FAHAMU KUHUSU DAWA YA STREPTOMYCIN


image


Post hii inahusu zaidi dawa ya streptomycin ni dawa mojawapo ya kupambana na bakteria hasa wanaoshambulia mfumo wa hewa.


Fahamu dawa ya streptomycin kama dawa inayopambana na bakteria wanaoshambulia mfumo wa hewa .

1. Streptomycin ni mojawapo wa dawa ya kupambana na bakteria hasa bakteria ambao ushambulia mfumo wa hewa , bakteria hao kwa kitaamu huiitwa mycobacterium ni bakteria ambao ueneza kifua kikuu kwa kutumia dawa hii pamoja na dawa nyingine kifua kikuu uweza kutibika kwa kufuata kanuni na utaratibu wa matibabu.

 

2. Dawa hii ya streptomycin inafanya kazi kwa kupitia kwenye mzunguko wa damu na ikifika kwa bakteria inashambulia Ganda la juu ambalo kwa kitaamu huiitwa cell wall na kuingia kwa Ganda la ndani kwa kitaamu huiitwa cell membrane na kujibanza kwenye protein kwa hiyo uzuia protini ya bakteria kuendelea kuzalishwa na kuzuia kuendelea kukua na kusababisha kuharibu kwa bakteria na ugonjwa hauwezi kuendelea kuwepo tena, na mafanikio ya kupona utokea kulingana na udumifu na maelekezo katika matumizi ya dawa.

 

3. Katika kufanya kazi dawa hii upitia sehemu mbalimbali na kuweza kufanikisha uponyaji kwa hiyo dawa hiyo inapoingia mwilini na ikishasambaa uweza kupitia kwenye maji maji mbalimbali kwenye mwili ambayo Kwa kitaamu huiitwa extracellular fluids, na inapiita kwenye plasenta au kwa lugha nyepesi kwenye kondo la nyuma kama mama ana mimba, pia zinaweza kupitia hata kwenye maziwa ya mama kama ananyonyesha na kwenda kwenye maji maji ambayo yamo kwenye ubongo kwa kitaamu huiitwa cerebral Spinal fluids.

 

4. Kwa hiyo kama mama ana mimba anaweza kumkinga mtoto dhidi ya maambukizi ya kifua kikuu,na kama mama ananyonyesha pia anaweza kumsaidia mtoto asipate kama hajapata kwa hiyo kwa watumiaji wa dawa hii wanaweza kusaidia hata vichanga na wanaonyonya .

 

5. Kwa matumizi ya dawa hii Kuna wale ambao hawapaswi kutumia dawa hii kwa mfano wenye aleji na streptomycin,wale wenye upungufu wa damu hawapaswi kutumia, watoto chini ya miezi miwili hawapaswi kutumia na wale wenye matatizo ya Figo wanapaswa kutumia dawa hii kwa kiwango kidogo na kwa wakati mwingine wanawapunguzia dozi.

 

6. Pia dawa hii nayo Ina mahudhi madogo madogo kama maumivu ya kichwa, kuwepo kwa ndoto za kutisha kwa baadhi ya wagonjwa au pengine mgonjwa anaweza kuwa na magonjwa ya akili kama vile kuwa mkimya sana au pengine kuchangamka sana ila ni kwa watu wachache mno, kwa sababu dawa hii upitia kwenye mmengenyo wa chakula Kuna hatari ya kupata kichefuchefu na kutapika, kuharisha pia utokea kukiambatatana na maumivu ya tumbo.

 

7. Kwa watumiaji wa mda mrefu wanaweza kuwa na matatizo ya macho au kuona kwa shida na pia mwili unaweza kuwa na vi upele pamoja na kujikuna kwa mda mrefu na pia dawa hizi zina tabia ya kupunguza damu mwilini wakati wa kutumia ni vizuri kuwa makini kwa wale wenye tatizo la upungufu wa damu wakati wa kutumia dawa hizi, kwa hiyo maudhi haya madogo madogo yakizidi na kuwa kama ugonjwa ni vizuri kabisa kuwaona wataalamu wa afya Ili kubadilishiwaa dawa au kutoa huduma yoyote inayofaa.

