Post hii inahusu zaidi dawa za magonjwa ya moyo, ni dawa ambazo utumika kusaidia pale moyo kama umeshindwa kufanya kazi ipasavyo.
Dawa za kutibu magonjwa ya moyo.
1. Kwanza kabisa kabla hatujaanza kuchambua dawa moja baada ya nyingine tunapaswa kufahamu kabisa kuhusu magonjwa ya moyo, ambapo kwa lugha ya kitaalamu magonjwa ya moyo huitwa cardiac failure , magonjwa ya moyo ni hali ambayo utokea kama moyo umeshindwa kufanya kazi yake vizuri kwa mfano moyo kushindwa kusukuma damu kwenye sehemu mbalimbali za mwili.
2. Kwa kawaida kuna dalili mbalimbali ambazo zinaweza kujitokeza kama moyo haufanyi kazi vizuri na dalili hizi ni pamoja na uchovu wa mara kwa mara, kushindwa kupumua vizuri, na wakati mwingine kifua kubana , kukonda kusiko kwa kawaida hata kama mgonjwa anakuwa anatumia chakula na dalili nyingine zinaweza kujitokeza kutoka kwa mgonjwa mmoja kwenda kwa mwingine.
3. Kutokana na kuwepo kwa magonjwa ya moyo kuna dawa mbalimbali ambazo utumika kutibu magonjwa ya moyo na lengo la dawa hizi ni kuhakikisha kwamba moyo unafanya kazi yake ipasavyo na kuhakikisha kwamba maumivu mbalimbali hayatokei kwa mgonjwa na pia dawa hizo zinatofautiana kutoka kwa dawa moja kwenda kwa nyingine kadri ya tatizo lilivyo.
4. Kuna dawa za moyo ambazo usaidia kama presha iko juu kitendo hiki kwa kitaalamu huitwa high blood pressure, hali hiyo uitwa magonjwa ya moyo kwa sababu kuna kipindi moyo unatumia nguvu kubwa kusukuma damu kwenye sehemu mbalimbali za mwili, hali hii ya moyo kutumia nguvu kusukuma damu utokea kwasababu ya mishipa ya damu kuwa nyembamba na kusababisha damu kutoweza kufika sehemu mbalimbali za mwili kusababisha moyo kutumia nguvu hali inayosababisha shinikizo la damu. Kwa hiyo kuna dawa za kutibu hali hiyo ya shinikizo la damu.
5. Pia kuna dawa za moyo ambazo usaidia kwenye matibabu ya kupambana na shinikizo kali la damu ambalo usababisha kiharusi, kwa kitaalamu huitwa stroke na myocardial infarction, kwa kawaida tunafahamu kwamba iwapo shinikizo la damu limekuwa sugu usababisha kiharusi ,kwa hiyo pia tutaweza kuona dawa za kutibu hali hiyo.
6 pia kuna dawa vile vile ambazo usaidia kutibu hali ya presha kuwa chini, kuna kipindi baada ya presha kubaki kwenye hali yake ya kawaida yenyewe inashuka hali inayosababisha matatizo kwa mgonjwa kama matibabu hayajatolewa, kwa hiyo tutaweza kuona dawa za kutibu hali hiyo.
7. Pamoja na kujua aina mbalimbali za magonjwa ya moyo tutaona jinsi dawa zinazotumika kutibu magonjwa ya moyo jinsi zinavyofanya kazi , kwanza dawa hizi uondoa chumvi kwenye moyo na maji yaliyozalishwa kwenye moyo na kusababisha moyo kuwa kawaida na kuweza kufanya kazi vizuri,kwa hiyo ili moyo ufanye kazi unahitaji chumvi na maji sawia yaani viwe vya kawaida, kwa hiyo maji yakiwa mengi kuzidi na chumvi ikizidi kwenye moyo ni hatari sana.
8. Pia dawa hizo usaidia kupandisha presha kama imeshuka na kuiweka kwenye hali ya kawaida, dawa ambayo kwa kawaida utumika uhakikisha kwamba presha hatishuki ovyo ovyo.
