Fahamu kuhusu dawa ya potassium sparing

Post hii inahusu zaidi dawa ya potassium sparing katika matibabu ya magonjwa ya moyo.

Dawa ya potassium sparing katika matibabu ya magonjwa ya moyo.

1. Dawa hii ya potassium sparing ni mojawapo ya dawa ambazo usaidia katika matibabu ya magonjwa ya moyo,na pia ni mojawapo ya dawa katika kundi la diuretics, dawa hii nayo ufanya Kazi kama dawa nyingine za matibabu ya magonjwa ya moyo ila yenyewe usaidia kudili zaidi na madini ya aina ya potassium ambnayo uongezeka sana mwilini na kusababisha matatizo zaidi hasa kwa wagonjwa wa moyo.

 

2. Kwa matumizi ya dawa hii ya potassium sparing Kuna maudhi madogo madogo ambayo yanaweza kutokea kwa watumiaji wa dawa na udhi la kwanza ni kukojoa mara kwa mara, kupoteza maji mwilini, kiwango cha sodium kupungua mwilini na vile vile kupungua kwa kiwango cha potassium, kushuka kwa presha, kizunguzungu na kukosa nguvu, ngozi kukauka na kuwepo kwa upele kwenye ngozi, na pia dawa hizi zina tabia ya kuleta matokeo mbalimbali kwa wanaume ambayo ni pamoja na.

 

3. Matiti kuvimba kwa wanaume hasa kwa watumiaji wa mda mrefu, na pengine sio kuvimba tu inawezekana mwanaume akawa na matiti kabisa, vile vile kwa wanaume walio wengi upatiwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume au kukosa hamu ya tendo la ndoa,hasa hasa wanaume wanaopatwa na matatizo kama hayo ni wale watumiaji wa dawa ya spirolactone ambayo imo ndani ya  potassium sparing ndio maana dawa hii huitwa potassium sparing diuretics- spirolactone, kwa hiyo spirolactone ndiyo unaleta shida kwa wanaume.

 

4. Kwa hiyo dwa hii inawezekana kabisa kutumiwa na watu mbalimbali kadri ya wataalamu wa afya ila umakini unahitajika kwa wenye presha ya kushuka, watu wenye tatizo la upungufu wa madini mwilini,na wale ambao Wana matatizo kwenye Figo, kwa hiyo dawa hii haipaswi kutumiwa kiholela Bali utumika kulingana na utaratibu wa wataalamu wa afya.

 Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2023/02/04/Saturday - 08:00:39 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 406


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-