image

Fahamu kuhusu dawa ya propranolol ambayo hutibu magonjwa ya moyo

Post hii inahusu zaidi dawa ya propranolol katika matibabu ya magonjwa ya moyo, dawa hii ipo kwenye kundi la beta blockers na ufanya Kazi mbalimbali hasa kwa wagonjwa wa moyo.

Fahamu kuhusu dawa ya propranolol.

1. Kama tulivyoona hapo mwanzoni kwamba hii ni dawa inayotokana na kundi la beta blockers, aina hii ya dawa ya propranolol usaidia kama kuna dalili yoyote ya kuganda damu kwenye sehemu mbalimbali za mwili hasa kwenye ubongo, tunafahamu kabisa kwamba kama kuna tatizo kwenye moyo usafirishaji wa damu huwa ni wa shida hali inayosababisha damu kutofika katika sehemu mbalimbali au pengine mzunguko wa damu kusimama kabisa au pengine damu kuganda, kwa hiyo kama kuna tatizo la damu kwenye ubongo dawa hii usaidia sana.

 

2. Dawa hii ufanya kazi ya kuhakikisha kwamba kuna damu ya kutosha kwenye ubongo kwa kupita kwenye system ya mzunguko wa damu uliopo kwenye ubongo na kuhakikisha kwamba damu inasafirishwa vya kutosha na shughuli za kwenye ubongo zinakuwa sawa kabisa, tunafahamu kwamba kuwepo kwa chumvi nyingi kwenye mfumo wa mzunguko wa damu ni tatizo kwa hiyo na dawa hii upunguza kiwango cha chumvi kwenye mfumo wa damu na hali huwa kawaida tu.

 

3. Pamoja na kazi nzuri ya dawa hii kuna wakati maudhi madogo madogo utokea hasa kwa watumiaji wa mda mrefu na wale wanaoanza kutumia dawa hii, maudhui hayo ni pamoja na mapigo ya moyo kuwa ya chini sana, macho kuwa makavu bila ya maji maji au pengine yanakuwepo kidogo, nywele zinaisha au zinanyonyoka kama wale watumiaji wa mionzi, kichefuchefu na kutapika, udhaifu wa mwili na uchovu wa mara kwa mara.

 

4. Kama maudhi haya ni kidogo kwa wanaoanza kutumia dawa wavumilie kwa sababu uisha taratibu na baadae mwili uweza kuzoea dawa na kama maudhi haya yakiendelea na kuleta matatizo makubwa kama kutapika mara kwa mara uchovu unaokufanya hata usifanye kazi yoyote nywele kuisha karibu zote kichwani, ongea na wataalamu wa afya ili uweze kubadilishiwa dawa kadri ya tatizo la mgonjwa, kwa sababu maudhui madogo madogo mengine yanaweza kufanya mtumiaji wa dawa kupata matatizo badala ya kupona.

 

5. Vile vile watumiaji wa dawa hii wanaweza kuwa na matatizo kwenye ngozi na wengine wanaweza kuona kwamba ni kama aleji hivi yaani kwa watumiaji hasa wale wa mwanzoni wanaweza kuwa na vipengele vidogo vidogo kwenye miili yao, kuwashwa na kujikuna hali inayosababisha mgonjwa pengine kuwa na wasiwasi, na pengine vidonda hivyo vinaweza kueneza mwili mzima na kuwepo kwa maji maji, kwa hiyo hali hiyo ikiendelea ni vizuri kuwaona wataalamu wa afya ili kuweza kutibu hivyo vidonda huku mgonjwa akiendelea na dawa lakini hali hiyo ikijitokeza mara kwa mara ni vizuri kubadilishiwa dawa.

 

6. Vile vile dawa hii ya propranolol ina tabia ya kusababisha kuwepo kwa shida wakati wa upumuaji kwa hiyo utakuta mtumiaji wa dawa anapumua kama mtu mwenye pumu hasa kwa wanaoanza, kwa hiyo ni vizuri kuwaona wataalamu wa afya endapo hali hii inaendelea kila mara ila kwa watumiaji wa dawa wa mwanzoni hali hii uwepo na baadae upitea lakini ikiendelea ni vizuri kabisa kubadilishiwa dawa.