9. Pia dawa hizo upanua mishipa ya damu kama ni midogo na kusababisha damu kuweza kupita vizuri na kwenda kwenye sehemu mbalimbali za mwili na kushusha presha na ikiwa ya kawaida.
10. Baada ya kufahamu kazi za dawa hizi za magonjwa ya moyo na kufahamu magonjwa mbalimbali ya moyo ni vizuri kufahamu kwamba kila ugonjwa wa moyo huwa na dawa zake maalum ambazo utumika kutibu ugonjwa huo kwa hiyo ni vizuri kabisa kufuata utaratibu wa wataalamu wa afya.
11. Kwa hiyo baada ya kufahamu tofauti za magonjwa ya moyo ni vizuri kupima kwanza ili kufahamu kwamba upo kwenye kundi gani na kupewa dawa kadri ya tatizo.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Dawa Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1646
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya
👉2 Madrasa kiganjani
👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉4 kitabu cha Simulizi
👉5 Kitau cha Fiqh
👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Ijue Dawa ya lignocaine
Posti hii inahusu zaidi dawa ya lignocaine kama mojawapo ya Dawa ambayo utumika wakati wa upasuaji. Soma Zaidi...
Fahamu Dawa inayotibu minyoo iitwayo albenza (albendazole)
Albenza (albendazole) hutumika kutibu magonjwa ya minyoo ya ndani ikiwa ni pamoja na maambukizi ya minyoo ya tegu. Albenza inafanya kazi kukomesha kuenea kwa maambukizo ya minyoo kwenye chanzo, na kukata chanzo chao cha nishati, na hivyo kuzuia kuenea k Soma Zaidi...
Fahamu dawa za 5-fluorouracil,Tegafur na uracili
Post hii inahusu zaidi dawa za 5-fluorouracil, Tegafur na uracili katika kupambana na kansa. Soma Zaidi...
Fahamu dawa ya sulfonamide dawa inayopambana na maambukizi ya bakteria mwilini.
Post hii inahusu zaidi dawa ya sulphonamide ni mojawapo ya dawa ambayo usaidia kutibu magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na bakteria ni dawa au antibiotics ya mda mrefu na pia matumizi yake sio makubwa sana kwa sababu ya kuwepo kwa antibiotics zenye ngu Soma Zaidi...
Mgawanyo wa tiba ya kifua kikuu
Post hii inahusu zaidi mgawanyiko wa tiba ya kifua kikuu, kwa kawaida tiba hii imegawanyika katika sehemu kuu mbili. Soma Zaidi...
Mebendazole kama dawa ya kutibu Minyoo.
Post hii inahusu zaidi dawa ya Mebendazole kama Dawa ya kutibu Minyoo, ni dawa inayotumiwa na watu wengi pale wanapokuwa na minyoo, walio wengi wamefanikiwa kupona kwa kutumia Dawa hii. Soma Zaidi...
Tiba mbadala za vidonda vya tumbo
Somo hili linakwenda kukuletea tiba mbadala za vidonda vya tumbo Soma Zaidi...
Fahamu antibiotics ya asili.
Post hii inahusu zaidi antibiotics ya asili, ni antibiotics inayotumia vitu vya kila siku na ya kawaida na mtu akaweza kupona kabisa na kufanya kazi kama antibiotics ya vidonge vya kawaida. Soma Zaidi...
Ifahamu dawa ya epinephrine kwa kutuliza aleji
Post hii inahusu zaidi dawa ya epinephrine kwa kutuliza aleji ni dawa ambayo imependekezwa kutuliza aleji kama dawa ya hydrocortisone, Prednisone hazipo au zimeshindwa kufanya kazi. Soma Zaidi...
Dawa ya Vidonda vya tumbo
Nitakujuza dawa ya kutibu vidonda vya tumbo, na kutibu vidonda vya tumbo sugu Soma Zaidi...
Fahamu dawa za kisukari
Post hii inahusu zaidi dawa za kisukari, kwa sababu ya kuwepo kwa ugonjwa wa kisukari vilevile kuna dawa zake ambazo utumika kurekebisha sukari kama imepanda au kushuka. Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu dawa ya potassium sparing
Post hii inahusu zaidi dawa ya potassium sparing katika matibabu ya magonjwa ya moyo. Soma Zaidi...