pili.

 

7. Kundi la mwisho la dawa za kupambana na kansa kwa kitaalamu huitwa hormones,

Kwa kawaida hizi ni homoni ambazo usaidia kupunguza kansa ambayo utegemea homoni, na homoni hiyo ambayo utumika ni steroids homoni,kwa hiyo homoni hiyo inayotumika usaidia kabisa kupunguza makali ya kansa hasa kansa za kwenye matiti na sehemu mbalimbali ambazo utegemea homoni,kwa hiyo ni vizuri kabisa kutumia dawa ya aina hizi kwa sababu kama kansa ipo kwenye hatua ya kwanza na ya pili kupona ni rahisi kwa kutumia homoni kuliko kama kansa iko kwenye stage ya tatu na ya nne.

 

 

 

8.  Pia dawa hizi nazo zina maudhui tofauti tofauti au zina matokeo mbalimbali kama vile kuwepo kwa kiasi kidogo cha seli mwilini kwa sababu katika matumizi ya dawa ili kuua seli ambazo zina maambukizi kuna baadhi ya seli ambazo hazina maambukizi nazo uharibiwa na dawa hali inayosababisha kupungua kwa seli mwilini na tunavyofahamu kabisa kama seli zikipungua na kinga ya mwili upungua pia.

 

9. Kuwepo kwa uchovu kwa sababu dawa ambazo mara nyingi zinatumika zinakuwa na nguvu zaidi, pia kuwepo kwa vidonda kwenye midomo hali huu utokea kwa sababu ya kupungua kwa kinga ya mwili, pia kwa sababu ya dawa mgonjwa anahisi kichefuchefu na kutapika pia, vile vile hamu ya kula kwa mgonjwa upungua kwa hiyo mgonjwa anapaswa kupewa vyakula anavyovipenda yeye na kuhakikisha kwamba anakula na kushiba kwa sababu dawa zinazotumika ni kali mno hata kama hana hamu ya kula anapaswa kulazimishwa.

 

10. Vile vile dawa hizi kwa kawa usababisha hali tofauti kwa mgonjwa Kuna Kipindi mgonjwa anaharisha na wakati mwingine anakuwa na choo kigumu, kwa hiyo uangalizi ni WA lazima kwa Kwa wagonjwa wa Kansa, na pengine mgonjwa uishiwa nywele kichwani hii ni kwa sababu ya dawa hasa wale wanaotumia mionzi katika matibabu,na kwa wakati mwingine mwili wa mgonjwa ubadilika wakati akiwa anatumia dawa, kuwepo kwa viupele kwenye mwili mzima hali hii usababishwa kwa sababu ya kinga ya mwili kupungua.

 

11. Pengine kwa watumiaji wa mda mrefu wa dawa za Kansa mgonjwa anaweza kushindwa kushika mimba na pia kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa,kwa sababu ya mabadiliko ya nevu,

 

12. Kwa hiyo dawa za Kansa Zina nguvu sana kwa watumiaji ni vizuri kabisa wakati wa kutumia wagonjwa wanapaswa kuwa na chakula cha kutosha na pia kuwepo na hali ya kuwatoa moyo na kuwafariji kwa sababu ni ugonjwa unaotisha, ila watu wanapaswa kuwahi matibabu endapo wameona dalili ambazo hazieleweki kwa sababu Kansa ikitibiwa mapema ni rahisi kupona hasa kwenye ngazi ya kwanza na ya pili ila matibabu yakicheleweshwa na kupona ni kwa shida .

