Home Afya Shule ICT Burudani Dini Maktaba Maswali Madrasa Apps Blog Legacy Login

FAHAMU VITAMINI A NA KAZI ZAKE


image


Je na wewe i katika wale ambaowanahitaji kujuwa kuhusu Vitamini A, kazi zake na vyakula vya vitamini A. post hii inakwenda kukujuza zaidi pamoja na historia ya vitamini A.


VITAMINI A

Vitamini A ni katika vitamini fat soluble vitamin akama vile retinol, retinal, retinoic acid na beta-carotene. Vitamini A ni moja kati ya vitamini vingi. Vitamini vingine ni viamini b, C, D, E, K. unaweza kupata vitamini A sana kwenye mboga za majani za kijani, maini, mayai, maziwa, karoti na spinach. Katika makala hii tutakwenda kuona mengi kuhusu vitamini A, kazi zake, vyakula vya vitamini A pamoja na athari za upungufu wake mwilini:


 

Yaliyomo:
1.Maana ya vitamini A
2.Kazi za vitamini A
3.Vyakula vya vitamini A
4.Upungufu wa vitamini A
5.Athari za kuzidi kwa vitamini A


 

Maana ya vitamini A


Vitamini ni aina ya fat soluble vitamini ambayo ni kampaind ogania (organic compound) inayopatikana katika makundi kama retinol, retinal, retinoic acid na provitamin ambazo ni beta-carotene. Vitamini A ni muhimu katika ukuaji, uboreshwaji wa mfumo wa kinga na kuboresha afya ya macho.


 

Ugunduzi wa vitamini A umeanza toka miaya ya 1816 na Mwanasayansi aliyejulikana kwa jina la Francois Magendie alipokuwa akimfanyia uchunguzi mbwa mgonjwa. Baada ya hapo tafiti mbalimbali zikafata mwaka 1912, 1913, 1918, 1920 na 1939 na 1947. vitamini A vimepewa jina hili katika tafiti za mwaka 1920.


 

Kazi za vitamini A


1.Husaidia katika afya ya macho yaani kuona
2.Husaidia katika ukuaji
3.Husaidia katika kuboresha mfumo wa kinga mwilini
4.Husaiia katika ukuaji wa mimba na mtoto aliye tumboni
5.Husaidia katika afya ya mifupa
6.Husaidia katika afya ya ngozi
7.Husaidia katika afya ya meno
8.Husaidia katika utengenezwaji wa uteute mwilini.


 

Vyakula vya vitamini A


1.Maini
2.Karoti
3.Viazi vitamu
4.Spinachi
5.Maboga
6.Pilipili
7.Maembe
8.Njegere
9.Maziwa
10.Mayai
11.Mboga za majani za rangi ya kijani

 

Upungufu wa vitamini A


Tafiti zinaonyesha kuwa upungufu wa vitamini A huathiri watoto wanaokadiriwa kufikia 670,000 waliochini ya umri wa miaka mitano kila mwaka. Pia inakadiriwa kuwa watoto katika ya 250,000 na 500,000 wanakuwa vipofu katika nchi zinazoendelea kila mwaka. Tafiti zinathibitisha kuwa chanzo kikuu cha upofu kwa watoto ni upungufu wa vitamini A.


 

Athari za vitamini A kupitiliza


Endapo mtu atakuwa na vitamini A vingi ndani ya mwili hata vikapitiliza kiwango ambacho mwili unaweza kudhibiti, athari zifuatazo zinaweza kutokea:-
1.Mkusanyiko wa sumu mwilini
2.Kichefuchefu
3.Kuwshwa
4.Kukosa hamu ya kula
5.Kutapika
6.Kuona maluelue
7.Maumivu ya kichwa
8.Kupotea kwa nywele na misuli
9.Maumivu ya tumbo na uchovu



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    2 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    3 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    4 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    5 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    6 Hadiythi za alif lela u lela    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS

Imeandikwa na Mahede Tags AFYA , vyakula , ALL , Tarehe 2021-11-10     Share On facebook or WhatsApp Topic school Zaidi Dini AFYA ICT Burudani Tags Uzazi maswali Afya mengineyo dini HIV Sira vyakula Matunda HTML php Alif Lela 1 Alif Lela 2 FANGASI Dawa SQL Tips Quran Sunnah fiqh DARSA Magonjwa Tajwid tawhid simulizi Dua Academy Wahenga chemshabongo WAJUWA Michezo ICT Imesomwa mara 767



Post Nyingine


image Faida za kiafya za kula biringanya (eggplant)
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula biringanya eggplant) Soma Zaidi...

image Faida za vitamin C mwilini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vitamini C mwilini Soma Zaidi...

image Faida za kiafya za kunywa chai
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kunywa chai Soma Zaidi...

image fahamu kuhusu vitamini B na faida zake
makala hii inakwenda kukupa faida, kazi na athari za vitamini B mwilini. Nini hutokea endapo utakuwa na upungufu wa vitamini B mwilini? Soma Zaidi...

image Kazi za virutubisho vya protini mwilini
Somo hili linakwenda kukuletea kazi za virutubisho vya protini mwilini Soma Zaidi...

image Faida za kula magimbi (taro roots)
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula magimbi Soma Zaidi...

image Faida za kiafya za kula korosho
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula korosho Soma Zaidi...

image Faida za kiafya za kula nyama
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula nyama Soma Zaidi...

image Faida za kitunguu swaumu wakati wa ujauzito
Posti hii inahusu zaidi faida za kitunguu swaumu wakati wa ujauzito, kuna kipindi ambacho wanawake wakati wa ujauzito uchaguza vyakula mbalimbali kuna ambao wanaweza kutumia vitunguu saumu na kupata faida kubwa Soma Zaidi...

image Namna ya kuandaa mdalasini kwa ajili ya tiba.
Posti hii inahusu namna au njia za kuandaa mdalasini kwa ajili ya tiba ya homoni imbalance kwa wanawake. Soma Zaidi...