Fahamu kuhusu dawa ya fluconazole.

Post hii inahusu zaidi dawa ya fluconazole ni dawa ya kutibu fangasi za aina au za sehemu mbalimbali,

Fahamu kuhusu dawa ya Fluconazole .

1. Dawa ya fluconazole ni aina ya dawa inayotumika kutibu fangasi za aina mbalimbali kama vile fangasi za kwenye koo, fangasi za kwenye oesophageal na fangasi za kwenye sehemu za siri,hii ni dawa ya kwanza iliyopendekezwa kwa kutibu fangasi mbalimbali kwenye watu mbalimbali.

 

2. Katika matumizi ya dawa hizi pia kuna maudhi maudhi madogo yanaweza kutokea ambayo ni pamoja na kutapika, kuharisha, na upele upele kwenye ngozi,na dalili hizi zikionekana ni kwenda kwa daktari mara moja au kwenda kwa wataalamu wa afya.

 

3. Dawa hii inatumika ila kuna watu ambao hawapaswi kutumia kwa mfano wale wenye aleji na pia dawa hizi uingiliana na matengenezo ya adrenal gland ambayo usaidia katia kutengeneza gonadal steroids na pia usababisha kubadilika kwa hedhi na pia matumizi ya mara kwa mara usababisha ugumba.

 

4. Kwa watumiaji wa dawa hizi wakipata tatizo la kubadilika kwa hedhi wasishangae kwa sababu hizi dawa uingilia na system za hedhi kwa ujumla.na pia matumizi ya mara kwa mara ya dawa hii sio nzuri ukitumia mara ya kwanza na nafuu haipatikani ni lazima kupata ushauri wa wataalamu wa afya ili kuweza kuepukana na matatizo makubwa kama vile ugumba na mambo kama hayo.

 

5. Katika matumizi ya dawa hii ni vizuri kabisa kula vizuri ukashiba na kutumia maji mengi ya kutosha kwa sababu maji mengi usaidia kupunguza sumu mwilini kwa hiyo tusipende kutumia dawa hii kiholela kwa sababu matatizo yake ni makubwa ikiwa matumizi hayaeleweki kwa sababu ni  vizuri kuwaona wataalamu wa afya kabla ya kutumia dawa hii.

 Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/12/15/Thursday - 12:46:03 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1414

Post zifazofanana:-