Post hii inahusu zaidi dawa ya ampicillin, ni mojawapo ya dawa za kutibu maambukizi ya bakteria kwenye mwili wa binadamu ba pia ni dawa ambayo IPO kwenye kundi la penicillin kundi hili kwa kitaa huitwa broad spectrum penicillin
1. Kwanza kabisa tunapaswa kufahamu kwamba hii ni dawa ambayo usaidia kutibu maambukizi ya bakteria na pia ni dawa ambayo imo kwenye makundi ya penicillin kama tulivyoona hapo kwenye utangulizi na pia dawa hii inaweza kusaidia pia kupambana na bakteria ambao utoa asidi Ili kuweza kuzuia kazi ya dawa, kama dawa husika haipo ampicillin inaweza kutumika.
2. Kwa kawaida ampicillin usaidia katika matibabu ya maambukizi ya bakteria kwenye Koo,sikio,mkojo na pia usaidia katika matibabu ya nimonia, dawa hii huwa na container lake kila container Ina milligrams mia mbili hamsini na na nyingine huwa na miigram mia tano na pia milligrams utolewa kulingana na wataalamu wa afya na pia dawa hii utolewa kila baada ya masaa sita , kabla ya kutumia dawa hii ni vizuri kutumiwa dakika thelathini kabla ya kula chakula.
3. Dawa pia IPO kwenye mfumo wa unga au poda na huwa na maji maalumu yametengwa kwa ajili ya kuchanganya poda hiyo na maji, maji hayo kwa kitaamu huiitwa water for injection, kwa hiyo dawa hiyo uchanganywa na maji na utikiswa na kuhakikisha kwamba poda haionekani tena na pia mgonjwa uweza kupewa dawa hiyo, kwa upande wa dozi utegemea umri na uzito wa mgonjwa. Pia dawa hiyo inawezekana kutolewa kwenye paja au Tako na pia kwenye mishipa ya damu.
Tunapaswa kufahamu kwamba mchanganyiko wa dawa inayopitia kwenye damu na kwenye paja au Tako ni tofauti kwa sababu ya kwenye mishipa inaenda Moja kwa moja kwenye damu kwa hiyo tunaongeza maji zaidi ya Ile inayopitia kwenye nyama ( Tako na paja).
4. Kwa wakati mwingine kuna syrup hizi ni kwa upande hasa wa watoto, mchanganyiko ni kutumia milligrams mia ishilini na tano kwenye mills tano na pia mtoto anapewa, mara nyingi hizi dawa zinakuja zimechanganywa Moja kwa moja na chupa Huwa na maagizo namna ya kutumia, kwa hiyo wazazi wa mtoto uweza kupewa maagizo na jinsi ya kumpatia mtoto dawa hiyo.
5. Dawa hii ya ampicillin na yenyewe Ina tabia kama dawa zote au makundi ya penicillin kwa hiyo kila mtu anaweza kutumia dawa hii ila kwa wale ambao Wana aleji na ampicillin hawapaswi kutumia dawa hii na pia wale wenye aleji ya penicillin hawapaswi kutumia kwa sababu dawa hii imo miongoni mwa makundi ya penicillin na pia kwa wale wenye tatizo la upungufu wa damu wanapaswa kuitumia kwa taahadhari au waitumie kwenye uangalizi maalumu Ili wasije kuleta tatizo kubwa zaidi kwa sababu dawa hii Ina tabia ya kupunguza damu hasa kwa watumiaji wa mara kwa mara.
6. Vile vile dawa hii Ina maudhi madogo madogo ambayo yanaweza kujitokeza wakati wa kuitumia maudhi hayo ni pamoja na maumivu kwenye joint, kichefuchefu na kutapika, maumivu ya tumbo , kizunguzungu na upungu wa damu au kama Kuna mtu ana kidonda au sehemu inayotoa damu anaweza kuendelea kutoa damu kwa mda mrefu wakati akiwa anatumia dawa hii. Kwa hiyo haya maudhi madogo madogo yakitokea ni kawaida wakati wa kutumia dawa hii ila yakiongezeka na kuleta madhara zaidi ni vizuri kuwaona wataalamu wa afya na kubadilishiwaa dawa.
