Fahamu kuhusu dawa ya pyrantel pamoate

Post hii inahusu zaidi dawa ya pyrantel pamoate ni dawa ambayo usaidia kutibu minyoo ambayo kwa kawaida ukaa kwenye utumbo mdogo.

Fahamu kuhusu dawa ya pyrantel pamoate.

1. Pyrantel pamoate ni aina mojawapo ya dawa ambayo utumika kutibu minyoo ambayo ukaa kwenye utumbo mdogo yaani kwa kitaalamu kwenye intestinal nematode hiyo ndiyo kazi yake na pia inaweza kufanya kazi kama dawa za Albendazole na mebendazole kwa sababu ya kupambana na aina ya minyoo inayotibiwa na na dawa hizo ambayo ni hookworm na pinworn.

 

2. Dawa hii pia ipo kwenye mfumo wa vidonge na pia utafunwa na kumezwa bila maji na pia utumika kabla ya kula kitu chochote ili kuweza kukabiliana vizuri na minyoo ambayo iko tumboni, kwa matumizi yake au namna ya kutumia ni kwa kadiri ya maagizo ya daktari au mtaalamu wa afya.

 

3. Pia dawa hii utumika kwa watu wote wakubwa na wadogo isipokuwa watoto wadogo chini ya miaka miwili na akina Mama wajawazito wenye mimba changa hawapaswi kutumia dawa hii kwa kuepukana na mimba kutoka, kwa hiyo wajawazito wanapaswa kufuata utaratibu wa wataalamu wa afya hasa wakiwa kliniki na sio kununua dawa na kutumia kwa sababu wanaweza kujiletea matatizo makubwa.

 

4. Pia dawa hii huwa na maudhi madogo madogo kama vile maumivu ya kichwa, maumivu ya tumbo, kichefuchefu na kutapika, kizunguzungu, kuchoka mara kwa mara kwa watumiaji wa dawa za pyrantel pamoate wakiona dalili kama hizi ni vema kabisa kufahamu kwamba ni matokeo ya dawa na pia hali ikiwa mbaya ni vema kabisa kuwaona wataalamu wa afya.

 

5. Pia jamii inapaswa kuelewa kwamba dawa hii haitumiki kiholela ni kufuata utaratibu wa wataalamu wa afya na kujua matumizi yake, endapo ikitumika visivyo inaweza kuleta matokeo mabaya kwa watumiaji hasa wajawazito na watoto chini ya miaka miwili, kwa hiyo kwa upande wa wajawazito ni vizuri kufuata masharti ya kliniki hasa mimba ikiwa changa katika matumizi ya dawa na pia mtoto anapaswa kupelekwa kliniki ikitokea kama anaumwa ili apewe dawa zake.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/12/15/Thursday - 11:16:49 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 498


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-