Menu



fahamu kuhusu vitamini B na faida zake

makala hii inakwenda kukupa faida, kazi na athari za vitamini B mwilini. Nini hutokea endapo utakuwa na upungufu wa vitamini B mwilini?

Fahamu vitamini B na kazi zake, Vyakula vya vitamini B na athari za upungufu wake

Vitamini B ni katika water soluble vitamin ambavyo vina kazi ya kuhakikisha kuwa michakato yote ya kikemikali mwilini inakwenda vizuri. Na hapa tunazungumzia kitaalamu metabolism. vitamini B vipo katika makundi mengi kma aB1, B2, B3, B5, B6, B7 na B12. katika makala hii nitakwenda kukueleza maana ya vitamini hivi, nini kazi zake hasa mwilini, wapi nitapata vitamini B na je ni zipi dalili za upungufu wa vitamini hivi.


 

Yaliyomo:

  1. Maana ya vitamini B
  2. Makundi ya vitamini B
  3. Kazi za vitamini B
  4. Vyakula vya vitamini B
  5. Upungufu wa vitamini B
  6. Athari za kuwa na vitamini B kupitiliza


 

Vitamini B ni nini?

Vitamini B ni katika kundi la vitamini vinavyofahamika kama water soluble vitamin. vitamini B ni kundi la vitamini ambavyo vinafanana sifa lakini vina utofauti kidogo. Vitamini B ndani ya miili yetu vinafanya kazi ya kuhakikisha kuwa michakato ya kikemikali inafanyika, michakato hiyo kitaalamu inafahamika kama metabolism.


 

Metabolism hii ni michakato ya kikemikali inayofanyika ndani ya seli kwa ajili ya mambo makuu matatu nayo ni:-

  1. Kubadili chakula kuwa nishati (nguvu)
  2. Kubadili chakula ama nishati kkuwa protein, carbohydrate, lipids na nucleic acid.
  3. Kuondoa uchafu na sumu mwilini (nitrogen waste)

Hivyobasi michakato hii yote ili ifanyike kwa ufasaha na ufanisi vitamini B vinahitajika katika miili yetu. Endelea kusoma makala hii ukaone kazi za vitamini B.


 

Makundi ya vitamini B

Makundi hayo ya vitamini B ni:

  1. B1 kitaalamu huitwa thiamine, hivi vimegunduliwa mwaka 1910 na mwanasayansi iliyeitwa Umetaro Suzuk Pia mwaka 1912 mwanasayansi aliyeitwa Casimir Funk aligundua thiamine.


 

  1. B2 kitaalamu huitwa riboflavinhivi navyo vimegunduliwa mwaka 1926 na wanasayansi wawili wanaokwenda kwa majina D.T Smith na E.G Hendrick.


 

  1. B3 pia hutambulika kama niacinau nicotinic acid kundi hili limegunduliwa mwaka 1937 na mwanasayansi anayekwenda kwa jina la Conrad Elvehjem.


 

  1. B5 na yo pia huitwa pantothenic acid, kundi hili limegunduliwa mwaka 1933 na Roger J. Williams


 

  1. B6 pia huitwa pyridoxine, pyridoxal, au pyridoxamine imegunduliwa na Paul Gyorgy mwaka 1934.


 

  1. B7 pia hufahamika kama biotinmwanasayansi aitwaye Margaret Averil Boas aliigundua vitamini hii miaka ya 1900


 

  1. B9 pia hujulikana kama folic acidMwanasayansi kwa jina la Lucy Wills aliigundua mwaka 1983


 

  1. B12 ama cobalaminshii imegunduliwa na jopo wanasayansi mbalimbali.


 

Kazi za vitamini B mwilini Na upungufu wa vitamini B mwilini

Kama tulivyoona kuwa kazi za vitamini B ni kuhakikishha kuwa mipambano ya kikemikali inafanyika ndani ya seli. Sasa hapa tutaona kazi za vitamini hivi kulingana na makundi yake:-


 

B1 hii husaidia mfumo wa fahamu (mfumo wa neva) kufanya kazi vyema. Upungufu wa vitamini hivi B1 huweza kuleta maatizo kwenye mfumo wa fahamu, moyo na mupotea kwa misuli.


 

B2 huhitajika kwa ajili ya uzalishwaji wa nishati, lipi, vitamini, madini na husaidia katika utengenezwaji wa antioxidant. Upungufu wa vitamini hivi huweza kusababisha kuvimba (imflamation) kwenye ngozi, ulimi, midomo, na matatizo kwenye mfumo wa fahamu.


 

B3 hii huhitajika katika kufanyika mchakato wa metabolism kwenye seli. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea ngozi kuwa na matatizo kama miwasho, mapele, ukurutu na kadhalika. Pia upungufu wa vitamini hivi huweza kusababisha tumbo kuvurugika na kuleta misongo ya mawazo




 

B6 hii hufanya kazi ya kuhakikisha metabolisma inayohusima katika kuchakata hamirojo asidi za amino, kuchakata hemoglobin hizi ni chembechembe za kwenye seli nyekundu za damu zinazo saidia katika kusafirisha hewa mwilini, pia katika kuthibiti kiwango cha sukari kwenye damu. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea madhara kwenye ubongo, shida kwenye fahamu ya mtu na pia ugonjwa wa anemia unaonasibiana na upungufu wa hewa ya oksijeni mwilini.


