Post hii inahusu zaidi kundi la diuretics,ni kundi mojawapo kati ya makundi ya dawa zinazosaidia katika matibabu ya magonjwa ya moyo.
Fahamu kuhusu kundi la diuretics.
1. Diuretics ni mojawapo ya kundi kwenye dawa za kutibu magonjwa ya moyo,kundi hili pia Lina dawa mbalimbali ambazo utumika kwenye matibabu, kundi hili la dawa ni kuzalisha mkojo Ili kuweza kutoa sumu mwilini ambazo ni chanzo cha kusababisha kuwepo au kuongezeka kwa tatizo kwenye moyo.
2. Dawa hizi ambazo zipo kwenye Kundi hili la diuretics zikitumika uweza kufanya kazi kupitia kwenye Figo na baadae kuongeza kiwango cha kuzalishwa kwa mkojo , kwa hiyo baada ya kutolewa mkojo nje uweza kusababisha moyo kuendelea na kazi yake kama kawaida,kwa sababu sumu utoka nje kupitia kwenye mkojo.
3. Dawa hizi kwenye kundi la diuretics ni pamoja na furosemide, bendofurothiazide, potassium sparing diuretics- spirolactone na amiloride hizi dawa ni kutokana na kundi Moja la diuretics lakini ufanya Kazi tofauti tofauti kutegemea na tatizo la mgonjwa.
4. Vili vile dawa hizi huwa na maudhi madogo madogo katika matumizi na maudhi hayo ni pamoja na kukojoa sana au pengine kizunguzungu na kutapika hasa kwa watumiaji ambayo wanaaoanza kutumia dawa,pia dawa hizi zina tabia ya kupandisha sukari juu ,kwa hiyo wenye tatizo la ugonjwa wa kisukari hasa ya kupanda wanapaswa kuwa makini katika matumizi ya dawa hii.
5. Vili vile kwa sababu dawa hii Inafanya mtu akojoe sana Ina tabia vile vile ya kupunguza madini mwilini kwa sababu madini mengi upitia kwenye mkojo na kutolewa nje, kwa hiyo ni vizuri na kuwa makini kwa wale wenye tatizo la upungufu wa madini mwilini.
6. Vile vile dawa hizi zinapaswa kutumiwa kadri ya wataalamu wa afya sio kuzitumia kiholela na pia watu wenye tatizo la kisukari hasa ya kupanda na wale wenye tatizo la upungufu wa madini mwilini wanapaswa kuwa macho katika matumizi.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Post hii inahusu zaidi dawa ya macrolide ni mojawapo ya dawa ya kutibu au kupambana na bakteria na upambana na bakteria wafuatao streptococcus pyogenes, staphylococcus aureus na haihusiki na haemophilia influenza ambao usababisha maambukizi kwenye mfumo w
Soma Zaidi...PID ni mashambulizi ya bakteria kwenye mfumo wa uzazi kwa wanawake. Hapa nitakujulisha dawa
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa za Doxorubicin and Daunorubicin katika kupambana na kansa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kazi ya paracetamol katika kutuliza maumivu, ni Aina ya dawa ambayo utumiwa sana katika kutuliza maumivu kwa wagonjwa.
Soma Zaidi...PoPosti hii inahusu zaidi vyakula ambavyo unaweza kutumia iwapo umepata tatizo la kiungulia
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya cloxacillin ambayo Iko kwenye kundi mojawapo la penicillin ambalo uzuia enzymes zinazotengenezwa na bakteria.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya Rifampin kama dawa mojawapo ya kutibu kifua kikuu.
Soma Zaidi...hapa utajifunza dalili za fangasi, dawa ya fangasi na aina za fangasi, pia nitakujuza njia za kukabiliana na fangasi
Soma Zaidi...