FAHAMU UGONJWA WA KASWENDE WAKATI WA UJAUZITO.


image


Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa kaswende wakati wa ujauzito, kaswende inaweza kukaa kwa mtu zaidi ya miaka mingi bila kuleta madhara ya moja kwa moja lakini kadiri ya siku zinavyokwenda madhara utokea hasa wakati wa ujauzito, madhara hayo umwadhiri mtoto zaidi.


Kaswende wakati wa ujauzito.

1. Kaswende ni ugonjwa ambao uenezwa na mdudu ambaye kwa kitaalamu huitwa Treponema pallidum ambaye kwa kawaida upitia kwenye njia ya kujamiiana kwa mtu ambaye ana ugonjwa huo akijamiiana na mtu ambaye hana ugonjwa huo,kwa kawaida wadudu hao wakiwa kwenye damu ya mama uweza kuingia kwa mtoto kupitia kwenye kondo la nyuma na kuweza kushambuliwa mtoto, ikiwa mama hatajulikanaa mapema kama ana ugonjwa huo mtoto anaweza kupata matatizo mbalimbali kama vile kuzaliwa akiwa kipofu au mtoto kufia tumboni.kwa hiyo ni vizuri kabisa akina Mama wakiwa wajawazito waweze kupima kaswende na iwapo mama akiwa na ugonjwa huo

 aanze matibabu mara moja.

 

2. Kwa kawaida ni vizuri kabisa akina mama wajawazito wanaoanza mahudhurio ya kliniki waweze kwenda na waume zao ili nao waweze kupima kaswende kwa sababu ukimtibu Mama pekee yake na huko na baba ana ugonjwa huo unakuwa umefanya kazi bure kwa hiyo ni vizuri kabisa kupima wote na wakigundulika wana ugonjwa huo ni vizuri kabisa kupewa dawa na wote waanze matibabu ili kuweza kunusuru maisha ya mtoto, pia kuna tatizo moja ambalo utokea ikiwa wote baba na Mama wamekuja kupima na wakagundulika wote wana maambukizi ni vizuri kabisa kuwashauri kabla ya kuwapima ili watoe hali ya kuanza kuulizana kwamba ni nani aliyeleta ugonjwa huu bali wote watibiwe na kuokoa maisha ya mtoto.

 

3. Pia  jinsi na njia ambazo uweza kusababisha kusambaa kwa kaswende kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, ya kwanza ni kufanya ngono zembe hali hii utokea pale mtu mwenye kaswende anapofanya ngono na mtu ambaye hana kaswende bila kupima afya zao na bila kutumia kondomu yaani ngono ya nyama kwa nyama, kwa hiyo watu wanashauliwa kama wanataka kufanya ngono zembe ni vizuri kabisa kupima afya zao ili kuweza kufahamu kama wana maambukizi au kama hawakuweza kupima ni vizuri kutumia kondomu, kwa hiyo jamii inapaswa kuelimika kuhusu ugonjwa huu hatari na kujihadhari kwa sababu madhara yake ni makubwa ingawa kwa bahati nzuri unatibika ila kinga ni nzuri  hasa hasa vijana wanapaswa kufahamu jambo hili kwa sababu wenyewe ndio tegemeo la taifa la kesho pia ndio wapo kwenye mategemeo ya kupata watoto wenye afya nzuri sio wenye kaswende na matatizo yote yanayohusiana na mambo kama hayo.

 

4. Njia ya pili ambapo ugonjwa huu unasambaa ni kujamiiana na mwanaume ambaye anajamiiana na wanaume wengine,

Tunavyojua kwa sasa hali ya ulimwengu ilivyo Kuna wanaume wanaojamiiana na wanaume wengine na pia huko ana mke mwenye mimba na anategemea kupata mtoto mwenye afya nzuri, kwa njia hii pia kaswende inaweza kueneza kutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanaume na kutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke na pia mwanamke kama ana mimba ana asilimia zote za kumwambikiza mtoto. Kwa hiyo ni vizuri kabisa kuachana na njia hizi za kujamiana hasa wanafamilia kama wanategemea kupata watoto kwa sababu hali kama hiyo ni hatari kwa familia na jamii nzima kwa sababu watoto wenye ulemavu wanapatikana na pia watoto wanapoteza maisha wakiwa mimba. Kwa hiyo jamii inapaswa kuelimika na kuhakikisha wanapunguza maambukizi ya kaswende hasa kwa wajawazito.

 

5. Pia wanawake wenye kiwango kikubwa cha virusi vya ukimwi,

Kwa kawaida mama akiwa na maambukizi na hatumii dawa inawezekana pengine anakuwa hajui kama ana maambukizi kwa sababu hajapima. Kwa kawaida mtu akiwa na maambukizi na kinga ya mwili inashuka kwa hiyo ni rahisi kabisa kupata maambukizi ya kaswende, kwa hiyo akina mama pindi wanapopata mimba ni vizuri kabisa kwenda kupima magonjwa hatarishi kwa mtoto na pia wasiende wenyewe ila waende na waume zao,na wakigundulika kwamba wana maambukizi ni vizuri kabisa kuanza matibabu mara moja ili kulinda afya ya mtoto.

 

6.Wanawake wenye wapenzi zaidi ya mmoja.