7. Pia ni vizuri kutumia dawa hii kwa ushauri wa wataalamu wa afya sio kutumia dawa hii kiholela kwa sababu matokeo yake yanaweza kuwa mabaya hasa kwa watu wenye damu kidogo wakitumia dawa hii wakiwa nyumbani wanaweza kuleta tatizo juu ya tatizo na pia kwa wale wenye sickle cell yaani wenye matatizo ya kuishiwa damu wanapaswa kuitumia dawa hii wakiwa kwenye uangalizi maalumu au wapime wingi wa damu kabla ya kutumia ai tatizo kama litakuwa kubwa zaidi na kuleta madhara ni Bora wabadilidhiwe na kupewa dawa ambazo hazitaleta madhara kwao.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 3331
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani
👉2 Kitau cha Fiqh
👉3 kitabu cha Simulizi
👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉5 Kitabu cha Afya
Fahamu kuhusu dawa ya propranolol ambayo hutibu magonjwa ya moyo
Post hii inahusu zaidi dawa ya propranolol katika matibabu ya magonjwa ya moyo, dawa hii ipo kwenye kundi la beta blockers na ufanya Kazi mbalimbali hasa kwa wagonjwa wa moyo. Soma Zaidi...
Dawa ya minyoo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za minyoo Soma Zaidi...
Fahamu dawa za 5-fluorouracil,Tegafur na uracili
Post hii inahusu zaidi dawa za 5-fluorouracil, Tegafur na uracili katika kupambana na kansa. Soma Zaidi...
Faida za vidonge vya zamiconal
Posti hii inahusu zaidi faida za vidonge vya zamiconal, ni baadhi ya faida ambazo upatikana kutokana na vidonge vya zamiconal,ni vidonge ambavyo utibu au kusaidia kwenye matatizo ya viungo vya uzazi. Soma Zaidi...
Matumizi ya dawa ya vidonda vya tumbo
Posti hii inahusu zaidi matumizi ya dawa za vidonda vya tumbo, ili kuweza kutumia dawa hizi ni vizuri kabisa kufuata mashariti kama ifuatavyo. Soma Zaidi...
Miungurumo haiishi tumboni nikishika upande wa kushoto wa tumbo kuna maumivu kwa mbali je mm nitumie dawa gan kuondoa tatizo hilo
Kukawa na gesi tumboni kunaweza kuwa ni dalili ya shida kwenye afya, hasa katika mfumo wa chakula. Hali itakuwa sio nzuri endapo utakosea hamu ya kula na kuhisivkushiba muda wowote. Soma Zaidi...
Fahamu dawa zinazopunguza maumivu
Post hii inahusu zaidi dawa zinazofanya kazi ya kupunguza maumivu kwa kawaida dawa hizi ufanya kazi kwa kupitia kwenye mfumo wa fahamu. Soma Zaidi...
Fahamu dawa za kisukari
Post hii inahusu zaidi dawa za kisukari, kwa sababu ya kuwepo kwa ugonjwa wa kisukari vilevile kuna dawa zake ambazo utumika kurekebisha sukari kama imepanda au kushuka. Soma Zaidi...
Fahamu antibiotics ya asili.
Post hii inahusu zaidi antibiotics ya asili, ni antibiotics inayotumia vitu vya kila siku na ya kawaida na mtu akaweza kupona kabisa na kufanya kazi kama antibiotics ya vidonge vya kawaida. Soma Zaidi...
Dawa za kutibu kiungulia
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za kutibu kiungulia Soma Zaidi...
Dawa ya kutibu mapunye
DAWA YA MAPUNYEMatibabu ya mapunye inategemea ni wapi mapunjye yapo. Soma Zaidi...
Nani anapaswa kutumia vidonge vya zamiconal.
Posti hii inahusu zaidi watu ambao wana uwezo wa kutumia vidonge vya zamiconal, ni baadhi ya watu au makundi yanayoweza kutumia vidonge hivi. Soma Zaidi...