image

Fahamu kuhusu dawa ya ALU au kwa lugha nyingine ni dawa ya mseto

Post hii inahusu zaidi dawa ya ALU ila kwa jina jingine huitwa dawa ya mseto,ni aina ya dawa inayotumika kutibu ugonjwa wa malaria ya kawaida.

Fahamu kuhusu dawa ya mseto au ALU.

1. Dawa hii ya ALU ni dawa ambayo utumika kutibu malaria ya kawaida, dawa hii ni muunganiko wa dawa mbili ambazo kwa kirefu zinaitwa Artemether lumefantrine, Artemether usimama kama A, na lumefantrine usimama kama LU kwa hiyo kwa ujumla utengeneza jina la ALU ambapo Artemether ina miligramu ishirini na lumefantrine ina miligramu mia ishirini kwa ujumla dawa hii huwa na jumla ya milligrams mia arobaini.

 

2. Kama tulivyotangulia kusema kwamba dawa hii utumika kutibu malaria ya kawaida, tunasema utibu malaria ya kawaida kwa sababu ya dalili zake kuwa za kawaida, dalili za malaria ya kawaida ni kama ifuatavyo maumivu kwenye jointi, maumivu ya kichwa, mwili kukosa nguvu, kichefuchefu na kutapika, maumivu ya tumbo la kawaida, kuhisi baridi au kwa watu wengine kutetemeka , dalili hizi hazimfanyi mtu kushindwa kutembea na kufika hospitali na akipata vipimo na kukutwa na malaria ya kawaida anapatiwa vidonge vya ALU au mseto na anapona kabisa na kurudia hali yake ya kawaida.

 

3. Matumizi ya dawa hii utegemeza umri wa mtu na kilo za mtu, watu wenye kilo kuanzia tano mpaka kumi na tano utumia kidonge kimoja, kidonge cha kwanza ukitumia siku ya kwanza , kidogo cha pili baada ya masaa manane na vidonge vifuatavyo utumika asubuhi na jioni kwa kawaida dozi hiyo utumia siku tatu kama mtu anatumia vidonge kwa mda na kwa wakati.

 

4. Watu wenye kilo kuanzia kumi na tano mpaka ishirini na tano utumia vidonge viwili, yaani siku ya kuanza anameza vidonda viwili, baada ya masaa nane anameza vidonge vingine viwili na siku zifuatazo anameza vidonge viwili asubuhi na jioni mpaka siku tatu zinaisha. Yaani asubuhi viwili na jioni viwili.

 

5. Watu kuanzia kilo ishirini na tano mpaka thelathini na tano kwa kawaida umeza vidonge vitatu, yaani siku ya kwanza anameza vidonge vitatu, baada ya masaa manane vidonge vitatu, na anaanza kumeza asubuhi na jioni yaani asubuhi vidonge vitatu na jioni vidonge vitatu mpaka dozi inaisha.

 

6. Watu wenye kilo kuanzia thelathini na tano na kuendelea kwa kawaida umeza vidonge vinne, yaani siku ya kuanza kutumia dawa anameza vidonge vinne na baada ya masaa manane anameza vidonge vingine vinne na akimaliza hapo anameza vidonge asubuhi na jioni yaani asubuhi vinne na jioni vinne mpaka dozi inaisha , kwa kawa wakati wa kutumia dawa hizi ni vizuri kutumia maji mengi ya kunywa pamoja na kula kushiba kwa sababu kama mtu hajashiba dawa hizi hazifanyi kazi vizuri na uweza kumsumbua mtumiaji kwa hiyo ni vizuri kula na kushiba wakati wa kutumia dawa hizi.

 

7. Pia dawa hizi uweza juwa na maudhi madogo madogo kama vile kizunguzungu, kutapika, kuishiwa nguvu na pia kupenda kulala mda mwingi, hasa hasa maudhi haya uwapata watu wale ambao hawako na kushiba kabla ya kutumia dawa ni vizuri kabisa kula na kushiba ndipo utumia dawa, pia wakati wa kutumia dawa hizi ni vizuri na ni lazima kutumia dawa za kupunguza maumivu hasa hasa panadol na dawa nyingine ambazo ufanya kazi kama paracetamol.

