image

Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Bawasili

Posti hii inahusu zaidi juu ya ugonjwa wa Bawasili, ni ugonjwa unaotokea kwenye njia ya haja kubwa hali ambayo upelekea kuwepo kwa uvimbe au nyama ambazo uonekana hadi nje, kwa lugha ya kitaalamu ujulikana kama haemorrhoid au pokea.

Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Bawasili.

1. Pamoja na kuwepo kwa Ugonjwa huu kuna aina mbili za Ugonjwa wa Bawasili kuna Bawasili ya nje ambayo uonekana kwa nje na kuna Bawasili ya ndani ambayo uonekana kwa ndani kwa hiyo tutaziona moja baada ya nyingine.

 

2. Bawasili ya nje. 

Aina hii ya Bawasili utokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa  na kuambatana na maumivu makali kwa mgonjwa na pia utokea miwasho wa ngozi katika sehemu hiyo  mara nyingi katika sehemu hiyo mishipa ya damu yaani veini upasuka  na damu kuganda  hivyo kusababisha aina hii ya Bawasili ambapo kwa kitaalamu huitwa thrombosed haemorrhoid.

 

3. Pia aina ya pili ya Bawasili ni Bawasili ya ndani.

Aina hizi ya Bawasili ni tofauti na ya kwanza hii kwa kawaida utokea ndani ya mfereji wa haja kubwa pia nayo uambatana na Maumivu ambayo Usababisha Mgonjwa kuumia sana na pengine miwasho inaweza kutokea kwa nje .

 

4. Baada ya kuona aina kuu mbili za Bawasili yaani Bawasili ya ndani na nje na matokeo yake ni hali ya kuwepo kwa maumivu makali yanayoambatana na miwasho, kwa hiyo ni vizuri kabisa kutafuta matibabu ili kuweza kuondokana na tatizo hili kwa sababu watu walio wengi wanapuuza kuwepo kwa dawa hospitalini wanakimbilia dawa mbadala ambazo kwa wakati mwingine zinaweza kusababisha madhara zaidi kuliko kuponesha .

 

5. Kwa hiyo baada ya kuona aina hizi ni vizuri kuwaona wataalamu wa afya na kuachana na mila potovu kabisa ambazo zinaweza kuleta madhara zaidi, kwa hiyo kwa watumiaji wa dawa mbadala ambazo uaminika na walio wengi ni vizuri kuzitumia ila tahadhari ni lazima na kama hali ikiwa mbaya katika matumizi ya dawa mbadala ni vizuri kabisa kumwona mtaalamu wa afya na kumweleza kila kitu kwa ukweli ili kusaidia katika kudili na tatizo.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 887


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Matatizo yanayosababisha mshtuko wa moyo.
Mshtuko wa moyo hutokea wakati mtiririko wa damu kwa moyo umezuiwa, mara nyingi kwa mkusanyiko wa mafuta, cholesterol na vitu vingine, ambayo huunda plaque katika mishipa inayolisha moyo (mishipa ya moyo). Mtiririko wa damu ulioingiliwa unaweza kuharibu Soma Zaidi...

Fangasi wa sehemu za Siri
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu fangasi wa sehemu za Siri Soma Zaidi...

Njia za jumla za kujikinga na magonjwa mbalimbali
Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kujikinga na magonjwa, kwa kawaida tunajua wazi kuwa magonjwa yapo na yanasambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na mengine hayasambai yanaweza kumpata mtu mmoja akapona au magonjwa mengine si ya kupona Soma Zaidi...

Je maumivu juu ya kitovu ni miongoni mwa dalili za mimba?
Kama unahisi maumivu ya tumbo huwenda umejiuliza swali hili ukiwa kama mwanamke "Je maumivu juu ya kitovu ni miongoni mwa dalili za mimba?". Post hii inakwenda kujibu swali hili Soma Zaidi...

Dawa za kutuliza vvu zinaongeza damu
Hakuna dawa ya UKIMWI ya kutibu kuondoa virusi mwilini, lakini zipo dawa za kuweza kupunguza makali ya virusi hawa. Hivi unesha jiuliza kuwa je zile dawa zinaongeza damu? Soma Zaidi...

Fangasi watambulikao kama invasive candidiasis
Hawa huweza kuingia kwenye mfumo wa damu na kuenda maeneo mengine nyeti sana ya mwili. Soma Zaidi...

Dalili na sababu za mawe kwenye in yaani liver stone au intrahepatic stones
Katika post hii utakwend akujifunza kuhusu tatizo la kuwa na vijiwe kwenye ini vijiwe hivi hufahamika kama intrahepatic stones. Soma Zaidi...

Maumivu ya magoti.
Maumivu ya magoti ni malalamiko ya kawaida ambayo huathiri watu wa umri wote. Maumivu ya goti yanaweza kuwa matokeo ya jeraha, kama vile ligament iliyopasuka au cartilage iliyochanika. Soma Zaidi...

Daliliza shinikizo la Chini la damu.
Shinikizo la chini la damu (hypotension) litaonekana kuwa jambo la kujitahidi. Hata hivyo, kwa watu wengi, shinikizo la chini la damu linaweza kusababisha dalili za Kizunguzungu na kuzirai. Katika hali mbaya, shinikizo la chini la damu linawez Soma Zaidi...

Dalilili za maumivu ya kifua
Maumivu ya kifua huja kwa aina nyingi, kuanzia kuchomwa na kisu hadi kuuma kidogo. Baadhi ya Maumivu ya kifua yanafafanuliwa kama kuponda kuungua. Katika baadhi ya matukio, maumivu husafiri juu ya shingo, hadi kwenye taya. Soma Zaidi...

Tatizo la Kikohozi Cha muda mrefu
Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili za Kikohozi cha muda mrefu ni zaidi ya kero. Kikohozi cha muda mrefu kinaweza kuharibu usingizi wako na kukuacha unahisi uchovu. Matukio makali ya kikohozi cha muda mrefu yanaweza kusababisha kutapika, kizunguz Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Bawasili
Posti hii inahusu zaidi juu ya ugonjwa wa Bawasili, ni ugonjwa unaotokea kwenye njia ya haja kubwa hali ambayo upelekea kuwepo kwa uvimbe au nyama ambazo uonekana hadi nje, kwa lugha ya kitaalamu ujulikana kama haemorrhoid au pokea. Soma Zaidi...