 

13. Pia dawa hizi hazipaswi kutumiwa kiholela zinapaswa kutumika kadri ya wataalamu wa afya na pia kwenye matibabu wagonjwa wa Kansa wanapaswa kuangaliwa kwa sababu dawa hizi zina nguvu, pia wakati wa kutumia dawa mgonjwa anapaswa kula vyakula mbalimbali na vyenye kujenga mwili Ili kurudisha mwili kwenye hali ya Kawaida,hasa hasa mboga za majani na matunda ni lazima kwa watumiaji wa dawa za Kansa.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Dawa Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 740


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Dawa ya kutibu fangasi wa kwenye mdomo na kinywa
Zipo dawa nyingi ambazo hufahamika katika kutibu fangasi kwenye mdomo ama kinywa. Miongoni mwa dawa hizo hapa nitakuletea baadhi yao. kama wewe pia unasumbuliwa na fangasi wa mdomo basi post hii itakusaidi sana. Soma Zaidi...

Matibabu ya Fangasi ukeni na dawa za fangasi wanaoshambulia uke.
Fangasi wanaweza kushambulia uke, kwa juu kwenye mashhav ya uke ama kwa ndani. Hali hii inaweza kusababisha miwasho na maumivu pia. Inaweza kusababisha michubuko na kutofurahia tendo la ndoa. Makala hii inakwenda kukujuza dawa na matibabu ya fangasi ukeni Soma Zaidi...

Miungurumo haiishi tumboni nikishika upande wa kushoto wa tumbo kuna maumivu kwa mbali je mm nitumie dawa gan kuondoa tatizo hilo
Kukawa na gesi tumboni kunaweza kuwa ni dalili ya shida kwenye afya, hasa katika mfumo wa chakula. Hali itakuwa sio nzuri endapo utakosea hamu ya kula na kuhisivkushiba muda wowote. Soma Zaidi...

Dawa za Anesthesia katika kutuliza maumivu.
Unapotaka kufanyiwa baadhi ya matibabu unatakiwa kupewa ganzi ama nusu kaput ili kulifanyia usihisi maumivu. Dawa hizi zinajulikana na Anesthesia. Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu dawa ya ketoconazole.
Post hii inahusu zaidi dawa aina ya ketoconazole ni dawa inayotumika kutibu fangasi za kwenye koo. Soma Zaidi...

Dawa ya UTI
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa ya UTI Soma Zaidi...

Njia zinazotumika Ili kumpatia mgonjwa dawa
Posti hii inahusu zaidi njia kuu nne ambazo utumika kumpatia mgonjwa dawa, Ili kumpatia mgonjwa dawa Kuna njia za kutumia kama ifuayavyo. Soma Zaidi...

Fahamu dawa ya diazepam katika kutuliza kifafa
Post hii inahusu zaidi dawa ya diazepam katika kutuliza kifafa, ni dawa ambayo matumizi yake yanaweza kuingilia pote kwenye kutuliza kifafa na pia kwa wagonjwa wa akili. Soma Zaidi...

Fahamu dawa za kutibu mafua
Post hii inahusu dawa za kutibu mafua ambazo ni cough seppessants na nasal congestion ni dawa ambazo zimependekezwa kwa ajili ya kutibu mafua. Soma Zaidi...

Dawa ya Albendazole katika kutibu Minyoo.
Posti hii inahusu zaidi dawa ya Albendazole katika kutibu Minyoo, ni Aina mojawapo ya dawa ambayo usaidia kutibu Minyoo inayosababishwa na bakteria mbalimbali. Soma Zaidi...

Fahamu Dawa inayotibu minyoo iitwayo albenza (albendazole)
Albenza (albendazole) hutumika kutibu magonjwa ya minyoo ya ndani ikiwa ni pamoja na maambukizi ya minyoo ya tegu. Albenza inafanya kazi kukomesha kuenea kwa maambukizo ya minyoo kwenye chanzo, na kukata chanzo chao cha nishati, na hivyo kuzuia kuenea k Soma Zaidi...

Ijue dawa ya paracetamol katika kutibu maumivu
Post hii inahusu zaidi dawa ya paracetamol katika kutibu maumivu, ni dawa inayosaidia kutibu maumivu ya Kawaida kama vile aspirin. Soma Zaidi...