Fahamu kuhusu Ugonjwa wa ukoma

Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa ukoma, ni Ugonjwa unaosababishwa na mdudu anayeitwa mycobacterium leprae, mdudu huyu kwa kawaida uathiri sana sehemu za ngozi na sehemu za Neva mbalimbali za mwili

Fahamu kuhusu Ugonjwa wa ukoma.

1. Kwa kawaida hapo mwanzoni kabisa Ugonjwa huu haukuwa na dawa , kwa hiyo watu waliopatwa na Ugonjwa huu walionekana ni watu wenye balaa kwa hiyo hawakuruhusiwa kuishi na watu wengine kwenye jamii, lakini kadiri siku zinavyokwenda kutoka siku moja kwenda nyingine watu wameelewa kuhusu Ugonjwa huu na dawa imepatikana kwa hiyo watu wanapona kwa kufuata mashariti mbalimbali.

 

2.ugonjwa  huu uweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya kugusana na mtu mwenye ukoma hasa wakigusana na maji maji ya mtu mwenye ukoma na hasiye na ukoma na pengine kwa njia ya hewa hizi , kwa hiyo watu wanapaswa kuwa makini wakati wanapoishi na watu wa ukoma ili kuweza kuepuka hali ya kusambaa kwa ugonjwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

 

3. Pia mgonjwa anaweza kuwa na Dalili mbalimbali kama vile kuharibika kwa ngozi, kuharibika kwa mfumo wa Neva, pengine mtu anaweza kuwa mgumba kama Ugonjwa umeingia mpaka ndani, pia kunakuwepo na kuharibika kwa mifupa na pengine mtu anaweza kuwa mgumba, kwa hiyo Dalili hizo uweza kuanza taratibu na kuenea taratibu kwenye mwili wa mtu na matibabu yasipotolewa mapema hali ya mtu huwa mbaya zaidi.

 

4. Kwa hiyo tunajua wazi kuwaa Ugonjwa huu una tiba na dawa zipo kwa hiyo hakuna sababu ya kuwatenga wagonjwa walioathirika na Ugonjwa huu kwa sababu matibabu yakitolewa ipasavyo Mgonjwa anapona Kawaida na kurudia kwenye hali ya kawaida,kwa hiyo watu wenye tabia ya kutenga wagonjwa wenye matatizo haya wanapaswa kupewa elimu ili kuweza kuwajali wagonjwa hawa ili waweze kupata matibabu ipasavyo.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/06/08/Wednesday - 07:26:43 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1386


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-