 

7. Katika matumizi ya dawa hii ya propranolol usababisha kubadilisha kiwango cha sukari mwilini, ndio maana kwa wagonjwa wa matatizo ya moyo wanapaswa kupima sukari mara kwa mara,kwa sababu katika matumizi ya dawa nyingine umaliza sukari mwilini hasa dawa hii ya propranolol ina tabia hiyo, kwa hiyo ni vizuri kabisa kwa watumiaji wa dawa hii ya propranolol wale vyakula vyenye sukari kabla na baada ya kutumia au ikiwezekana  kupima sukari mara kwa mara ili kupunguza tatizo la kuishiwa na sukari na pia kupima sukari mara kwa mara ni lazima kabisa.

 

8. Pia watumiaji wa dawa hii ya propranolol mara nyingi miguu yao na mikono huwa ya baridi hasa kwa watumiaji wa mwanzoni na baadae hali huwa ya kawaida, kwa hiyo watumiaji wakihisi hali hiyo hawapaswi kuogopa bali waone ni hali ya kawaida tu,na pengine wanapata shida wakati wa kulala, pengine usingizi hawaupati au wanasinzia wanashutuka shutuka shutuka au kwa wakati mwingine wanakuwa wanajigeuza sana wakati wa kulala kwa ujumla wanakuwa na maangaiko wakati wa kusinzia.

 

9. Kwa wale ambao hawasinzii kabisa na kwa mda mrefu wanapaswa kuwaona wataalamu wa afya ili waweze kubadilishiwa dawa mara moja kwa sababu kitendo cha kukosa usingizi ni kibaya mno na uweza kuleta matatizo makubwa zaidi kuliko yaliyokuwepo,na sio kwa usingizi tu ila maudhi madogo madogo yakiwa ya mda mrefu ni vizuri kuyariport na kupata msaada mapema kuliko kuongeza matatizo.

 

10. Pia dawa hii ya propranolol inawezekana kuleta matatizo kwenye misuli ambayo kwa kitaalamu huitwa muscle cramp au kwa wakati mwingine miguu kulegea na pengine kuchoka baada ya kutembea kwa mda mfupi, au kwa wakati mwingine uzito kuongezeka ghafla unakuta mtu amenenepeana ghafla na hapo misuli umelemewa na kwa hiyo kutembea huwa shida kwa sababu mtumiaji wa dawa uchoka mara kwa mara na kuwepo na maumivu kwenye sehemu mbalimbali za mwili hasa kwenye jointi.

 

11. Kwa hiyo tunaona dawa hii ya propranolol ina maudhi madogo madogo mengi hasa kwa watumiaji wa mwanzo endapo maudhi haya hayatatibika mapema yanaweza kuleta magonjwa au matatizo zaidi kwa watumiaji kwa hiyo ni vizuri kabisa ikitokea hali imebadilika kwa watumiaji ni vizuri kuwaona wataalamu wa afya ili kuweza kuepukana na matatizo makubwa zaidi, na pia dawa hizi hazitumiki kiholela bali ni kwa ushauri wa daktari na wataalamu wengine wa afya,kwa sababu ukitumia kiholela unaweza kujikuta kwenye matatizo makubwa zaidi.

 

12. Pia dawa hii inapaswa kutumiwa na watu mbalimbali kadri ya wataalamu wa afya ila kwa wale wenye matatizo kwenye ubongo wanapaswa kuitumia chini ya uangalizi maalumu,na wale wanaoanguka kifafa wanapaswa kuitumia kwa uangalifu maalum.

 

13. Vile vile napenda kutoa angalizo kidogo kwa wagonjwa wa kisukari na vilevile wana magonjwa ya moyo na wanatumia dawa hii ya propranolol, kama tulivyoona hapo mwanzoni kwamba dawa hii inatabia ya kupunguza kiwango cha sukari mwilini na kwa wale hasa wenye sukari ya kushuka  kabla ya kutumia dawa hii ya propranolol wanapaswa kupima sukari na kuona iko kwa kiasi gani na wakiona iko chini wasitumie dawa hii wahakikishe kwamba sukari inakuwa kwenye hali ya kawaida, na pia wahakikishe kwamba wanakula vyakula vyenye wingi wa sukari na wale na kushiba, na wakiona matumizi ya dawa hii ni shida kwao kwa sababu ya hali yao ya sukari ni vizuri wakabadilishiwa dawa.

