Fahamu Ute unaotoka wakati wa ujauzito

Posti hii inahusu zaidi Ute unaotoka wakati wa ujauzito, kwa kawaida wakati wa ujauzito Kuna Ute ambao utoka na ni tofauti na kawaida pale mwanamke akiwa Hana mimba.

Fahamu Ute unaotoka wakati wa ujauzito.

1. Kwanza wakati wa ujauzito Kuna Ute ambao utoka na huwa ni mweupe kwa aina yake na ikitokea Ute huo ukawa na rangi tofauti na nyeupe kunakuwepo na maambukizi.

 

2. Ute huo uongezeka kwa sababu ya kuongezeka kwa homoni aina ya estrogen kwa sababu ya kufanya kazi mbalimbali kwenye mwili wa Mama wakati wa ujauzito kwa hiyo na Ute wakati wa ujauzito uongezeka zaidi.

 

3. Kwa upande wa akina Mama kama Kuna Ute wowote unaotoka wanapaswa kuwa makini Ili kuangalia ni Ute wa aje kwa sababu kama ni wa njano panakuwepo na maambukizi na hivyo ni vizuri kabisa kugundua na kuweza kupata matibabu.

 

4. Kwa sababu mabadiliko ya Ute usababishwa na hali yoyote iliyopo kwenye via vya uzazi kwa sababu kwenye via vya uzazi kama Kuna magonjwa kama vile kaswende na kisonono usababisha na rangi ya Ute kubadilika kwa hiyo kama Kuna aina yoyote ya mabadiliko ni vizuri kutafuta matibabu mapema na iwezekanavyo kwa sababu mtoto akipata maambukizi akiwa tumboni anaweza kupata shida ikiwepo kupoteza maisha.

 

5. Kwa upande wa akina Mama wajawazito hasa wanaochelewa kuanza clinic wanapaswa kuanza mara Moja Ili kuweza kupata vipimo mbalimbali kama vile vipimo vya magonjwa ya zinaa ikiwemo kaswende na Ukimwi, kwa kufanya hivyo hata kama mama hawezi kuangalia Ute wake hata kama una maambukizi anaweza kujua kama Kuna maambukizi kutokana na vipimo.

 

6. Kwa hiyo wajawazito wakiona Ute unaongezeka 

Wakati wa ujauzito wasishangae wajue kuwa ni kawaida kwa sababu ya kuwepo kwa mabadiliko ya homoni na hasa hasa Ute uongezeka wakati wa kukaribia kujifungua, kwa hiyo wasishangae ni kawaida tu na pakiwepo wasiwasi wowote ni vizuri kuwaona wataalamu wa afya Ili kuweza kupata matibabu zaidi.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/07/06/Wednesday - 04:21:31 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 15851


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-