image

Fahamu vyakula vya nyuzinyuzi

Posti hii moja kwa moja inaenda kuelezea vyakula vya nyuzinyuzi zinazopatikana kwenye matunda na mboga mboga.

  Je, wafahamu kuwa matunda yanafaida nyingi mwilini? 

Moja kwa moja tuone matunda yanayokuwa na nyuzinyuzi na huwa na Faida gani;

 

1. Parachichi; hili Ni tunda lenye nyuzinyuzi na linasaidia uyeyushaji wa chakula tumboni hasa kwa wale wenye Matatizo ya Vidonda vya tumbo, Na nyuzinyuzi hizo Ni muhimu kukinga kuta za utumbo,. Pia husaidia watu wenye maradhi ya upungufh wa damu, kisukari, Matatizo ya mfumo wa Neva na maradhi mengine mengi watu hawa wanatakiwa kula tunda hili kwa wingi ili kuboresha Kinga ya mwili.

 

2.chungwa: nyuzinyuzi zinazopatikana kwenye chungwa huwa na vitamini C pia husaidia kuponesha Vidonda hivyo tunda hili ukilila kula pamoja na nyuzinyuzi zake tafuna mapaka zile kamba zake kwasababu zinasaidia usagaji wa chakula tumboni ( digestion) japo kuwa watu wengi hunyonya maji yalliyopo kwenye chungwa na kutupa nyuzinyuzi haishauriwi kula hivyo.

 

3.Embe;  tunda hili hiwa na nyuzinyuzi nyingi Sana ambazo huweza Kuzuia Saratani, pia huborasha Uwezo wa kumbukumbu na kufikiria kwa wingi hivyo watu tusipuuzie kula embe.

 

4. Nanasi: Ni tunda ambalo Lina sukari na Ni tamu Sana tunda hili Lina nyuzinyuzi ambazo Zina virutubisho vingi na vingine vinauwezo was kuupa mwili wAko Kinga dhidi ya Magonjwa tunda hili Lina vitamini C na madini ya chuma.

 

5. Ndizk mbivu; nyuzinyuzi za kwenye ndizi mbivu husaidia Sana Katika usagaji wa chakula tumboni,pia tunda hili Lina Uwezo wa kuimarisha nishati ya mwili. Mwili kuwa na nguvu na pia huweza kuongeza uzito. Hivyo hushauriwa kwa wale wenye uzito kupitiliza waepuka kutumia ndizi.

 

6. Papai; Hilo Ni tunda ambalo husaidia vitu vingi mwilini Kama vile kuua minyoo na kuondoa mazalia ya minyoo tumboni, na husaidia kwa wale wenye Vidonda vya tumbo Na kuboresha Kinga ya mwili.

 

Na je wafahamu kuwa mboga mboga Zina Faida nyingi mwilini?

 

Mboga mboga hasa za majani husaidia tumbo kusukuma uchafu wote tumboni hasa kwa wale wanaopenda kula vyakula vilivyokobolewa na vigumu kwani Magonjwa yote yanaanzia tumboni ndipo yanasambaa mwilini;.

 

1. Kabeji; ni mojawapo ha mboga yenye nyuzinyuzi ambayo hutibu Matatizo ya choo kigumu, na husaidia kuponesha haraka Vidonda vya tumbo vile vile husaidia kupunguza uzito uliozidi pamoja na kuondoa sumu mwilini.

 

2.Mchicha Hii pia Ni mboga ya majani ambayo Ina nyuzinyuzi nyingi na zinazosadia kuboresha mwili, Kinga ya mwili pia husaidia kwa wale wasioona endapo watatumia kwa wingi mboga hii.

 

3. Matembele; Ni mboga ambazo hupatikana kwenye majani ya viazi ambayo pia hutoa nyuzinyuzi matembele Yana vitamini A na vitamini C ambazo huimarisha Ngozi na fizi, endapo fizi zako zinatoa Damu Ni vyema kutumia matembele kwa wingi kwani husaidia kuponesha na pia mboga hii huwa na protini pia.

 

4. Spinachi; mboga hii pia Ina nyuzinyuzi ambayo Ina potassium kwa wingi, vitamini C na vitamini E ambazo zinasaidia kuimarisha afya ya Ngozi na pia kuimarisha Ngozi da Damu kuganda pia.

 

 Mwisho; hizi Ni baadhi ya mboga mboga na matunda yenye nyuzinyuzi Ila vyakula hivi Ni muhimu Sana endapo vikizingatiwa.           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/03/09/Wednesday - 06:55:28 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 5833


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Aina 20 za Vitamini, kazi zake, vyanzo vyeke na madhara ya upungufu wake
Katika post hii utakwenda kujifunza aina 20 za vitamini. Utajifunza kazu zake mwilini, vyanzo vyake na madhara yanayoweza kutokea kutokana na upungufu wake. Soma Zaidi...

Vyakula vya vitamin D
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya vitamin D Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Pilipili
Soma Zaidi...

Vyakula hatari kwa vidonda vya tumbo, na vyakula salama kwa vidonda vya tumbo
Makala hii inakwenda kufundisha vyakuna na vinjwaji salama anavyopaswa kutumia mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Pia utajifunza vyakula na vinywaji hatari kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Soma Zaidi...

Umuhimu wa kutumia maharage kwa wingi
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kutumia maharage kwa wingi, maharage ni aina ya chakula ambacho upatikanaji wake ni rahisi na watu wengi hawajui kwa ulaji wa maharage una faida kubwa sana mwilini kwa hiyo tunapaswa kuangalia faida za maharage kama ifua Soma Zaidi...

Faida za chungwa na chenza ( tangarine)
Somo hili litakwenda kukueleza kuhusu faida za chungwa na chenza mwilini Soma Zaidi...

Vyakula vya vitamini D na faida zake
Soma Zaidi...

Faida za biringanya/ eggplant
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za biringanya/ eggplant Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula pera
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula pera Soma Zaidi...

Nini maana ya protini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya protini Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Mahindi
Soma Zaidi...

Papai lililo iva ni salama kwa mama mjamzito au halifai
Papai ni moja kati ya matunda yenye vitamini C na virutubisho vinginevyo. Lakini papai pia ni moja kati ya vyakula ambavyo mjamzito anatakiwa awe makini navyo. Soma Zaidi...