 

14. Pia napenda kutoa angalizo tena kwa wale wenye matatizo ya kupumua, hasa wenye pumu na matatizo mengine kama hayo na pia wanatumia dawa hizi ya propranolol wanapaswa kuwaona wataalamu wa afya ili waweze kubadilishiwa dawa kwa sababu kama dawa yenyewe inaleta tatizo la kupumua vipi ikiongezea na tatizo la asili la mgonjwa na hapo hali inaweza kuwa mbaya zaidi, waone wataalamu wa afya kama tatizo linaleta shida.

 

15. Pia na wagonjwa wa akili na wenyewe wanapaswa kuwa kwenye uangalizi zaidi kwa sababu dawa hii inaleta tatizo la kuwaza na kuwasababishia watumiaji kutokuwa na hali ya kawaida vipi kama mtu ana magonjwa ya akili na akiongezea na dawa hii hali huwa mbaya zaidi na kuleta madhara yadiyotarajiwa.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1664


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Fahamu Dawa inayotumika kupunguza maumivu (ibuprofen)
Ibuprofen ni mojawapo ya dawa zinazotumiwa sana duniani kote! Ili kupunguza maumivu na kuvimba, agiza Ibuprofen leo na upate afya bora! Ni kiungo amilifu katika dawa za jina kama vile Motrin na zaidi. Ibuprofen pia inaweza kuuzwa kama: Advil Motrin, Soma Zaidi...

Dawa ya kutibu ugonjwa wa PID
PID ni mashambulizi ya bakteria kwenye mfumo wa uzazi kwa wanawake. Hapa nitakujulisha dawa Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu dawa ya fluoroquinolones/quinolones
Post hii inahusu dawa ya kupambana na bakteria, hili kundi la fluoroquinolones lina dawa kuu mbili ambazo ni ciprofloxin na ofloxacin. Soma Zaidi...

Kazi ya Dawa ya salbutamol
Posti hii inahusu dawa ya salbutamol na kazi yake ya kutibu ugonjwa wa Asthma, ni dawa mojawapo ambayo imetumia na watu wengi na wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa, kwa hiyo zifuatazo ni kazi ya Dawa hii ya salbutamol katika kutibu Asthma. Soma Zaidi...

Nini dawa ya fangasi na Je ni kwel kwamba fangas huweza kuxababxh upungufu wa nguvu za kiume.
Soma Zaidi...

Dawa za mapunye
Somo Hili linakwenda kukuletea dawa za maounye Soma Zaidi...

Mebendazole kama dawa ya kutibu Minyoo.
Post hii inahusu zaidi dawa ya Mebendazole kama Dawa ya kutibu Minyoo, ni dawa inayotumiwa na watu wengi pale wanapokuwa na minyoo, walio wengi wamefanikiwa kupona kwa kutumia Dawa hii. Soma Zaidi...

Fahamu dawa za kutuliza aleji au mzio
Post hii inahusu zaidi dawa hydrocortisone kwa kutuliza aleji au mzio, kwa kawaida Kuna mda mtu anapotumia dawa Fulani anakuwa na mabadiliko mbalimbali kama vile kifua kubana , viupele na mambo kama hayo. Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu dawa ya pyrantel pamoate
Post hii inahusu zaidi dawa ya pyrantel pamoate ni dawa ambayo usaidia kutibu minyoo ambayo kwa kawaida ukaa kwenye utumbo mdogo. Soma Zaidi...

Fahamu dawa za cyclophosphamide na mustargen.
Post hii inahusu zaidi dawa za cyclophosphamide na mustargen katika kupambana na ugonjwa wa Kansa. Soma Zaidi...

Vyakula vya kusaidia katika matibabu ya kiungulia
PoPosti hii inahusu zaidi vyakula ambavyo unaweza kutumia iwapo umepata tatizo la kiungulia Soma Zaidi...

Ni dawa gani hatari kwa mjamzito?
Ukiwa mjamzito uwe makini sana katika kuchagua matumizi ya dawa. Vinginevyobinawwza kuwa hatari. Hapa nitakujuza dawa ambazo ni hatari kutumia kwa ujauzito wako. Soma Zaidi...