image

Fahamu kuhusu dawa ya Albendazole

Post hii inahusu zaidi dawa ya Albendazole ni mojawapo ya dawa ambazo usaidia kutibu minyoo, na pia imefanikiwa sana kadri ya watumiaji wa dawa hiyo.

Fahamu kuhusu dawa ya Albendazole .

1. Dawa ya Albendazole ni mojawapo ya dawa ambayo imechaguliwa kutibu minyoo aina ya ascrarisisi, hookworm, maambukizi yatokanayo na minyoo,strongyloidiasis,trichuria,anterobiasisi na trichostrongyloidiasi hayo ni majina ya kitaalamu yanayotumika kuitwa na minyoo ambayo utibiwa na dawa ya Albendazole,

 

2. Kwa kawaida dawa hizi uwekwa kwenye tumbo lililowazi  ili kama wadudu wapo waweze kuuawa vizuri bila kujificha kwenye chakula na pia ushauliwa kutumiwa wakati wa asubuhi kabla mtu hajala chakula chochote na kwa kawaida dawa hizo utafunwa na pia kumezwa bila maji na baadae mtu anaweza kula chakula.

 

3. Pia  dawa hii huwa na maudhui madogo madogo ambayo ujitokeza baada ya kutumia dawa na maudhui hayo yakizidi ni vizuri kumwona daktari au mtaalamu wa mambo ya afya, na maudhui hayo ni kama kiungulia,kuharisha, maumivu ya kichwa, kichefuchefu na kutapika, kizunguzungu kwa hiyo kwa watumiaji wa dawa za Albendazole baada ya kuona dalili kama hizo ni matokeo ya dawa.

 

4. Kwa kawaida dawa hizi hazitumiki kwa watu wote, wengine wanaweza kutumia ila akina Mama wenye mimba changa na wajawazito hawapaswi kutumia na watoto chini ya miaka miwili hawapaswi kutumia dawa hii kwa sababu ya matokeo yake kwao kama mimba kutoka kwa wanawake wenye mimba changa na watoto wadogo wako kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa degedege.

 

5. Kwa hiyo katika kutumia dawa hiii ni vizuri kabisa kufuata utaratibu wa wataalamu wa afya sio kutumia kiholela kwa sababu madhara yake yanaweza kuwa makubwa zaidi ikiwa dawa hii inatumika visivyo kwa hiyo ni lazima kuwaona wataalamu wa afya kabla ya kutumia dawa hizi.           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/12/15/Thursday - 10:50:58 pm Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2215


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Fahamu Dawa inayotumika kupunguza maumivu (ibuprofen)
Ibuprofen ni mojawapo ya dawa zinazotumiwa sana duniani kote! Ili kupunguza maumivu na kuvimba, agiza Ibuprofen leo na upate afya bora! Ni kiungo amilifu katika dawa za jina kama vile Motrin na zaidi. Ibuprofen pia inaweza kuuzwa kama: Advil Motrin, Soma Zaidi...

Fahamu dawa ya kutuliza mishutuko.
Post hii inahusu zaidi dawa ya phenytoin,ni dawa inayotuliza mishutuko mbalimbali inayoweza kutokea kwenye mwili na kutokana na mishutuko hiyo tunaweza kupata kifafa. Soma Zaidi...

Dawa za maumivu ya jino
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za maumivu ya jino Soma Zaidi...

Dawa ya chango na maumivu ya hedhi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa ya chango na dawa ya maumivu ya hedhi Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu dawa ya fluoroquinolones/quinolones
Post hii inahusu dawa ya kupambana na bakteria, hili kundi la fluoroquinolones lina dawa kuu mbili ambazo ni ciprofloxin na ofloxacin. Soma Zaidi...

Madhara ya Tiba mionzi
Post hii inahusu zaidi madhara ya Tiba mionzi kwa wagonjwa wa saratani, ni madhara yanayotokea kwa wagonjwa wanaotumia mionzi katika matibabu ya saratani. Soma Zaidi...

Fahamu dawa ya carvedilo katika matibabu ya magonjwa ya moyo
Post hii inahusu zaidi dawa ya carvedilo katika matibabu ya magonjwa, ni mojawapo ya dawa kwenye kundi la beta blockers na pia uhusika katika matibabu ya magonjwa ya moyo kama nyingine. Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu dawa za kifua kikuu
Post hii inahusu dawa za kifua kikuu ni dawa ambazo utumika kutibu kifua kikuu, kwanza kabisa kabla ya kuanza kufahamu dawa hizo ni vizuri kabisa kufahamu kifua kikuu nini hili kuweza pia kufahamu dawa zake. Soma Zaidi...

Ifahamu dawa ya kutibu kifua kikuu
Post hii inahusu zaidi dawa ya Rifampin kama dawa mojawapo ya kutibu kifua kikuu. Soma Zaidi...

Dawa ya kutibu macho
Hizi ndio dawa za macho yenye ukavu, kuwasha ama kutoa machozi Soma Zaidi...

Fahamu dawa ya sulfonamide dawa inayopambana na maambukizi ya bakteria mwilini.
Post hii inahusu zaidi dawa ya sulphonamide ni mojawapo ya dawa ambayo usaidia kutibu magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na bakteria ni dawa au antibiotics ya mda mrefu na pia matumizi yake sio makubwa sana kwa sababu ya kuwepo kwa antibiotics zenye ngu Soma Zaidi...

Fahamu kazi ya dawa ya ampicillin inayopambana na maambukizi ya bakteria
Post hii inahusu zaidi dawa ya ampicillin, ni mojawapo ya dawa za kutibu maambukizi ya bakteria kwenye mwili wa binadamu ba pia ni dawa ambayo IPO kwenye kundi la penicillin kundi hili kwa kitaa huitwa broad spectrum penicillin Soma Zaidi...