 

8. Vile vile dawa hizi uweza kuingiliana na dawa nyingine na kumaliza nguvu dawa hizo na kufanya uponyaji kuwa wa shida, kwa hiyo kwa watumiaji wa penicillin na cephalosporin , dawa hii ya streptomycin uweza kumaliza nguvu dawa hizo na kufanya uponyaji wa kutumia penicillin na cephalosporin kushindwa kufanikiwa, kwa hiyo ni vizuri kuongea na mgonjwa ipasavyo Ili kuweza kuwa na uhakika wa dawa anazozitimia na kuweza kuwepo kwa tiba ya kweli na inayofaa.

 

9. Kwa hiyo katika matibabu au kutumia dawa hii ni vizuri kabisa kuwaona wataalamu wa afya na sio kutumia dawa hii kiholela kwa sababu Zina matokeo mengine ni ya kuhitaji uangalizi na pia dawa hii uingiliana na dawa nyingine ni vizuri kabisa kabla ya kutumia dawa hii kuwaona wataalamu wa afya Ili kuweza kutumia dawa kwa umakinu Zaidi na kuepuka matatizo ambayo yanaweza kutokea.

 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    2 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    3 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    4 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    5 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    6 Mafunzo ya php    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Faida za vidonge vya antroextra
Posti hii inahusu zaidi faida za vidonge vya antroextra, ni vidonge kwa ajili ya mifupa, viungo na gegedu, hivi vidonge vimetumiwa na watu wengi na matokeo yake ni mazuri sana, kwa hiyo zifuatazo ni faida za vidonge hivi. Soma Zaidi...

image Namna ya kutumia tiba ya jino.
Posti hii inahusu zaidi namna au njia ya kufanya Ili kuweza kutumia tiba hii ya jino, kwa sababu ya mchanganyiko ambao umekwisha kuwepo kwa hiyo unachumua mchanganyiko unafanya kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

image Madhara ya kutumia vidonge kwa akina dada vya uzazi wa mpango
Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kwa sababu ya kutumia vidonge vya uzazi wa mpango kwa akina dada. Soma Zaidi...

image Fahamu dawa ya captopril katika matibabu ya magonjwa ya moyo
Post hii inahusu zaidi dawa ya captopril katika matibabu ya magonjwa ya moyo, ni dawa ambayo imo kwenye kundi la vasodilators na ufanya Kazi mbalimbali zinazousu magonjwa ya moyo. Soma Zaidi...

image Faida za dawa za NMN
Posti hii inahusu zaidi faida za dawa za NMN maana yake ni Nicotinamide mononucleotide ni dawa ambazo usaidia kutibu magonjwa mbalimbali kama vile. Soma Zaidi...

image Matibabu ya vidonda vya tumbo nyumbani
Post hii inahusu zaidi matibabu ya vidonda vya tumbo nyumbani, ni njia ya kawaida ya kujitibu vidonda vya tumbo kama tulivyoona. Soma Zaidi...

image Madhara ya vidonge vya P2
Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kwa sababu ya kutumia mara kwa mara vidonge vya P2, Soma Zaidi...

image Dawa ya ALU kama Dawa inayotibu Ugonjwa wa Malaria
Posti hii inahusu zaidi dawa ya ALU kama Dawa inayotibu Ugonjwa wa Malaria ,ni dawa ambayo utumiwa na watu wengi kwa matibabu ya ugonjwa wa Malaria. Soma Zaidi...

image Matibabu ya ugonjwa wa uti wa mgongo
Posti hii inahusu zaidi matibabu kwa mgonjwa wa uti wa mgongo, kwa kawaida tunajua kuwa homa hii ya uti wa mgongo usababisha na wadudu mbalimbali kama vile bakteria, virus, fungasi, sumu mbalimbali kama vile madini ya lead na arseni, na vitu kama vile Magonjwa ya kansa, damu na magonjwa mbalimbali hasa yake makubwa makubwa. Soma Zaidi...

image Fahamu kazi ya dawa ya ampicillin inayopambana na maambukizi ya bakteria
Post hii inahusu zaidi dawa ya ampicillin, ni mojawapo ya dawa za kutibu maambukizi ya bakteria kwenye mwili wa binadamu ba pia ni dawa ambayo IPO kwenye kundi la penicillin kundi hili kwa kitaa huitwa broad spectrum penicillin Soma Zaidi...