Fahamu kuhusu madhara ya uzito mkubwa
Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kwa mtu mwenye uzito mkubwa,kwa kawaida ili mtu aweze kuwa na uzito wa kawaida ni vizuri na kiafya kupima urefu ukilinganisha na uzito wa mtu.
Madhara ya uzito kuwa mkubwa.
1 kwanza kabisa tunafahamu kwamba uzito mkubwa ni chanzo cha matatizo mbalimbali kwenye mwili wa binadamu, kuna watu wengine ni kawaida kuwaa wanene kwa sababu familia yao yote wanafanana hivyo wanakuwa na miili mikubwa pia na uzito mkubwa,ila kama kwa asilimia mwili ulikuwa mdogo na kwa sababu ya mtindo wa maisha mwili umeongezeka ni vizuri kabisa kuhakikisha kuwa umepunguza uzito kwa namna moja au nyingine kwa sababu kuna madhara mbalimbali yanaweza kutokea kwa sababu ya kuwepo kwa uzito mkubwa kama tutakavyoona.
2. Kuwepo kwa maumivu makali kwenye mgongo.
Maumivu hayo uanzia kiunoni na kushuka kueneza kwenye mgongo hali hiyo utokea kwa sababu pingili za kwenye mgongo Uweza kuelemewa na kusababisha pingili kuchoka na kusababisha maumivu kwenye mgongo hali ambayo kwa wakati mwingine usababisha pingili za kwenye utu wa mgongo kusagika.
3. Kuna wakati mwingine kama unene umekuwa mkubwa sana usababisha matatizo mbalimbali ambayo ni pamoja na kushindwa kubeba ujauzito kwa wanawake kwa hiyo ni vizuri kabisa kupunguza uzito ili kuweza kupunguza na matatizo mengine ya maisha yakiwemo kushindwa kubeba mimba.
4. Kuwepo kwa shinikizo la damu.
Kwa kawaida unene na uzito ukiwa mwingi pia usababisha na kuwepo kwa Tatizo la shinikizo la damu kwa sababu mishipa huwa midogo na kusababisha moyo kutumia nguvu ili kuweza kusukuma damu kwa nguvu kwenye sehemu mbalimbali za mwili.
5. Kuwepo kwa kufa ganzi kwenye sehemu mbalimbali.
Kuna kipindi kunakuwepo na ganzi kwenye sehemu mbalimbali za mwili kwa sababu ya hewa ya oxygen gas inakuwa haifiki sehemu mbalimbali za mwili na kusababisha kuwepo kwa ganzi kwenye mikono, miguu na sehemu nyingine.
6. Kwa hiyo ni vizuri kabisa kuhakikisha kwamba tunapunguza uzito na kuwa kwenye hali ya kawaida kwa sababu kuwepo kwa uzito mkubwa ni chanzo cha kuwepo pia kwa magonjwa mbalimbali.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitau cha Fiqh 👉2 Kitabu cha Afya 👉3 Dua za Mitume na Manabii 👉4 ai web app 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
Jinsi moyo unavyosukuma damu
Post hii inahusu zaidi jinsi moyo unavyosukuma damu, moyo ni ogani ambayo usukuma damu kwenye sehemu mbalimbali za mwili.
Soma Zaidi...Kushiriki ngono na mtu aliye na vvu na ukimwi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu kushiriki-ngono-na-mtu-aliye-na-vvu-na-ukimwi
Soma Zaidi...fahamu kuhusu vitamini B na faida zake
makala hii inakwenda kukupa faida, kazi na athari za vitamini B mwilini. Nini hutokea endapo utakuwa na upungufu wa vitamini B mwilini?
Soma Zaidi...HUDUMA YA KWANZA KWA MWENYE KIZUNGUZUNGU
Unapokuwa na kizunguzungu unashindwa kuudhibiti mwili wako, unaweza kuanguka kabisa.
Soma Zaidi...Imani potofu kuhusu kifua kikuu
Posti hii inahusu zaidi imani potofu waliyonayo Watu kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu, hizi ni imani ambazo uwepo kwenye jamii na pengine uweza kuaminika lakini si za ukweli.
Soma Zaidi...Zijue dalili za upungufu wa maji mwilini
Posti hii inaelezea kuhusiana na upungufu wa maji mwilini
Soma Zaidi...