 

B9 huhusika katika kuchakata DNA, kuchakata amino acid, katika kukua na kukomaa kwa seli mwilini hasa hasa seli hai nyekundu. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea matatizo katika ukuaji, utengenezwaji na ukomaaji wa seli hai nyekundu za damu, uchovu, maumivu ya kichwa, kutokea uvimbe kwenye mdomo na hata kuathiri mtoto aliyepo tumboni.




 

B12 huhitajika kwa ajili ya utengenezwaji wa seli mpya, utengenezwaji wa damu na pia kwa ajili ya mfumo wa fahamu kufanya kazi vyema. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea kuvurugika kwa tumbo, shida kwenye mfumo wa fahamu pamoja na matatizo kwenye ulimi.


 

Vyakula vya vitamini B

Tunaweza kupata vitamini B kwenye vyakula vifuatavyo:-

  1. Nyama
  2. Nafaka kama mchele, mtama, mahindi n.k
  3. Mimea jamii ya maharagwe kama kunde
  4. Viazi
  5. Ndizi
  6. Pilipili
  7. Mayai
  8. Mimea jamii ya karanga na alizeti
  9. Mboga za majani zenye kijani iliyowiviana na kutia weusi kama spinachi
  10. Matunda kama palachichi na ndizi


 

Dalili za upungufu wa vitamini B

  1. Kupata ugonjwa wa Anaemia huu ni upungufu wa hewa ya oksijeni mwilini
  2. Matatizo kwenye ngozi
  3. Kupata vidonda kwenye mdomo, ma kupasuka kwa mdomo
  4. Misongo ya mawazo ama kuchanganyikiwa
  5. Kuharisha
  6. Kupotesa kumbukumbu kwa urahisi
  7. Misuli kupoteza ujazo
  8. Kubadilika badilika kwa mood (fikra na hisia) yaani mara umekasirika mara umefurahi


 

Athari za kuwa na vitamini b kupitiliza

  1. Kichefuchefu
  2. Kuona maluelue
  3. Kutapika
  4. Kuharisha
  5. Maumivu ya tumbo
  6. Shida kwenye ngozi
  7. Kuzidi kwa kiu


 

Makala nyingine kwa ajili yako:

  1. Vyakula vya protini
  2. Vyakula vya vitamin K
  3. Vyakula vya vitamini C
  4. Afya ya uzazi
  5. Afya na magonjwa

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea

Ndio     Hapana     Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Huduma Main: Post File: Download PDF Views 1885

Share On:

Facebook WhatsApp

Post zinazofanana:

Namna ya kuchoma chanjo

Posti hii inahusu zaidi namna ya kuchoma chanjo, ni njia ambazo utumika kutoa chanjo kwa watoto na watu wazima kwa utaratibu uliowekwa.

Soma Zaidi...
Fahamu kuhsu vitamini E na kazi zake mwilini

Je unazijuwa faida za kuwa na vitamini E mwilini mwako.Unahani utapata matatizo yapi ya kiafya endapo utakuwa na upungufu wa vitamini E mwilini? Makala hii ni kwa ajili yako.

Soma Zaidi...
Msaada kwa wenye tonsils

Posti hii inahusu zaidi msaada kwa wenye tonsils, kwa wale wenye tonsils wanapaswa kufanya yafuatayo ili kuweza kupambana na ugonjwa huu.

Soma Zaidi...
Nini husababisha kizunguzungu?

Posti hii inazungumzia kuhusiana na Mambo mbalimbali ambayo husababisha kizunguzungu.

Soma Zaidi...
Kumsaidia mtu aliyeingiwa na uchafu au kitu chochote machoni

Posti hii inahusu hasa jinsi uchafu, wadudu na vitu vingine vinavyoweza kuingia machoni.macho ni mojawapo ya milango mitano ya fahamu ambapo kazi yake ni kuona.

Soma Zaidi...
Namna ya kumhudumia mtu aliyeingongwa na nyoka

Posti hii inahusu njia na namna ya kumhudumia aliyeingiwa na nyoka. Nyoka ni kiumbe ambacho Kina sumu kali na mtu akifinywa na nyoka asipohudumiwa anaweza kupata ulemavu au kupoteza maisha

Soma Zaidi...
Upungufu wa damu mwilini

Post inaenda kuzungumzia kuhusiana na upungufu wa damu mwilini ambapo tutaona SABABU na dalili zake lakin upungufu wa damu mwilini hujulikana Kama ANEMIA.

Soma Zaidi...
Faida za tumbo katika mwili wa binadamu

Posti hii inahusu zaidi faida za tumbo,tumbo ni sehemu ya mwili ambayo ushughilika na kutunza chakula,

Soma Zaidi...
Zijuwe athari za vidonda mwilini

Posti hii inahusu zaidi athari za kutotibu vidonda, hizi ni athari mbalimbali ambazo zinaweza kutokea ingawa kama vidonge haujatibiwa au vimetibiwa kwa kuchelewa.

Soma Zaidi...
Mambo ya kuzingatia unapokuwa unatoa huduma ya kwanza

Huduma ya kwanza ni huduma inayotolewa kwa mtu yeyote aliyepata ajali au mgonjwa yeyote kabla hajapelekwa hospitalini

Soma Zaidi...