image

Fahamu kuhusu dawa ya fluoroquinolones/quinolones

Post hii inahusu dawa ya kupambana na bakteria, hili kundi la fluoroquinolones lina dawa kuu mbili ambazo ni ciprofloxin na ofloxacin.

Fahamu kuhusu dawa ya fluoroquinolones .

1. Hii ni mojawapo ya dawa za kupambana dhidi ya maambukizi ya bakteria dawa hii kama tulivyoona hapo mwanzoni Ina dawa muhimu mbili ambazo ni ciprofloxin na ofloxacin na kundi hili pamoja na kutibu magonjwa mengine ni maarufu katika matibabu ya maambukizi kwenye mfumo wa hewa, maambukizi kwenye ngozi ambayo uambatana na viupele pamoja na miwasho, maambukizi ya kaswende na kisonono au kwa lugha ya kitaamu huiitwa sexual transmission diseases and sexual transmission infection.

 

2. Dawa hizi ufanya kazi mwili kwa kuharibu kabisa kazi ya bakteria kwa kuingilia DNA ya bakteria na kuzuia bakteria kuendelea kuzaliana hatimaye kufa, dawa hizi kwa kawaida utumiwa kwenye mdomo kama vidonge na pia uweza kuingia kwenye mmengenyo wa chakula na kuelekea kwenye mzunguko wa damu ambapo usambaza sehemu mbalimbali kama vile kwenye sehemu zozote za mwili zenye maambukizi na kuharibu kabisa kazi ya bakteria kwa kuingilia DNA ya bakteria.

 

3. Pamoja na magonjwa ambayo utibiwa na dawa hizi Kuna magonjwa mengine kama hays kuharisha na kutapika, maambukizi kwenye kibofu cha mkojo, kwenye joint na kweye magoti, kwenye tumbo na pia maambukizi kwenye via nya uzazi kama Kuna bakteria ameshambulia huko.

 

4. Ambao hawapaswi kutumia dawa hii ni wale wenye aleji na dawa hii pamoja na watoto chini ya miaka kumi na minane pamoja na wanawake wenye mimba.pia utumika kwa uangalizi kwa wenye magonjwa ya Figo na inii.

 

5. Maudhi madogo madogo ya dawa hii ni pamoja na kizunguzungu, maumivu ya kichwa, maumivu ya tumbo, kichefuchefu na kutapika, kuharibu na pengine kupandisha sukari.

 

6. Kwa hiyo dawa hii haiitumiki kiholela mpaka kuwepo kwa maagizo ya wataalamu wa afya kwa sababu dawa hii Ina maudhi madogo madogo ambayo yanaweza kuleta shida ikiwa mgonjwa yupo nyumbani ila kama yupo hospital ni rahisi kumpatia huduma ya kwanza.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 860


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Dawa ya kutibu minyoo
Zijuwe aina za minyoo na tiba yake. Dawa 5 za kutibu minyoo ya aina zote Soma Zaidi...

Fahamu dawa ya kutibu kikohozi inayoitwa expectorant
Post hii inahusu zaidi dawa aina ya expectorant katika matibabu ya kikohozi,ni dawa ambayo usaidia au uzuia kikohozi kuendelea kutokea. Soma Zaidi...

Dawa ya maumivu ya jino
Somo Hili linakwenda kukuletea dawa ya maumivu ya jino Soma Zaidi...

Dawa ya kutibu UTI
Nitakujuza dalili za UTI na dawa za kutibu UTI. Pia tutaona njia za kujikinga na UTI pamoja na dalili za UTI Soma Zaidi...

Dawa za kutibu kiungulia
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za kutibu kiungulia Soma Zaidi...

Dawa za maumivu ya jino
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za maumivu ya jino Soma Zaidi...

Ijue dawa ya sulphadoxine na pyrimethamine (sp)
Post hii inahusu zaidi dawa ya Sp , kirefu cha dawa hii ni sulphadoxine na pyrimethamine hii dawa ilitumika kutibu malaria kwa kipindi fulani lakini sasa hivi imebaki kutumiwa na wajawazito kama kinga ya kuwazuia kupata malaria. Soma Zaidi...

Kazi ya Dawa ya salbutamol
Posti hii inahusu dawa ya salbutamol na kazi yake ya kutibu ugonjwa wa Asthma, ni dawa mojawapo ambayo imetumia na watu wengi na wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa, kwa hiyo zifuatazo ni kazi ya Dawa hii ya salbutamol katika kutibu Asthma. Soma Zaidi...

Penicillin dawa ya kutibu maambukizi ya bakteria mwilini
Post hii Inahusu zaidi dawa za kutibu maambukizi yoyote Yale yanayosababishwa na bakteria dawa hizi kwa kitaamu huiitwa antibiotics Kuna dawa mbalimbali zinazotibu maambukizi ya bakteria leo tutaanza na dawa ambayo inaitwa penicillin. Soma Zaidi...

dawa ya minyoo, dalili za minyoo na sababu na vyanzo vya minyoo
MWISHO Mwisho tunapenda kusema kuwa unapohisi una minyoo kutokana na dalili ambazo tumezitaja humu, nenda kituo cha afya ukapate ushauri zaidi. Soma Zaidi...

Dawa ya kutibu mapunye
DAWA YA MAPUNYEMatibabu ya mapunye inategemea ni wapi mapunjye yapo. Soma Zaidi...

DAWA YA FANGASI
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za fangasi Soma Zaidi...