 

8. Dawa hizi ya ALU haipaswi kutumiwa na akina mama wenye mimba na pia wale wenye mzio au aleji na dawa hizi , na pia ikiwa mtu anatumia dawa hizi na akatapika baada ya nusu saa kutumia anapaswa kurudia tena kwa sababu dawa haijafanya kazi.

 

9. Katika matumizi ya dawa hii ni vizuri kabisa kufuata taratibu za wataalamu wa afya ili kupata maelekezo sio kutumia kiholela kwa sababu unaweza kupata matatizo kutokana na matumizi yasiyo sahihi ya dawa hizi ya ALU.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 3478


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Fahamu kuhusu dawa ya ALU au kwa lugha nyingine ni dawa ya mseto
Post hii inahusu zaidi dawa ya ALU ila kwa jina jingine huitwa dawa ya mseto,ni aina ya dawa inayotumika kutibu ugonjwa wa malaria ya kawaida. Soma Zaidi...

Dawa ya kutibu minyoo
Zijuwe aina za minyoo na tiba yake. Dawa 5 za kutibu minyoo ya aina zote Soma Zaidi...

Fahamu dawa za 5-fluorouracil,Tegafur na uracili
Post hii inahusu zaidi dawa za 5-fluorouracil, Tegafur na uracili katika kupambana na kansa. Soma Zaidi...

Dawa ya fangasi ukeni
Makala hii itakueleza dawa ya kutibu fangasi wa ukeni Soma Zaidi...

Njia zinazotumika Ili kumpatia mgonjwa dawa
Posti hii inahusu zaidi njia kuu nne ambazo utumika kumpatia mgonjwa dawa, Ili kumpatia mgonjwa dawa Kuna njia za kutumia kama ifuayavyo. Soma Zaidi...

Ifahamu dawa ya isoniazid katika kupambana na ugonjwa wa TB
Post hii inahusu zaidi dawa ya isoniazid katika mapambano na kifua kikuu, tunafahamu kabisa kwamba kifua kikuu ni hatari katika jamii kwa hiyo dawa ya isoniazid ni mkombozi katika mapambano na kifua kikuu. Soma Zaidi...

Fahamu kundi la veta blockers katika matibabu ya magonjwa ya moyo.
Post hii inahusu zaidi kundi la beta blockers katika matibabu ya magonjwa ya moyo,hili kundi lina dawa mbalimbali ambazo utumika katika matibabu ya magonjwa ya moyo na kila dawa tutaiongelea tofauti tofauti ili kuweza kujua kazi zake. Soma Zaidi...

Fahamu matumizi ya Ampicillin.
Ampicillin ni antibiotic yenye msingi wa penicillin ambayo inafanya kazi kupambana na maambukizi ya ndani ya bakteria. Ampicillin hufanya kazi ya kuharibu kuta za kinga ambazo bakteria huunda ndani ya mwili wako na kuzuia bakteria wapya kutokeza. Ampici Soma Zaidi...

Matumizi ya dawa ya vidonda vya tumbo
Posti hii inahusu zaidi matumizi ya dawa za vidonda vya tumbo, ili kuweza kutumia dawa hizi ni vizuri kabisa kufuata mashariti kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

Ni dawa gani hatari kwa mjamzito?
Ukiwa mjamzito uwe makini sana katika kuchagua matumizi ya dawa. Vinginevyobinawwza kuwa hatari. Hapa nitakujuza dawa ambazo ni hatari kutumia kwa ujauzito wako. Soma Zaidi...

Dawa ya quinenes katika kutibu Malaria
Post hii inahusu zaidi dawa e quinine katika kutibu Malaria ni dawa inayotibu Ugonjwa wa Malaria ikiwa dawa nyingine zimeshindwa kufanya kazi. Soma Zaidi...

Ifahamu dawa ya kupunguza maumivu
Post hii inahusu dawa ya aspirin katika kupunguza maumivu,ni dawa ambayo upunguz maumivu ya Kawaida, kushusha homa na pia usaidia kwenye magonjwa ya moyo hasa kuzuia stroke kama imetokea mda ndani ya masaa ishilini na manne Soma Zaidi...