Pia na hili ni tatizo unaweza kukuta mwanamkea ana familia yake ana mme wake na pia ana wapenzi wengi nje na pia anajamiiana nao bila kinga ,na kuna wakati mwingine mama anakuwa ameshatoka kliniki kupima pamoja na mme wake na kukutwa hawana maambukizi ila mama anaendelea kutembea na wanaume wengi na bila mpangilio, kwa hiyo tunawasihi akina Mama wote wakishabeba mimba watulie na mme mmoja na hata kama labda mimba hiyo imepatikana bila matarajio au mama hana matunzo anapata matunzo kutoka kwa wanaume mbalimbali ila kwa usalama wa mtoto na kuepuka kupata mtoto wa ajabu atakayekutesa maisha yako yote ni vizuri kabisa kumlinda mtoto akiwa tumboni kwa kuachana nakutembea na wanaume wengi wakati wa ujauzito na kusababisha maambukizi ya kaswende kwa mtoto.

 

7. Napenda kuwashauri akina Mama na baba pia kwamba kaswende inatibika pindi ukipata ugonjwa huu ni vizuri kwenda hospitali kwa ajili ya matibabu na pia wazazi wanapaswa kuja madhara ya kaswende kwa mtoto ambapo mtoto anaweza kuzaliwa akiwa kipofu au na ulemavu wowote au pengine anaweza kuzaliwa akiwa mfu, na pia ugonjwa huu unaweza kukaa kwenye mwili wa mtu kwa mda mrefu kwa hiyo ni vizuri kabisa kupima afya mara kwa mara, na kwa upande wa vijana wanapaswa kulinda maisha yao kwa kuepuka maambukizi haya ambayo yanasababisha kuwepo kwa watoto wasiohitajika kwenye jamii pia kuacha ngono zembe na pia kuwa waaminifu kwenye mahusiano maana vijana ndilo taifa la kesho.



Sponsored Posts


  πŸ‘‰    1 Mafunzo ya html kwa kiswahili       πŸ‘‰    2 Hadiythi za alif lela u lela       πŸ‘‰    3 Magonjwa na afya       πŸ‘‰    4 Maktaba ya vitabu       πŸ‘‰    5 Mafunzo ya php       πŸ‘‰    6 Madrasa kiganjani    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Kazi ya homoni ya testosterone
Posti hii inahusu zaidi kazi ya homoni ya testosterone, hii homoni kwa kiwango kikubwa ukutwa kwa wanaume ndiyo homoni ambayo umfanya mwanaume aonekane jinsi alivyokuwa na sifa zake zote. Soma Zaidi...

image Sababu za za ugumba kwa Mwanaume
Post hii inahusu zaidi sababu za ugumba kwa Mwanaume, ni sababu ambazo umfanye mwanaume ashindwe kumpatia mwanamke mimba. Soma Zaidi...

image Jinsi mimba inavyotungwa na namna ambavyo jinsia ya mtoto inavyotokea
Posti hii hasa inahusu kasoro ,utatuzi,na jinsi ya kutunga mimba kwa upande wa mwanamke na mwanaumeΒ  .itatupelekea jinsi ya kuangalia kasoro na jinsi ya kutatua hizo kasoro katika jamii zetu. Soma Zaidi...

image Zijue sababu za kutobeba mimba
Posti hii inahusu zaidi sababu mbalimbali ambazo zinamfanya mama au dada kutobeba mimba. Kwa hiyo tutaziona hapo chini kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

image Vyanzo vya kuharibika kwa mimba ya miezi kuanzia 0-3
Posti hii inahusu zaidi vyanzo vya kuharibika kwa mimba kuanzia miezi zero mpaka miezi mitatu, kwa sababu hii ni miezi ya kwanza kabisa Kuna sababu au vyanzo vya kuharibika kwa mimba katika kipindi hiki. Soma Zaidi...

image Zijue sababu zinazosababisha kupungua kwa idadi ya mbegu za kiume
Kupungua kwa idadi ya mbegu za kiume kunamaanisha kuwa Majimaji (shahawa) unayotoa wakati wa kufika kileleni huwa na mbegu chache kuliko kawaida. Hesabu yako ya manii inachukuliwa kuwa chini kuliko kawaida ikiwa una chini ya mbegu milioni 15. Kuwa na idadi ndogo ya manii hupunguza uwezekano kwamba moja ya manii yako itarutubisha yai la mwenza wako, na hivyo kusababisha mimba. Hata hivyo, wanaume wengi ambao wana idadi ndogo ya manii bado wanaweza kuzaa mtoto. Soma Zaidi...

image Dalili za ongezeko la homoni ya estrogen
Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo mtu anaweza kupata ikiwa homoni ya estrogen imeongezeka, hizi dalili zikitokea mama anapaswa kuwahi hospital ili kuweza kupata matibabu au ushauri zaidi. Soma Zaidi...

image Dalili za uchungu
Uchungu wa uzazi hutokana na kubana nakuachia kwa misuli hii husababishwa kufunhuka kwa mlango wa tumbo la uzazi pamoja na shingo ya kizazi na kumuongezea mama uchungu wakati wa kujifungua(during labour) Pia kubana na kuachia huanza polepole wakati wa siku za mwisho mpaka mama atakapo fikia stage ya jifungu. Soma Zaidi...

image Mwanamke anatema mate mara kwa mara je inaweza kuwa ni ujauzito?
Ni kweli kuwa kutema mate mara kwa mara inaweza kuwa ni dlili za ujauzito. Lakini itambulije kuwa pekee sio kithibitishi cha ujauzito. Soma Zaidi...

image Changamoto za kwenye ndoa kwa waliotoa mimba mara Kwa mara
Posti hii inahusu zaidi changamoto za kwenye ndoa kwa wale waliotoa mimba mara Kwa mara,hizi ni changamoto za wakati wa kufanya tendo na mme wake au mtu mwingine kwa ajili ya kupata mtoto. Soma Zaidi...